- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook na Instagram, likidai kuwa taifa la Afrika Kusini limetoa orodha mpya ya nchi 22 za Afrika ambazo raia wake wanaruhusiwa kuingia nchini humo bila visa kwa madhumuni ya utalii, biashara au ziara fupi.
Chapisho hilo linaeleza kuwa muda unaoruhusiwa wa kukaa nchini Afrika Kusini ni kati ya siku 30 na 90, kutegemeana na uraia wa msafiri na aina ya pasipoti anayotumia.
Aidha, linadai kuwa raia wa nchi hizo wanaweza kusafiri kwenda Afrika Kusini bila kuomba visa kabla ya safari, mradi ziara yao iwe ndani ya muda unaoruhusiwa na watimize masharti ya kuingia nchini humo.
kando na hilo chapisho pia limesambazwa kupitia kiungo hiki,hiki
Je ni upi uhalisia wa chapisho hilo?

- Tunachokijua
- Kumekuwa na madai na sintofahamu kuhusu nchi za Afrika ambazo raia wake wanaweza kuingia Afrika Kusini bila kuhitaji visa. Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa madai ya kuwa kuna nchi Za Afrika zinaweza kuingia Afrika Kusini bila visa ni ya kweli.
Kwa mujibu wa Department of Home Affairs (DHA) ya Afrika Kusini, raia wa nchi zifuatazo za Afrika wenye pasipoti za kawaida (ordinary passports) wanaruhusiwa kuingia nchini humo bila visa kwa safari za muda mfupi:
- Angola
- Algeria
- Botswana
- Cabo Verde (Cape Verde)
- Comoros
- Eswatini
- Gabon
- Gambia
- Ghana
- Ivory Coast (Republic of Còte D’Ivoire)
- Kenya
- Lesotho
- Madagascar
- Malawi
- Mauritius
- Mozambique
- Namibia
- Seychelles
- Tanzania
- Tunisia
- Zambia
- Zimbabwe
Aidha, msamaha huu unahusu safari za muda mfupi pekee. Raia wanaokusudia kufanya kazi, kusoma au kuishi Afrika Kusini wanapaswa kuomba visa au kibali kinachofaa kabla ya kuingia nchini.