Kama kuna mchezo unaochezwa, itakua kwa ushirikiano wa TISS na NIS ya Kenya, maana pale ilisemwa amelazwa kwetu hapa, hospitali yetu ingetoa press conference kukanusha, wewe kwa akili yako umevimbiwa ubwabwa hapo na kujiaminisha TISS itacheza mchezo kusema yuko Nairobi na NIS yetu wasijue kweli yupo au la.
Ikulu yetu iko kimya, hakuna hata kiongozi mmoja ametolea tamko, hospitali iko kimya.....nyie makajamba wa mtaani ndio mumechezewa gemu, na ili kuwadumaza ikachezwa ya kuzuia mahindi ili mkurupuke kama taifa na kuongea ongea lawama dhidi ya Kenya hadi ipite wiki moja au mbili ili muda upatikane wa kumpa mkulu wenu aibuke kuzindua kamradi sehemu na kuonyesha yupo yupo, sema naona imeshindikana na kuvuta muda sana zaidi ya walivyokisia na sasa zuio la mahindi limeondolewa.
Haya magemu huchezwa sana na hizi taasisi za intelijensia, kuna wakati hata CIA na KGB hushirikiana kwenye baadhi ya mambo.
Kuhusu wimbi la tatu au hata la kumi isikupe tabu maana walau kwetu tunafuatilia na kujuzwa, kwenu huko mumekaa mpo mpo tu hata hamna habari jua linachomozea wapi na kuzamia wapi, mumekaa kufuatilia nyuzi za tanzia tu.