- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan nchini Afrika Kusini, zikidaiwa kuwaonyesha raia wa nchi hiyo kushindwa kufanya kazi za viwandani kufuatia kuondoka kwa idadi kubwa ya wahamiaji ambao hawakuwa na nyaraka halali za kuishi na kufanya kazi nchini humo.
- Tunachokijua
- Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan nchini Afrika Kusini, zikidaiwa kuwaonyesha raia wa nchi hiyo kushindwa kufanya kazi za viwandani kufuatia kuondoka kwa idadi kubwa ya wahamiaji ambao hawakuwa na nyaraka halali za kuishi na kufanya kazi nchini humo.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali za uthibitishaji wa taarifa, ikiwemo utafutaji wa maneno muhimu umebaini kuwa madai yanayoambatana na picha hizo yanapotosha na hayana ushahidi wa kuthibitisha kuwa picha hizo ni za matukio halisi.
Aidha, kuna viashiria vinavyoonyesha kuwa baadhi ya picha hizo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde . picha hizo zimeundwa kwa kutegemea matukio ya hivi karibuni nchini afrika kusini
Licha ya hivyo picha zimekuwa zikisambaa kuwaonyesha wakishindwa kufanya kazi ngumu ila madai hayo ynatumia picha zilizo undwa kwa kutumia akili unde
Sambamba na hilo, picha hizo zimeendelea kusambazwa wakati kukiwa na taarifa zilizoripotiwa na Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini SABC zikieleza kuwa baadhi ya viwanda katika eneo la KwaZulu-Natal vinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wafanyakazi, hali iliyochochea mijadala kuhusu athari za kuondoka kwa baadhi ya wafanyakazi wahamiaji.
hata hivyo baadhi ya picha zimesambazw kupitia hapa, hapa .