Afisa wa Umoja wa Mataifa hapa nchini akana gari zilizotumia namba za UN huko Hai kwenye tukio la kushambulia walinzi wa Mbowe

Afisa wa Umoja wa Mataifa hapa nchini akana gari zilizotumia namba za UN huko Hai kwenye tukio la kushambulia walinzi wa Mbowe

Nifahamuvyo mimi matumizi yoyote mabaya ya alama (Emblems, Signs) za Umoja wa Mataifa au Shirika la Msalaba Mwekundu bila ruhusa ni kosa la kimataifa.

Vitani magari ya msalaba mwekundu hutumiwa kubebea silaha na king'ora kikizisindikiza kwenda ICU. Usisahau Tanzania tuko katika vita ya kiuchumi.
 
Mjiandae kwa miaka mitano ya kuendesha serikali bila mikopo na misaada kutoka kwa Wahisani na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa uhuni mlioufanya katika huu uchaguzi.
Kama hayo mashirika ni yakwako, hapo Sawa!!
 
Amenifurahisha alivyomalizia eti " the matter has been reported to the police " ngoja nicheke tu . Polisi hawa ambao hawajui had leo nani alimpiga lisu risasi . Ngoja niongeze k vant
 
Na Watalii hawatatia mkuu Nchini angalia anguko la makusanyo ya mapato. Nadhani vikwazo pia vinaweza kuhusu kutoruhusiwa kununua
wala kuuza chochote nje ya Nchi na pia External bank accounts zinawea kuwa FROZEN.
Mjiandae kwa miaka mitano ya kuendesha serikali bila mikopo na misaada kutoka kwa Wahisani na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa kwa uhuni mlioufanya katika huu uchaguzi.
 
Hii ilikua saa 8 na nusu usiku wa kuamkia leo. Huyu anayeonekana pichani aliyeshika bunduki si jambazi, si gaidi, si jinamizi. Ni Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Akiwa na genge lake la zaidi ya watu 20 walivamia hoteli ya kitalii ya Aishi Protea inayomilikiwa na Mhe.Freeman Mbowe ambapo waliwakamata wageni kadhaa walikuwemo hotelini hapo na kuwaweka rumande kituo cha polisi Bomang'ombe kwa madai kuwa wanapanga kuvuruga uchaguzi.

Pia aliwakamata walinzi wa hoteli hiyo na kuwapiga, kuwanyang'anya silaha na kuwasweka matambara mdomoni, kisha kuwachukua na kwenda kuwatelekeza porini kabla ya kufika uwanja wa ndege wa KIA. Wakati akitekeleza uhalifu huo alikua na magari yenye plate number za Umoja wa mataifa (UN) lakini UN imetoa taarifa kuwa magari hayo si yake.

Hii ina maana DC Sabaya alighushi namba za magari hayo kinyume cha sheria. Yani ameingiza nchi kwenye mgogoro wa kidiplomasia usio na tija kwa maslahi ya kisiasa.

#MyTake:
Hawa ndio watu ambao JPM anawapenda na anawalinda sana. Just like Bashite. Yani DC hana mafunzo yoyote ya kijeshi lakini anatembea na silaha ya kivita, anavamia hoteli bila kujali wageni waliopo. Anapiga walinzi, anawanyang'anya silaha, anawafunga mikono na miguu na kuwajaza matambara mdomoni. Kisha anaagiza wakatupwe porini. Saa 8 za usiku. Unyama gani huu?

Lakini hatachukuliwa hatua zozote za kinidhamu na mamlaka yake ya uteuzi. Labda kikubwa atakachopewa ni pongezi. Wanaojiita Viongozi wa dini hawatakemea na watajifanya hawajaona tukio hili. Wanaharakati nao watakaa kimya, lakini lingetokea Marekani wangepanua midomo kupayuka BlackLifeMatters. Afrika kuna unafiki mwingi sana.!

GJ Malisa

84899E40-F1A4-4055-98BA-839E687E55FF.png
 
Amemaliza kazi aliyotumwa apewe kazi ya waziri wa Mambo ya ndani
 

Attachments

  • FB_IMG_1603932400512.jpg
    FB_IMG_1603932400512.jpg
    17.8 KB · Views: 1
Usiombee hilo litokee maana hali ya uchumi ilivyo mbaya tutakoma kabisa
Hili sio la kuomba Ila watawala wanataka iwe hivyo kwa kiburi Chao.Maana maisha hata yawe magumu vipi wao maisha yatakuwa mteremko kwa upande wako tutakaoumia Ni sisi
 
Back
Top Bottom