Afrika hii tabia tutaacha lini?

Afrika hii tabia tutaacha lini?

Tuliongozwa na ........
Halafu akaja mwingine nae akasema " Sijui kwanini sisi masikini
Hao ndio walipewa nchi kucheka cheka tu
 
Naunga mkono hoja tena Mwalimu Nyerere alisisitiza hakuna umasikini mbaya kabisa kama umasikini wa fikra!. Jambo hili niliwahi kuliulizia Umasikini wa Afrika, Je tumelogwa?. Licha ya Kuongoza kwa Utajiri, Tuna Bilionea 1 tu kwenye Top Hundred Mabilionea wa Dunia. Ni Aliko Dangote Pekee!

P
Sisi tunao wataalamu tena wabobezi shida ni hii tabia ya walio pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data , yaani unyumbu, unyumbu ni tabia ya wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), anaye sema ukweli, (kujutia), jibu lake alienda porini kuchimba dawa
 
Mwalimu Nyerere aliwahi sema "Uchumi tunao, lakini tumeukalia' ithibati ya maneno ya Baba wa taifa ilikuwa sahihi kabisa, kwa kuzingatia baraka ya rasilimali asili na rasilimali watu katika bara letu la Afrika ni nguzo na mtaji muhimu wa kujiletea maendeleo, kwa kupitia vile vilivyo ndani yetu wenyewe.

Lakini kwa sababu ya upumbavu, ukosefu wa maarifa, ubinafsi na kupenda vya kupewa bure au vya nafuu mfano ni hii mikopo ya riba nafuu. Viongozi wetu wamekuwa makuwadi na madalali wa rasilimali zetu(Madini, gesi, Wanyamapori, misitu, ardhi nk) kwa mataifa ya kigeni, kwa kile wanachodai kudumisha ushirikiano katika sekta za kimkakati na kutafuta wawekezaji na uhisani.

Tabia hii ndio imezaa makongamano ambayo nchi zenye uchumi mkubwa mfano USA, Urusi, China nk wamekuwa wakiwaita viongozi madalali na makuwadi wa rasilimali za nchi zao, kwenda kusaini mikataba ya kinyonyaji, kifedhuli na kibaradhuli, pasi kuangalia maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Ni jambo la aibu, fedhea na dhihaka mtu kuwa katika utajiri halafu Kutwa kutembeza bakuli ughaibuni, huku ukitambua wazi kabisa kufanya hivyo ni kuuza uhuru wako, utu wako na watu wako, hili hata Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi (rip) wa Tanzania kashawahi sema.

Ni Afrika pekee ambayo viongozi wa nchi wanajisifu nchi zao kuwa na sifa ya kukopesheka badala ya kujisifu ni kwa namna gani matumizi bora ya rasilimali zilizipo katika nchi zao zimeweza kubadili maisha ya raia wao na mageuzi katika kila sekta na mwisho kutoa mikopo kwa nchi hitaki.

Na kitu kibaya zaidi nao baadhi ya wadau kutoka bara la Afrika na wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa, wanahoji na kulalamika juu ya kiwango kidogo Cha pesa kinachotolewa na mataifa makubwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimaendeleo barani Afrika, huu ni upumbavu na uzuzu.

Toka lini nguo ya kuazima kwa jirani ikawa yako milele? Au toka lini mpangaji wa vyumba akampagia kiwango cha Kodi Baba/Mama mwenye nyumba? Hawa ndo aina ya wasomi ambao bwana Denis Mpagaze aliwaandika katika kitabu chake cha "Wasomi Huru Gerezani"

Hakuna taifa duniani ambalo wananchi wake wanavuja jasho na damu kulipa Kodi kwa maendeleo ya taifa lao, wakubali kukupa pesa ya kufanya maendeleo makubwa wewe uliye mvivu wa fikra, kazi, ujuzi na maarifa. Mikopo yote toka nchi zenye uchumi mkubwa malipo yake ni kuchuma rasilimali muhimu kwa ajili ya ujenzi wa nchi zao, huku sisi tukibaki na mashino na mikataba ya kinyonyaji.

