Africa Cup of Nations (AFCON) 2017, Special thread

Africa Cup of Nations (AFCON) 2017, Special thread

Hapa tunaongelea mpira..sasa la ugaidi sijui limekujaje tena, naona mada tunaihamishia kwenye ugaidi😀ndio maana soka letu haliendelei.
 
Siku ya jana timu ya taifa ya Misri imetinga fainali ya klabu bingwa Africa kwa kuinyuka Burkinabe kwa penati 4-3,mpambano huo uliisha kwa sare ya kufungana mabao 1-1 huku bao la Misri likifungwa dakika ya 63 na Mo Salah huku goli la kusawazisha la Burkinabe likifungwa dakika ya 73 na Aristide Bance ''sura ngumu ya kazi''.

bance.jpg


Shukran za pekee zimwendee kipa mkongwe Essam El Haddari (44yrs) aliyeokoa michomo miwili ya penati hivyo kuiwezesha timu yake itinge fainali ya 9 katika mashindano ya Afcon.Mapharaoh wa Egypt wanamsubiria mshindi wa leo kati ya Ghana na Cameroon.

Essam el Haddari (44yrs)

mechi 5
cleansheet 4
penati 2 kaokoa


4 clea.jpg



Egypt ndio timu pekee inayoongoza kwa mafanikio Afcon wakiwa wametwaa makombe 7 huku wakifuatiwa na Ghana&Cameroon ambao wana makombe 4 kila mmoja kisha Nigeria makombe 3.

Endapo Ghana au Cameroon akiingia fainali na kushinda basi atajiongezea makombe na kufikisha idadi ya makombe 5 na hivyo kumsogelea Pharaoh au endapo Egypt akishinda fainali atazidi kujiongezea gap ya makombe.

Egypt ilipotea katika soka la Africa miaka 5-6 iliyopita kutokana na machafuko ya kisiasa nchini kwao lakini wameweza kujipanga na kurudi katika ubora wao.Egypt hii ipo tofauti na Egypt ya akina Aboutrika,A.Fathi,Zidan, Misri ile ulikuwa unapigiwa pasi mpaka unachanganyikiwa muda wote unaelemewa golini kwako lakini Egypt hii wapo defensive sana.Egypt ile walikuwa wanajivunia sana katika eneo la kiungo lakini ya sasa eneo lao la kiungo la kawaida sana sio tishio kihivyo lakini nidhamu yao imewafikisha fainali .

Je Ghana au Cameroon watamzuia Pharaoh asiweke rekodi na asizidi kupaa juu kwa makombe.

Ghana=makombe 4
Cam=makombe 4

tukutane usiku wa leo Cameroon vs Ghana ...karata yangu nampa Ghana
 
Mi siumwi pole ya nini? Magaidi wanapondwapondwa na Trump
Sawa kbs !! sasa kama mgaidi ? ilikuwajee mliwashirikisha ktk michiano.. na iwejee muwe na ubalozi zao??! na vipi mnatumia Lugha zao?? jee ni wapi DT amemgusa au kumponda au kuvurumisha kombora kwa hao ..?!!
Pole sana!! tafadhali nenda ukajitibu....!!
 
Mohamed Aboutreka mchezani mahiri wa Egypt anatautwa kwa kosa la ugaidi

Kamanda kosa la mtu mmoja haliwezi sababisha tim nzima ichukiwe... kwanza hizo ni tetezi tu, hakuna ukweli wowote, na hata kama atakutwa na kosa atajijua yeye huko alipo,sisi hayatuhusu kabisa..hapa tupo kwa ajili ya whole team..so asikuumize kichwa
 
Sioni kama kuna wakuwazuia Mafarao kubeba hii ndoo,lets wait n see anything can happen...

Binafsi Ningeshauri tu kitim cha Ghana na kitim cha cameroon waungane waunde kikosi kimoja wakaenda kucheza na Mafarao angalau wafike hata matuta tu na hilo kama litawezekana😀😀
 
Burkina Faso wamekuwa washindi wa tatu Kombe la mataifa ya Afrika.
Burkina Faso 1 - 0 Ghana
[emoji460] A. Traore 89'
Full-Time #AFCON2017GABON#
 
Under 17 AFCON2017, GABON.

Group A
Gabon,
Ghana,
Cameroon
& Guinea

Group B
Tanzania,
Niger,
Angola
& Mali.
 
Nawatakia kila la heri Serengeti Boys iweze kushinda taji la U17 litalofanyika Mwezi wa 4 huko Gabon.

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
b80c511d0bf3b0d03eba8d8501c3771b.jpg
1584d9b6a9241136bda7445ff784aa0c.jpg
7ca164d33ec39b801bf7796cfe1fc6ee.jpg
 
Sioni kama kuna wakuwazuia Mafarao kubeba hii ndoo,lets wait n see anything can happen...

Binafsi Ningeshauri tu kitim cha Ghana na kitim cha cameroon waungane waunde kikosi kimoja wakaenda kucheza na Mafarao angalau wafike hata matuta tu na hilo kama litawezekana😀😀
Mkuu hii kasi walioanza nayo cameroon unaionaje lakini?
 
EGYPT 1-O CAMEROON

DAK 38

ILA HII GAME KIMSINGI NI KAMA IMEISHA TAYARI.

NAONA CAMEROON WAMESHAPOTEA TAYARI NA MUDA WOWOTE WANAONGEZWA.
 
Cameroon wanapaisha mipira leo sijui wamekula maharagwe ya wapi hawa!
 
77' Egypt 1-1 Cameroon
Mohamed Elnemy 24'
Samwel Nkoulou 60'
 
Back
Top Bottom