Huwa nasikia watu wanamsifia Magufuli eti ni Baba wa Barabara/Mabarabara, hakutaka Demokrasa Nchini eti yeye ni Hapa kazi tu.
Lakini hakuna kazi hata moja alofanya inatambulika kwa watu wenye akili zao wanaojua nzuri na au maendeleo ni nini.
Your browser is not able to display this video.
Hayati Magufuli alivyokuwa anajisifia hadi kujiita Askari wa Mwamvuli kwa kufanya kazi ya barabara vizuri
Umasikini Ujinga na Maradhi; Kundi la Wajinga likapumbaza Taifa eti Hayati ni Mchapa kazi kajenga barabara, sijui Nchi iliibiwa sana hivyo kaongea na Barrick watalipa Kodi trilioni zaidi ya 347, huku bajeti ya nchi kwa mwaka ikiwa haifiki trilioni 40.
Haya mambo ya kumsifia hayati Magufuli tuwaachie Wananchi wa Chato japo hajawahi kuwa hata balozi wao wa nyumba kumi.
Mungu anajibu maombi.
Top 11 African Countries With Quality Road🛣
1: Namibia🇳🇦 (score 5.2) world ranking 23
2: Egypt 🇪🇬(Score 5.0)world ranking 28
3: South Africa🇿🇦 (score 5.0) world ranking 29
4: Rwanda🇷🇼 (score 5.0) world ranking 31
5: Ivory Coast🇮🇪 (score 4.7) world ranking 42
6: Mauritius🇲🇺 (score 4.7) world ranking 44
7: Morocco🇲🇦 (score 4.4) world ranking 55
8: Kenya🇰🇪 (score 4.2) world ranking 61
9: Botswana🇧🇼 (score 4.1) world ranking 64
10: Cape Verde🇨🇻 (score 4.1) world ranking
11: Senegal🇸🇳 (score 4.0) world ranking 71
🌐Source: World Economic Forum’s Global Competitiveness Report Index
Namibia sijawahi fika ila niliangalia youtube wale jamaa wana barabara yaan huko watu wanakandamiza kibati mpaka mwisho maana barabara zimenyoooka km rula
Namibia sijawahi fika ila niliangalia youtube wale jamaa wana barabara yaan huko watu wanakandamiza kibati mpaka mwisho maana barabara zimenyoooka km rula
Aibu sana sana kwa nchi yetu speed kuwa 80 kwa zaidi ya 90% ya barabara zetu,yan hata kimara-kibaha highway eti unakuta vibao vya speed 50!tanroad pale sijui wazee wengi ambao hata nje ya nchi hawajatoka kuangalia wenzetu wanavyofanya kwenye barabara!yan tuta tuta na speed limit 80 wanachojua wao!
Uliyemtaja ni awamu ya 5 ,umesema hajafanya kitu,hao wengine mbona huwazungumzii?Nchi ulizotaja hapo hizo barabara zilijengwa ndani ya awamu moja au mbili?Ujenzi wa nchi ni mchakato.Siyi jambo la kuamka na mtu mmoja ghafla tu na kutimiza.Sema chama Tawala kwa zaidi ya miaka 40 na awamu zaidi ya nne bado inasua sua katika ujenzi wa nchi kulinganisha na nchi nyingine Afrika.
Kwa maana ya quality roads, Tanzania haiwezi kuingia kabisa. Hizi barabara zinazojengwa na Wachina zinazojaa mashimo baada ya mwaka mmoja (nyingine chini ya miezi 6), utaziingiza kwenye quality roads?
Barabara ambayo angalao ilikuwa na kiwango cha juu ni ile iliyojengwa na Denmark (Mikumi to Mafinga) lakini baadaye tena imekuja kuharibiwa kwa kuweka matuta. Uliona wapi highway inakuwa na matuta?
Hizo nchi zote na baadhi ambazo hazimo kwenye hizo 10 best, mijini wana flyovers hasa, siyo yale madaraja yetu ya Ubungo na TAZARA ambayo ukiwa kwenye barabara moja huwezi kubadili kwenda barabara nyingine.
SHIDA YA CHAWA, MAFANIKIO KIDOGO, SIFA INAKUWA KAMA VILE SISI TUMEFANYA MAMBO YA AJABU KULIKO DUNIA NZIMA. TANZANIA KATIKA MAMBO MENGI, BADO TUPO NYUMA.
Tanzania ni ya 12 kutokana na hio list ranking.
Kuweka mpka namba kumi na moja kwenye list ya nchi 15 zilizotajwa ni wazi kia upo biased.
Tujitaidi kusema ukweli objectively.
Wewe itakua ulitumbuliwa kwa ufisadi au ni cheti feki. Samia mwenyewe kaenda ghana akaja na cheti cha benki ya afrika kutambua kazi ya magufuli tanzania kwenye miundombinu.
Mwenyewe kaabika ikabidi akubali jpm ndio kafanya kazi kubwaya miundombinu tz.
Tatizo ni wapambe wa Magu kutaka kuwadanganya watu kuwa eti Magu alifanya mambo makubwa sana wakati alifanya mambo ya kawaida sana, na mengine mengi alifanya vibaya.