Siku ya jana timu ya taifa ya Misri imetinga fainali ya klabu bingwa Africa kwa kuinyuka Burkinabe kwa penati 4-3,mpambano huo uliisha kwa sare ya kufungana mabao 1-1 huku bao la Misri likifungwa dakika ya 63 na Mo Salah huku goli la kusawazisha la Burkinabe likifungwa dakika ya 73 na Aristide Bance ''sura ngumu ya kazi''.
Shukran za pekee zimwendee kipa mkongwe Essam El Haddari (44yrs) aliyeokoa michomo miwili ya penati hivyo kuiwezesha timu yake itinge fainali ya 9 katika mashindano ya Afcon.Mapharaoh wa Egypt wanamsubiria mshindi wa leo kati ya Ghana na Cameroon.
Essam el Haddari (44yrs)
mechi 5
cleansheet 4
penati 2 kaokoa
Egypt ndio timu pekee inayoongoza kwa mafanikio Afcon wakiwa wametwaa makombe 7 huku wakifuatiwa na Ghana&Cameroon ambao wana makombe 4 kila mmoja kisha Nigeria makombe 3.
Endapo Ghana au Cameroon akiingia fainali na kushinda basi atajiongezea makombe na kufikisha idadi ya makombe 5 na hivyo kumsogelea Pharaoh au endapo Egypt akishinda fainali atazidi kujiongezea gap ya makombe.
Egypt ilipotea katika soka la Africa miaka 5-6 iliyopita kutokana na machafuko ya kisiasa nchini kwao lakini wameweza kujipanga na kurudi katika ubora wao.Egypt hii ipo tofauti na Egypt ya akina Aboutrika,A.Fathi,Zidan, Misri ile ulikuwa unapigiwa pasi mpaka unachanganyikiwa muda wote unaelemewa golini kwako lakini Egypt hii wapo defensive sana.Egypt ile walikuwa wanajivunia sana katika eneo la kiungo lakini ya sasa eneo lao la kiungo la kawaida sana sio tishio kihivyo lakini nidhamu yao imewafikisha fainali .
Je Ghana au Cameroon watamzuia Pharaoh asiweke rekodi na asizidi kupaa juu kwa makombe.
Ghana=makombe 4
Cam=makombe 4
tukutane usiku wa leo Cameroon vs Ghana ...karata yangu nampa Ghana