Utaelewa tu, mdogomdogo
Amani hulindwa kwa njia nyingi.Cha msingi uhakikishe amani inakuwepo.Amani haina njia moja ya kuilinda.Amani yaweza lindwa hata kwa risasi.Waliotoa tuzo wanajielewa na waelewa amani.Polisi na wanajeshi wanaitwa walinzi wa Amani zana zao za kuhakikisha amani inakuwepo ni pamoja na kutumia silaha zao. Zile silaha nazo sina mchango mkubwa sana kuhakikisha amani inakuwepo
Naona makamanda wameita kikao cha kamati kuu kwa dharura kutoa tamko la kupinga tuzo!
Fake NewsHeri wangempa Diamond au Alikiba
Acha upuuzi kwani we na mmeo mkimchikia jpm unadhani ni woteHakuna kitu kama hiki South Africa. Sio Mandela Peace Prize wala sio hiyo Mandela Institute. Na huyo Dr. Paul Kananura aliyetajwa ni mrwanda ambaye anaendesha ka small organization sijui wapi huko, wala sio Johannesburg. It is such a shame that in this day and age of technological advancement bado kuna watu wanadhani wanaweza kupotosha umma kwa habari za uongo. Halafu ma bloggers wengi wanadandia story bila kucheck authenticity.
Ndio amani yetu hiyoMhhh Hata kwenye mazishi ya wazalendo hatukufika (kutoa heshima za mwisho)
Tittle hii nimeipataje? Amani bila uchumi wala demokrasia ?
Kwa mtiririko huo wamemsahau Kagame ma Mseveni.Hapo kwa Nkrunzinza ndiyo wameharibu kabisa
Si lazima wote tuone nyekundu!Ushabiki wa kipuuzi utakufanya kudharaulika. Bado Kakobe yuko sahihi.
Si lazima wote tuone nyekundu!
Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.
Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.
"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).