Hii ilikua saa 8 na nusu usiku wa kuamkia leo. Huyu anayeonekana pichani aliyeshika bunduki si jambazi, si gaidi, si jinamizi. Ni Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Akiwa na genge lake la zaidi ya watu 20 walivamia hoteli ya kitalii ya Aishi Protea inayomilikiwa na Mhe.Freeman Mbowe ambapo waliwakamata wageni kadhaa walikuwemo hotelini hapo na kuwaweka rumande kituo cha polisi Bomang'ombe kwa madai kuwa wanapanga kuvuruga uchaguzi.
Pia aliwakamata walinzi wa hoteli hiyo na kuwapiga, kuwanyang'anya silaha na kuwasweka matambara mdomoni, kisha kuwachukua na kwenda kuwatelekeza porini kabla ya kufika uwanja wa ndege wa KIA. Wakati akitekeleza uhalifu huo alikua na magari yenye plate number za Umoja wa mataifa (UN) lakini UN imetoa taarifa kuwa magari hayo si yake.
Hii ina maana DC Sabaya alighushi namba za magari hayo kinyume cha sheria. Yani ameingiza nchi kwenye mgogoro wa kidiplomasia usio na tija kwa maslahi ya kisiasa.
#MyTake:
Hawa ndio watu ambao JPM anawapenda na anawalinda sana. Just like Bashite. Yani DC hana mafunzo yoyote ya kijeshi lakini anatembea na silaha ya kivita, anavamia hoteli bila kujali wageni waliopo. Anapiga walinzi, anawanyang'anya silaha, anawafunga mikono na miguu na kuwajaza matambara mdomoni. Kisha anaagiza wakatupwe porini. Saa 8 za usiku. Unyama gani huu?
Lakini hatachukuliwa hatua zozote za kinidhamu na mamlaka yake ya uteuzi. Labda kikubwa atakachopewa ni pongezi. Wanaojiita Viongozi wa dini hawatakemea na watajifanya hawajaona tukio hili. Wanaharakati nao watakaa kimya, lakini lingetokea Marekani wangepanua midomo kupayuka BlackLifeMatters. Afrika kuna unafiki mwingi sana.!
GJ Malisa