Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Tetesi: Afrika Kusini: Rais Magufuli adaiwa kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize)

Status
Not open for further replies.
Mbona hizi habari zimekanushwa kwamba sio kweli na huo mchakato haujafanyika???
 
Kushabikia ujinga ni tatizo. Hivi unaweza kuona kwenye hizo tuzo yupo Nkurunzinza na bado ukatoka unashangilia rais wetu kuwepo? Hii aibu mnaitia nchi ni ajabu na kweli. Halafu huu upuuzi mnautumia kama sehemu ya kujifariji kwa kile alichokisema Kakobe juzi. Shida ukweli hauzuiliki kirahisi.
Wewe tindo unafikiri siasa zenu maji taka za hapa bongo unataka kuzivusha nje ya mipaka?
Wale waliochagua hawa viongozi na kuwapa tuzo si model yenu, ni watu wabobezi wa siasa za kimataifa.

Sasa Wewe endelea kukaririshwa na Dutch welle, mliambiwa Gaddafi mbaya wanaingia kuikomboa Libya, matokeo yake Sasa Libya ndo hiyo imekombolewa, vyombo vya kimagharibi hata kuripoti kinachoendelea huko wanaona aibu baada ya Kuisambaratisha nchi hiyo

Akili ya kuambiwa changanya na zako
 
Mhhh Hata kwenye mazishi ya wazalendo hatukufika (kutoa heshima za mwisho)

Tittle hii nimeipataje? Amani bila uchumi wala demokrasia ?
hivi hujui anaogopa kuona maiti mubashara huyoooooo
 
Kwa hiyo malikia akikuambia ww ni mpumbavu utafurahia coz yeye ni mzungu?
Ukunielewa hapo imetumika fasihi ndo maana nikasema kuna mtu alisema "Miafrika ndivyo tulivyo"
 
Wewe tindo unafikiri siasa zenu maji taka za hapa bongo unataka kuzivusha nje ya mipaka?
Wale waliochagua hawa viongozi na kuwapa tuzo si model yenu, ni watu wabobezi wa siasa za kimataifa.

Sasa Wewe endelea kukaririshwa na Dutch welle, mliambiwa Gaddafi mbaya wanaingia kuikomboa Libya, matokeo yake Sasa Libya ndo hiyo imekombolewa, vyombo vya kimagharibi hata kuripoti kinachoendelea huko wanaona aibu baada ya Kuisambaratisha nchi hiyo

Akili ya kuambiwa changanya na zako

Nina uelewa wa kutosha, najua kipi kinatangazwa kwa usahihi na kipi kinatangazwa kwa kupakana matope. Ila kushabikia rais wetu kupewa tuzo na taasisi ambayo na Nkurunzinza kapewa pia huu ni ujuha.

Huo mfano wa suala la Gadaffi na Libya hebu liache maana najua viwango vyako vya uelewa, utaishia kujichanga tu. Hebu tubaki kwenye haya ya kwetu unayoyafahamu wangalau tutaelewana hata kama hatutakubaliana.
 
magufuli+pic.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wawania tuzo 4,956. Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Pia, Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.

Rais wa Taasisi ya Mandela, Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

"Hii inaonyesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya,” amesema Dk Kananura. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

Ikiwa Mugabe, Museveni na Kagame hawajapewa hizi Tuzo basi watakuwa hawajatendewa haki hata kidogo![emoji41]
 
Wakfu wa Nelson Mandela umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo za “Nelson Mandela”, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari Tanzania, Kenya na Burundi Disemba 27, 2017. Habari hiyo pia haikutajwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Swahili Times on Twitter

Source:Swahili Times Twitter

Ushauri wangu:Vyombo vya habari nchini viwe vinajiridhisha kama habari ina ukweli wasikimbilie kuwa wa kwanza kuripoti,kuna media kubwa tunazoziamini nazo ziliingia ktk mkumbo huo wa kutoa fake news.
 
U missed the point..Ngoja kiloba kikiisha kichwani utafakari upya.
Sasa wewe hata spelling tu ni shida tena kwa kiswahili sijui nikuweke wapi mwanangu wa tisa.

Elimu ya kiLOba itakuachaje hapa duniani?
 
Kazi ya tbc km kaiwaida yao wazee wakuandaa fake news kwajili ya kumsifu mfalme mwenye enz
 
Wakfu wa Nelson Mandela umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo za “Nelson Mandela”, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari Tanzania, Kenya na Burundi Disemba 27, 2017. Habari hiyo pia haikutajwa na vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Swahili Times on Twitter

Source:Swahili Times Twitter

Ushauri wangu:Vyombo vya habari nchini viwe vinajiridhisha kama habari ina ukweli wasikimbilie kuwa wa kwanza kuripoti,kuna media kubwa tunazoziamini nazo ziliingia ktk mkumbo huo wa kutoa fake news.
mmmmmmmmmm
 
CCM iko mwishoni sasa, watatupisha katika vipindi vigumu sana ila ni vifupi..
 
Nina uelewa wa kutosha, najua kipi kinatangazwa kwa usahihi na kipi kinatangazwa kwa kupakana matope. Ila kushabikia rais wetu kupewa tuzo na taasisi ambayo na Nkurunzinza kapewa pia huu ni ujuha.

Huo mfano wa suala la Gadaffi na Libya hebu liache maana najua viwango vyako vya uelewa, utaishia kujichanga tu. Hebu tubaki kwenye haya ya kwetu unayoyafahamu wangalau tutaelewana hata kama hatutakubaliana.
Tatizo la Nkurunzinza ni Nini, ina maana Wewe unamjua Nkurunzinza kuliko hao jamaa?
Sasa underline list ubaya wa Nkurunzinza unaoujua ambao hao jamaa hawaujui mpaka wakaamua kumpa tuzo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom