Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 5,200
- 12,762
Mwalimu Nyerere aliwahi sema "Uchumi tunao, lakini tumeukalia' ithibati ya maneno ya Baba wa taifa ilikuwa sahihi kabisa, kwa kuzingatia baraka ya rasilimali asili na rasilimali watu katika bara letu la Afrika ni nguzo na mtaji muhimu wa kujiletea maendeleo, kwa kupitia vile vilivyo ndani yetu wenyewe.
Lakini kwa sababu ya upumbavu, ukosefu wa maarifa, ubinafsi na kupenda vya kupewa bure au vya nafuu mfano ni hii mikopo ya riba nafuu. Viongozi wetu wamekuwa makuwadi na madalali wa rasilimali zetu(Madini, gesi, Wanyamapori, misitu, ardhi nk) kwa mataifa ya kigeni, kwa kile wanachodai kudumisha ushirikiano katika sekta za kimkakati na kutafuta wawekezaji na uhisani.
Tabia hii ndio imezaa makongamano ambayo nchi zenye uchumi mkubwa mfano USA, Urusi, China nk wamekuwa wakiwaita viongozi madalali na makuwadi wa rasilimali za nchi zao, kwenda kusaini mikataba ya kinyonyaji, kifedhuli na kibaradhuli, pasi kuangalia maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Ni jambo la aibu, fedhea na dhihaka mtu kuwa katika utajiri halafu Kutwa kutembeza bakuli ughaibuni, huku ukitambua wazi kabisa kufanya hivyo ni kuuza uhuru wako, utu wako na watu wako, hili hata Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi (rip) wa Tanzania kashawahi sema.
Ni Afrika pekee ambayo viongozi wa nchi wanajisifu nchi zao kuwa na sifa ya kukopesheka badala ya kujisifu ni kwa namna gani matumizi bora ya rasilimali zilizipo katika nchi zao zimeweza kubadili maisha ya raia wao na mageuzi katika kila sekta na mwisho kutoa mikopo kwa nchi hitaki.
Na kitu kibaya zaidi nao baadhi ya wadau kutoka bara la Afrika na wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa, wanahoji na kulalamika juu ya kiwango kidogo Cha pesa kinachotolewa na mataifa makubwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimaendeleo barani Afrika, huu ni upumbavu na uzuzu.
Toka lini nguo ya kuazima kwa jirani ikawa yako milele? Au toka lini mpangaji wa vyumba akampagia kiwango cha Kodi Baba/Mama mwenye nyumba? Hawa ndo aina ya wasomi ambao bwana Denis Mpagaze aliwaandika katika kitabu chake cha "Wasomi Huru Gerezani"
Hakuna taifa duniani ambalo wananchi wake wanavuja jasho na damu kulipa Kodi kwa maendeleo ya taifa lao, wakubali kukupa pesa ya kufanya maendeleo makubwa wewe uliye mvivu wa fikra, kazi, ujuzi na maarifa. Mikopo yote toka nchi zenye uchumi mkubwa malipo yake ni kuchuma rasilimali muhimu kwa ajili ya ujenzi wa nchi zao, huku sisi tukibaki na mashino na mikataba ya kinyonyaji.
Hawa viongozi wetu ipo siku wakishamaliza kuuza rasilimali zote za asili, watageukia kuuza rasilimali watu.