Afrika inaongozwa na wanasiasa uchwara

Afrika inaongozwa na wanasiasa uchwara

George Bush mtoto alikuwa mvuta bangi na hakuwa na matokeo mazuri chuoni, lakini alikuwa Rais wa Marekani kwasababu ya connections za wazazi wake. Tusijidharau!!
Kwa hiyo kwako George Bush unamwonaje?
Nadhani kati ya watu ambao Marekani itawakumbuka milele ni pamoja na yeye ndo maana alipewa 2 terms
 
Ukweli mchungu!

Nchi nyingi za Kiafrika, zinaongozwa na wanasiasa mbumbumbu. Hii wala haihitaji kutumia nguvu kubwa kulitambua. Fuatilia wanasiasa wetu wengi, elimu zao ni za kuunga-unga. Wengi wana viraka vya elimu. Wengi wako kwenye nafasi aidha kwa sababu ya mchango wa wazazi wao au walitumia rushwa kupata uongozi.

Hii hali inaziumiza sana nchi nyingi za Kiafrika maana viongozi wake wengi wanatokana na wanasiasa uchwara hawa hawa. Wengi hawana uzalendo wala uchungu kwa nchi zao. Wengi hawana uwezo hata wa kufikiria maslahi mapana ya nchi zao hata kwa miaka kumi tu mbele. Wengi ni wepesi wa visasi na wamejaa vinyongo.
Matokeo yake wengi hawana uzalendo wala uchungu kwa nchi zao. Ndiyo maana kila uchao maliasiri za bara ili zinasombwa na kupelekwa nje ya Afrika.

Nchi kama USA, UK, Germany, Israel, Russia n.k ili uwe kiongozi lazima kwanza uwe vizuri ghorofani (kichwani) na uwe umetoa mchango chanya kwa Nchi yako. Haiwezekani tu kujikuta umekuwa kiongozi ghafla. Na ikitokea hivyo, mfumo utafanya kila linalowezekana kukuondoa. Hawataki ujinga linapokuja suala la uzalendo kwa nchi zao.

Sasa matokeo ya kuwa na wanasiasa uchwara, tunapata pia viongozi uchwara ambao matokeo yake yanaonekana wazi kote barani Afrika! Wengi wa viongozi wa Kiafrika, wako kwenye nafasi zao kwa hisani kama si ya wazazi basi marafiki au rushwa. Matokeo yake wengi hawawezi kuwa na uchungu wala uzalendo kutokana na njia zilizotumika kwao kuwepo kwenye nafasi zao. Hivyo, badala ya kuhangaika na kujenga nchi zao, wengi wanakuwa wanahangaika kulipa fadhila au kuona ni namna gani watarudisha fedha walizotumia kupata huo uongozi.

Hivyo, nimalizie kwa kusema kwamba, ili Afrika iendelee, basi tuachane na mfumo huu mbovu tulionao wa kuwapata viongozi. Tuwe na mfumo imara wa kuchagua viongozi makini watakaotuwezesha kutuvusha kutoka katika mkwamo tulio nao sasa. Afrika ni bara lenye kila kitu. Halipaswi kuendelea kubaki kwenye lindi la umaskini kama ilivyo sasa.
Viongozi wenyewe akina Kigwangala na akina Salma Kikwete
 
Kama magu hii ndo inathibitisha Africa bado Sana matumizi ya nguvu bila akili.
 
Mstaafu mmoja alipata kusema URais au Uwaziri hausomewi !
Nikajua kumbe hivi vyeo ni vya bahati bahati tu na kujuana juana !
Kwakweli nilishindwa kumuelewa !
Wakati anamaliza muhula wake walijitokeza wanasiasa zaidi ya 40 kutoka kwenye Chama chake wakiutaka URais !! 🙏🙏
 
Sijui Mzee wa watu alikukosea nini hicho ambacho akisameheki!!
Anyway, sisi tunajadili walioko hai, waliokufa tuachane nao maana hawawezi kutusaidia kwa lolote na wala hawawezi kujitetea pia
Kama magu hii ndo inathibitisha Africa bado Sana matumizi ya nguvu bila akili.
 
Sijui Mzee wa watu alikukosea nini hicho ambacho akisameheki!!
Anyway, sisi tunajadili walioko hai, waliokufa tuachane nao maana hawawezi kutusaidia kwa lolote na wala hawawezi kujitetea pia
Ni moja ya viongozi uchwara nimemtaja ili kunakisha mada yako
 
Viongozi wa Africa ni wajinga wa kupindukia! limtu kama Paul Biya, Kisekedi, Tinubu,Mnangagwa, Kirr, Ndayishimiye na lile li Bongo walilolipindua kule Gabon.

Binafsi namkubali sana General Paul Kagame yule jamaa ni akili kubwa sana, kidogo na Hichilema wa Zambia na yule mtumishi wa Mungu wa Malawi H.E Lazarius Chakwera.
 
Huyu sawa wengine wote ni hewa tupu
 
Back
Top Bottom