Africa Kusini wasipoitoa ANC madarakani mapema itakuwa kama Haiti siku moja

Africa Kusini wasipoitoa ANC madarakani mapema itakuwa kama Haiti siku moja

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Majambazi na wezi wanakwida watu, wanawapukutisha hadharani na kufanya mauaji kiholela sana kama vile hakuna kitu kinaitwa police au magereza.
 
Sorry

Hivi watu weusi huko marekani wameendelea sawa na jamii zingine zilizopo huko marekani mfano jamii ya wazungu,wayahudi,wachina,wahindi ?

Kuna kitu nataka kuona hapa
 
ANC ndio dira sahihi kwa South Africa.

Alafu wewe jamaa unaonekana kama vile mwajiriwa wa CIA hapa nchini...
 
ANC ndio dira sahihi kwa South Africa.

Alafu wewe jamaa unaonekana kama vile mwajiriwa wa CIA hapa nchini...
Labda kama kwako dira sahihi ni kuwa taifa kinara katika ujambazi, mauaji, rushwa, ubakaji na maambukizi ya Ukimwi.
 
Sorry

Hivi watu weusi huko marekani wameendelea sawa na jamii zingine zilizopo huko marekani mfano jamii ya wazungu,wayahudi,wachina,wahindi ?

Kuna kitu nataka kuona hapa
Hawawezi kuendelea sawa na jamii nyingine kwa sababu wakati hizo jamii nyingine zinaendelea wao walikuwa watumwa mashambani na hawatambuliki kama binadamu.
 
Hawawezi kuendelea sawa na jamii nyingine kwa sababu wakati hizo jamii nyingine zinaendelea wao walikuwa watumwa mashambani na hawatambuliki kama binadamu.
O.k o.k o.k o.k wahindi walienda marekani kama watu gani ningependa kujua ?
 
Labda kama kwako dira sahihi ni kuwa taifa kinara katika ujambazi, mauaji, rushwa, ubakaji na maambukizi ya Ukimwi.
Afrika kusini kuna wageni wengi sana waliochukua uraia wa nchi hiyo, wengine ni raia wa kigeni ila wanaishi kihunihuni bila kuwa na maelezo ya kueleweka. Sasa kwa mazingira ya ile nchi kuna vitu huwezi kupambana navyo na kuvimaliza.
Pia suala la vyombo vya habari kama haupo makini vinaweza kukupoteza au kukuchota ukawa unatangaza ajenda za waliowatuma....
Makaburu wa afrika kusini wanajitetea alafu wanatetewa na nchi zao huko nje ambazo ni matajiri na wenye kauli kwenye taasisi za kimataifa hivyo usione ni kazi ndogo kudili nao.

Hivyo unaposema ANC imeshindwa nitakataa sababu ile nchi bado inafanya vyema kwenye mambo mengi.
 
Back
Top Bottom