Polisi nchini Afrika kusini imesema Imamu aliyejitangaza kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja Muhsin Hendricks, amepigwa risasi na kuuwawa na watu wasiojulikana. Imami huyo aliye na umri wa miaka 57 kutoka mjini Cape Town, alikuwa ndani ya gari na mwenzake kabla ya gari jengine ghafla kuegeshwa mbele yao na kuwazuwia.
Baadae watu hao waliokuwa wamefunika nyuso zao walimmiminia risasi na kumuua papo hapo. Sababu ya kuuwawa kwake hadi sasa hazijajulikana na polisi wanaendelea na uchunguzi.
Muhsin Hendricks aliyejitangaza mwaka 1996 kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, alikuwa akisimamia Msikiti wa Al-Ghurbaah, ulionuiwa kuwa eneo salama kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na jamii nyengine za kiislamu zilizotengwa.
Tangu wakati huo, kiongozi huyo wa kidini amekuwa akipokea vitisho dhidi yake, lakini akasema kwamba ni bora kuwa muwazi juu ya jinsia yake kuliko kuogopa kufa.
View attachment 3239255