Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe tindo unafikiri siasa zenu maji taka za hapa bongo unataka kuzivusha nje ya mipaka?Kushabikia ujinga ni tatizo. Hivi unaweza kuona kwenye hizo tuzo yupo Nkurunzinza na bado ukatoka unashangilia rais wetu kuwepo? Hii aibu mnaitia nchi ni ajabu na kweli. Halafu huu upuuzi mnautumia kama sehemu ya kujifariji kwa kile alichokisema Kakobe juzi. Shida ukweli hauzuiliki kirahisi.
hivi hujui anaogopa kuona maiti mubashara huyooooooMhhh Hata kwenye mazishi ya wazalendo hatukufika (kutoa heshima za mwisho)
Tittle hii nimeipataje? Amani bila uchumi wala demokrasia ?
Hata huko Kenya wanabeza Uhuru kupewa tuzo, wanadai kwa Magufuli wamepatiaKwa kinyata uhuru wamepatia
Ukunielewa hapo imetumika fasihi ndo maana nikasema kuna mtu alisema "Miafrika ndivyo tulivyo"Kwa hiyo malikia akikuambia ww ni mpumbavu utafurahia coz yeye ni mzungu?
Wewe tindo unafikiri siasa zenu maji taka za hapa bongo unataka kuzivusha nje ya mipaka?
Wale waliochagua hawa viongozi na kuwapa tuzo si model yenu, ni watu wabobezi wa siasa za kimataifa.
Sasa Wewe endelea kukaririshwa na Dutch welle, mliambiwa Gaddafi mbaya wanaingia kuikomboa Libya, matokeo yake Sasa Libya ndo hiyo imekombolewa, vyombo vya kimagharibi hata kuripoti kinachoendelea huko wanaona aibu baada ya Kuisambaratisha nchi hiyo
Akili ya kuambiwa changanya na zako
hacha usengeHizo tuzo za ki bwege tu!
![]()
Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.
Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.
"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).
Mkuu, hizi habari mlitengeneza kwa nia gani? Kwanini mnacheza na taasisi ya urais?Magufuli ni chaguo la Mungu wasiopenda wahame nchi maana bado ana miaka 7 ya kuingoza nchi hii
Bwana vita ni lini alisuluhisha Sudan Kusini?
Sasa wewe hata spelling tu ni shida tena kwa kiswahili sijui nikuweke wapi mwanangu wa tisa.U missed the point..Ngoja kiloba kikiisha kichwani utafakari upya.
mmmmmmmmmmWakfu wa Nelson Mandela umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo za “Nelson Mandela”, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari Tanzania, Kenya na Burundi Disemba 27, 2017. Habari hiyo pia haikutajwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Swahili Times on Twitter
Source:Swahili Times Twitter
Ushauri wangu:Vyombo vya habari nchini viwe vinajiridhisha kama habari ina ukweli wasikimbilie kuwa wa kwanza kuripoti,kuna media kubwa tunazoziamini nazo ziliingia ktk mkumbo huo wa kutoa fake news.
Tatizo la Nkurunzinza ni Nini, ina maana Wewe unamjua Nkurunzinza kuliko hao jamaa?Nina uelewa wa kutosha, najua kipi kinatangazwa kwa usahihi na kipi kinatangazwa kwa kupakana matope. Ila kushabikia rais wetu kupewa tuzo na taasisi ambayo na Nkurunzinza kapewa pia huu ni ujuha.
Huo mfano wa suala la Gadaffi na Libya hebu liache maana najua viwango vyako vya uelewa, utaishia kujichanga tu. Hebu tubaki kwenye haya ya kwetu unayoyafahamu wangalau tutaelewana hata kama hatutakubaliana.