Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.
Utaelewa tu, mdogomdogo

Kushabikia ujinga ni tatizo. Hivi unaweza kuona kwenye hizo tuzo yupo Nkurunzinza na bado ukatoka unashangilia rais wetu kuwepo? Hii aibu mnaitia nchi ni ajabu na kweli. Halafu huu upuuzi mnautumia kama sehemu ya kujifariji kwa kile alichokisema Kakobe juzi. Shida ukweli hauzuiliki kirahisi.
 
Amani hulindwa kwa njia nyingi.Cha msingi uhakikishe amani inakuwepo.Amani haina njia moja ya kuilinda.Amani yaweza lindwa hata kwa risasi.Waliotoa tuzo wanajielewa na waelewa amani.Polisi na wanajeshi wanaitwa walinzi wa Amani zana zao za kuhakikisha amani inakuwepo ni pamoja na kutumia silaha zao. Zile silaha nazo sina mchango mkubwa sana kuhakikisha amani inakuwepo

Hiki ulichoongea kinaonyesha ni jinsi gani mnaendesha maisha yenu kwa kutetea uovu. Bado Kakobe yuko sahihi na ukweli utabaki kuwa ukweli. Huwezi kizuia ukweli kwa kutumia uongo
 
Hakuna kitu kama hiki South Africa. Sio Mandela Peace Prize wala sio hiyo Mandela Institute. Na huyo Dr. Paul Kananura aliyetajwa ni mrwanda ambaye anaendesha ka small organization sijui wapi huko, wala sio Johannesburg. It is such a shame that in this day and age of technological advancement bado kuna watu wanadhani wanaweza kupotosha umma kwa habari za uongo. Halafu ma bloggers wengi wanadandia story bila kucheck authenticity.
Acha upuuzi kwani we na mmeo mkimchikia jpm unadhani ni wote
 
Huu ni uongo mwenye uthibutisho hii tuzo imetoka atuwekee link hapa vinginevyo ni sawa na kujamba alafu mnaziba pua wenyewe!
 
Hii habari ina walakini. Uwalakini wake ni kuonekana kwenye tovuti moja tu duniani kote ya azaniapost.com. Kadhalika, uwalakini wake upo kwa Nkurunzinza kupewa tuzo hiyo inayodaiwa kuwa ni ya Mandela. Na kama hii habari ingekuwa ya kweli, hakika nawaambia, gazeti fulani hivi lingeiandika habari hii kila kurasa ya toleo lake la leo, na hata kesho na hadi Jumatatu ya mwaka mpya. Sijajua hao walioitoa habari hii walikuwa wana dhamira gani? Nakumbuka kuna wakati kuna watangazaji wa TBC walifukuzwa kazi kwa kudai Rais Magufuli amesifiwa na Donald Trump, ila wanahabari wale walirudishwa kazini kwa parole ya Rais. Ha ha ha ha ha ha Ha.
 
Nkurunzinza naye kazawadiwa? Angalieni hizo tuzo badala ya ku-promote democracy ndo zikawa zinaididimiza
Afu yy si kapewa ya ujasiri ( Mandela courage) so ataendeleza ubabe wake maana huo ndo ujasiri unaompa hizo tuzo
 
Hizi tuzo zingine bwana..nielekezeni namna ya kufungua kesi kupinga huyu mtu kupewa tuzo..hakustaili kabisa na vielelezo vya kwanini nakataa hii tuzo asipewe ninavyo..SISI RAIA NDO TUNATUNZA AMANI NA WALA SIYO YEYE.umetubomolea nyumba tumekaa kimya mnapiga watu risasi tumekuvumilieni..watu wanaokotwa kwenye mifuko bahari bado tunavumilia..waandishi wanapotezwa na wasiojulikana bado tunavumilia..na SASA TUKISEMA UFUATE KATIBA ULIYOAPA KUILINDA UNAYOVUNJA KILA SIKU UNATUITA WACHOCHEZI..NGOJA CKU HAO WACHOCHEZI WATAKAPOAMUA KUPLAY PARTY YAO YA UCHOCHEZI KAMA AMANI ITAKUWEPO
 
Si lazima wote tuone nyekundu!

Ni kweli ila uwe na aibu. Haiwezekani uone tuzo bila kujali ni za kweli au uongo zinamuhusisha na Nkuruzinza kisha ushabikie kwamba hata rais wetu kapata. Kama una akili timamu unapaswa kutia shaka.
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).



Hizo tuzo ziktakuwa za mtaa wa Lumumba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom