Afrika mashariki na afrika kwa ujumla Tanzania kuongoza kuwa na reli ya kisasa ya umeme.

Afrika mashariki na afrika kwa ujumla Tanzania kuongoza kuwa na reli ya kisasa ya umeme.

Wakenya niwatu wahovyo kuwahi kutokea Duniani!!
Wivu na ujuaji vimewatawala
na kila kizuri wao hutamani kiwe chao pekee!!
hili limevuka mipaka
kupelekea hata kumuonea wivu mkenya mwenzie,
Asifanikiwe Mjaluo
mkikuyu Hutokwa na povu!!

Ila kwa awamu hii ya Magu Lazima wakae
ndo maana tumewatosa AU! thanks to Museveni's advice
 
Hapa bavicha hutawasikia.....wanasubiria mradi ukwame waje na pumba
Mimi ni Pro-Bavicha 100% ila nnajivunia utekelezaji wa miradi kama hii ya kimaendeleo,kwa maana kwa miaka mingi hichi ndicho kilichowafanya ccm watuchukie! Sisi ni watu wa kudai yale ambayo ni haki ya watanzania wote na ambayo tuna imani kuwa yapo ndani ya uwezo wa serikali,kwa mradi huu hata ungeniambia nipunguze bajeti ya mlo wa familia yangu ili kuchangia mradi huu NIPO TAYARI!! Wala hutauona UBAVICHA wangu hapo! Hata kama ningeambiwa kuwa nitakufa kesho bado nina hamasa ya kuona mradi huu unafanikiwa,ili watoto na wajukuu wangu waje kujua ni nini baba na babu yao alikuwa akipigania enzi zake alipodharaulika kwa UBAVICHA wake!! Kwa maana nchi isipokuwa Nna maendeleo hata watoto na wajukuu zetu watatudharau kwa kushindwa kuibana serikali ya ccm na kupelekea maccm kujinufaisha huku yakiiacha nchi ikiwa hoi taabani!! Hivyo kama kuna mahali Bavicha wanahitajika kujitoa kwa hali na mali ni kwenye miradi ya aina hii!! MIMI NIPO TAYARI!
 
Wote tunafurahi nchi yetu ikisonga mbele ila dizaini yako ya kuchekacheka na kuandikaandika kama chizi inaboa!! Ficha upumbavu wako!
Ukiona nimekuboa ujue ujumbe umekupata.
 
Nimejaribu kuvuta picha baada ya hiyo reli nakaona fahari kwa Tanzania yangu lakin nikajiuliza tena huo umeme wa uhakika kiasi hicho tunao?
 
Yaani unanichekesha sana. Yaani kenya muwe na train ya speed 240km/hr kwa reli ipi hiyo!!? Mbona kona za reli hiyo kali sana?? Au hujasoma physics. Yaani mkiwa na hiyo train sisi TZ tutakuwa na train ya Jet engine.
Train ya jet engine? Are you even listening to yourself? A jet engine train was tried in France over 100 years ago and it failed. These days people talk of MAGLEV technology which you obviously are not cognizant with.
 
Morocco.And they bought second hand trains ,sioni nini tanzania wanasema ,read reports and see ethiopia is the first ...tayari wana electric railway kutoka djibouti soo the fact that tanzania hata construction ya reli bado haija commence ...ni manaongoza ...tayari morocco wana trains ..nyinyi hata reli na stima yenyewe hamna
 
Wewe uko nyuma sana mambo ya ulimwengu kaa kimya. South Africa ina standard Gauge siku nyingi sana.
Kenya imepata juzi Ethiopia siku nyingi
 
AnkaraKonya.jpg
Kampuni zilizotiliana saini makubaliano hayo na Serikali ni ya ubia kati ya YAPI MERKEZI ya uturuki na MOTA-ENGIL AFRIKA ya ureno kwa grahama ya dola zaidi ya bilioni moja za kimarekani.

Akishuhudia utiliaji saini uliofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi wa reli hiyo itayotumia umeme na kwenda kwa spidi ya kilometa 160 kwa saa itakuwa ni ya kwanza kwa Afrika ikifuatiwa na nchi ya Morocco.

“Tunataka kuifanya nchi yetu iwe ndogo kwa kutumia miundombinu ya kisasa ndio maana Serikali imeamua kujenga reli hii itakayotumia umeme na kwenda spidi kubwa kuliko nyingine zote barani Afrika”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa ujenzi wa reli hiyo utaongeza chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na kubainisha kuwa Safari ya Dar hadi Moro itatumia muda wa saa 1:16 wakati Dar hadi Dodoma itatumia muda wa saa 2:30 na safari ya Dar had Mwanza itatumia muda wa saa 7:30.
train-jpg.466922


Aidha, Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa gharama za ujenzi wa reli hiyo haitakuwa sawa na mikoa mingine kutokana na kutofautiana na hali ya jiografiia kwenye mikoa ambapo reli hiyo itapita.

Kuhusu kukamilisha mradi huu, Waziri Prof. Mbarawa ameahidi kuongeza bajeti ya ujenzi wa reli hiyo kwa mwaka ujao wa fedha na kuendelea kutafuta mkopo wa gharama nafuu ili kufanikisha ukamilishawaji wake.

Waziri Prof. Mbarawa amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kuomba zabuni zIlizotangazwa hivi karibuni za ujenzi wa reli hiyo kwa awamu nyingine kutoka Morogoro-Makotopora KM 336, Makotopora-Tabora KM 294, Tabora-Isaka KM 133 na Isaka hadi Mwanza KM 248 ambazo zinatarajiwa kufunguliwa mwezi Aprili mwaka huu na kuahidi kuwa utaratibu wake utatendeka kwa uwazi na haki.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo utajengwa kwa muda wa miezi 30 kutokea sasa na kuhusisha ujenzi wa miundombinu ya umeme, Stesheni sita za abiria na sita za kupishani treni na ujenzi wa wigo wa KM 102 kwa usalama wa watu na magari.

Kwa upande wake Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yassemin Eralp ameiahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali katika mradi huo mkubwa na kuupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano katika kufanikisha maendeleo kwa wananchi wake.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Kabla ya kuropoka chunguza kwanza
 
Back
Top Bottom