Hawa viongozi wetu ipo siku wakishamaliza kuuza rasilimali zote za asili, watageukia kuuza rasilimali watu.
"Black people are not complete human beings because THEY DON'T HAVE A GOOD BRAIN to govern the society as White people. They are still under the process of becoming the complete human beings."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Ni laana ya CCM, serikali ya Tanzania ina matumizi makubwa na ya anasa kuliko China, kuna Ikulu kila Wilaya zimejengwa kwa mabilioni eti za kulala Rais siku akitembelea kuna Wilaya mpaka anamaliza miaka 5 hajawahi kutembelea lakini kuna nyumba inamsubiri kulala siku akitembelea na hapo hapo kuna zahanati hazina dawa na watumishi, wizi na ujinga ndiyo maendeleo yetu.
"Let us agreed that Black people cannot rule themselves, Whites are born in order to rule and Blacks are born to be ruled.

Duh...!, yamekuwa hayo?.
P
Yap, matatizo yote haya ni sababu ya mifumo yenu ya hovyo, serikali ya Tanzania ina matumizi makubwa ya anasa kuliko serikali ya Marekani, bunge la Marekani lina kaa miezi 4 kujadili budget ya kutumika miezi 12? kuna misafara ya hovyo kama huku? kuna magari ya anasa kama Tanzania?
 
"Let us agreed that Black people cannot rule themselves, Whites are born in order to rule and Blacks are born to be ruled.

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
Mablack waonje Kwanza utawala wa kijeshi miaka 3 ili wanyoloke hakuna cha wabunge hapo jeshi mtaa kwa mtaa ole wako ukojoe kitandani hakuna mboko ni push ups na kichura chura
 
Huu ni upu
Ni laana ya CCM, serikali ya Tanzania ina matumizi makubwa na ya anasa kuliko China, kuna Ikulu kila Wilaya zimejengwa kwa mabilioni eti za kulala Rais siku akitembelea kuna Wilaya mpaka anamaliza miaka 5 hajawahi kutembelea lakini kuna nyumba inamsubiri kulala siku akitembelea na hapo hapo kuna zahanati hazina dawa na watumishi, wizi na ujinga ndiyo maendeleo yetu.
Huu ni upumbavu ambao mara kadhaa nimekuwa nikiupinga hapa JF,kwa serikali kupenda starehe na matumizi ya anasa mfano ni bajeti ya Tamisemi ya kununua magari ni kubwa kuzidi ya baadhi ya wizara kama ya biashara na Viwanda.
 
Naunga mkono hoja tena Mwalimu Nyerere alisisitiza hakuna umasikini mbaya kabisa kama umasikini wa fikra!. Jambo hili niliwahi kuliulizia Umasikini wa Afrika, Je tumelogwa?. Licha ya Kuongoza kwa Utajiri, Tuna Bilionea 1 tu kwenye Top Hundred Mabilionea wa Dunia. Ni Aliko Dangote Pekee!

P
Matendo yetu yamekuwa Sawa na maneno ya dhihaka toka kwa Kaburu Botha,kwamba hatuna akili ya kuongoza na kujiongoza.Yote haya sababu ya viongozi wetu wanao jali matumbo Yao tu.
 
Mablack waonje Kwanza utawala wa kijeshi miaka 3 ili wanyoloke hakuna cha wabunge hapo jeshi mtaa kwa mtaa ole wako ukojoe kitandani hakuna mboko ni push ups na kichura chura
Nchi kadhaa za Afrika mfano Nigeria,imepitia katika tawala nyingi za kijeshi,je,Kuna nini kilicho badilika zaidi ya kushamiri kwa rushwa.

Utawala wa kijeshi sio suluhu ya matatizo yetu,Sudan ipo katika utawala wa kijeshi,lakini hakuna amani na usalama.
 
Lengo watu waache kujitoa ufay
Nchi kadhaa za Afrika mfano Nigeria,imepitia katika tawala nyingi za kijeshi,je,Kuna nini kilicho badilika zaidi ya kushamiri kwa rushwa.

Utawala wa kijeshi sio suluhu ya matatizo yetu,Sudan ipo katika utawala wa kijeshi,lakini hakuna amani na usalama.
Lengo langu wanao pewa dhamana waache kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data, wewe unadhani nini kifanyike ili wanaopewa dhamana waache kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Mwalimu Nyerere aliwahi sema "Uchumi tunao, lakini tumeukalia' ithibati ya maneno ya Baba wa taifa ilikuwa sahihi kabisa, kwa kuzingatia baraka ya rasilimali asili na rasilimali watu katika bara letu la Afrika ni nguzo na mtaji muhimu wa kujiletea maendeleo, kwa kupitia vile vilivyo ndani yetu wenyewe.

Lakini kwa sababu ya upumbavu, ukosefu wa maarifa, ubinafsi na kupenda vya kupewa bure au vya nafuu mfano ni hii mikopo ya riba nafuu. Viongozi wetu wamekuwa makuwadi na madalali wa rasilimali zetu(Madini, gesi, Wanyamapori, misitu, ardhi nk) kwa mataifa ya kigeni, kwa kile wanachodai kudumisha ushirikiano katika sekta za kimkakati na kutafuta wawekezaji na uhisani.

Tabia hii ndio imezaa makongamano ambayo nchi zenye uchumi mkubwa mfano USA, Urusi, China nk wamekuwa wakiwaita viongozi madalali na makuwadi wa rasilimali za nchi zao, kwenda kusaini mikataba ya kinyonyaji, kifedhuli na kibaradhuli, pasi kuangalia maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Ni jambo la aibu, fedhea na dhihaka mtu kuwa katika utajiri halafu Kutwa kutembeza bakuli ughaibuni, huku ukitambua wazi kabisa kufanya hivyo ni kuuza uhuru wako, utu wako na watu wako, hili hata Rais wa awamu ya pili Mzee Mwinyi (rip) wa Tanzania kashawahi sema.

Ni Afrika pekee ambayo viongozi wa nchi wanajisifu nchi zao kuwa na sifa ya kukopesheka badala ya kujisifu ni kwa namna gani matumizi bora ya rasilimali zilizipo katika nchi zao zimeweza kubadili maisha ya raia wao na mageuzi katika kila sekta na mwisho kutoa mikopo kwa nchi hitaki.

Na kitu kibaya zaidi nao baadhi ya wadau kutoka bara la Afrika na wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa, wanahoji na kulalamika juu ya kiwango kidogo Cha pesa kinachotolewa na mataifa makubwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya kimaendeleo barani Afrika, huu ni upumbavu na uzuzu.

Toka lini nguo ya kuazima kwa jirani ikawa yako milele? Au toka lini mpangaji wa vyumba akampagia kiwango cha Kodi Baba/Mama mwenye nyumba? Hawa ndo aina ya wasomi ambao bwana Denis Mpagaze aliwaandika katika kitabu chake cha "Wasomi Huru Gerezani"

Hakuna taifa duniani ambalo wananchi wake wanavuja jasho na damu kulipa Kodi kwa maendeleo ya taifa lao, wakubali kukupa pesa ya kufanya maendeleo makubwa wewe uliye mvivu wa fikra, kazi, ujuzi na maarifa. Mikopo yote toka nchi zenye uchumi mkubwa malipo yake ni kuchuma rasilimali muhimu kwa ajili ya ujenzi wa nchi zao, huku sisi tukibaki na mashino na mikataba ya kinyonyaji.

Hawa viongozi wetu ipo siku wakishamaliza kuuza rasilimali zote za asili, watageukia kuuza rasilimali watu.
😭😭😭😭
 
Huu ni upu
Huu ni upumbavu ambao mara kadhaa nimekuwa nikiupinga hapa JF,kwa serikali kupenda starehe na matumizi ya anasa mfano ni bajeti ya Tamisemi ya kununua magari ni kubwa kuzidi ya baadhi ya wizara kama ya biashara na Viwanda.
Ndiyo hivyo mkuu, nchi imejaa rushwa kwenye ununuzi wa magari kuna rushwa kubwa sn
 
Back
Top Bottom