Afrika: Nchi 10 zenye barabara nzuri Tanzania haimo, Hayati Magufuli alikuwa anafanya nini?

Afrika: Nchi 10 zenye barabara nzuri Tanzania haimo, Hayati Magufuli alikuwa anafanya nini?

Sasa Sisi ni wangapi ?.
Bwana yuleeee alikuwa mwongo kweri kweri.
Orodha ilitakiwa ziwe Nchi 10 tu, wakatoa bonasi ya Nchi moja ziwe 11, bado Tanzania haimo. Tatizo ni nini?
 
Wewe itakua ulitumbuliwa kwa ufisadi au ni cheti feki. Samia mwenyewe kaenda ghana akaja na cheti cha benki ya afrika kutambua kazi ya magufuli tanzania kwenye miundombinu. Mwenyewe kaabika ikabidi akubali jpm ndio kafanya kazi kubwaya miundombinu tz.
Lqbda cheti cha milembe
 
Alikuwa busy kutupiga kamba👇😁😁😁
 
Uliyemtaja ni awamu ya 5 ,umesema hajafanya kitu,hao wengine mbona huwazungumzii?Nchi ulizotaja hapo hizo barabara zilijengwa ndani ya awamu moja au mbili?Ujenzi wa nchi ni mchakato.Siyi jambo la kuamka na mtu mmoja ghafla tu na kutimiza.Sema chama Tawala kwa zaidi ya miaka 40 na awamu zaidi ya nne bado inasua sua katika ujenzi wa nchi kulinganisha na nchi nyingine Afrika.
hao shida baba zao walikuwa wezi wakafilisiwa ndo maana hasira zao hazitaisha.wengine walitumbuliwa sababu walijazana kwenye ofisi zenye malipo mazuri huku watoto wa walalahoi wakifanya kazi zenye malipo duni hivyo wataendelea kulia lia humu lkn ndo hiyvo wako nje ya mfumo.
 
Mkuu mbona unajichoresha, kwaiyo Ujenzi wa Barabara ulianza awamu ya tano?mbona hutaji Mawaziri wa awamu ya kwanza na ya pili?
Acha chuki Mkuu,zitakupa ugonjwa wa moyo.Magufuli alizaliwa ,akakua,akatumikikia Taifa na muda ulipofika akauwawa.Kwaiyo nadhani na wewe pambana kivyako ili vizazi vyako vije kuona kazi zako.
Wewe umemzidi nini Magufuli kimaisha?pamoja na kufa kwake familia yake inakula bata,wewe familia yako unaendeleaje 🤣🤣🤣🤣
 
Kwa maana ya quality roads, Tanzania haiwezi kuingia kabisa. Hizi barabara zinazojengwa na Wachina zinazojaa mashimo baada ya mwaka mmoja (nyingine chini ya miezi 6), utaziingiza kwenye quality roads?

Barabara ambayo angalao ilikuwa na kiwango cha juu ni ile iliyojengwa na Denmark (Mikumi to Mafinga) lakini baadaye tena imekuja kuharibiwa kwa kuweka matuta. Uliona wapi highway inakuwa na matuta?

Hizo nchi zote na baadhi ambazo hazimo kwenye hizo 10 best, mijini wana flyovers hasa, siyo yale madaraja yetu ya Ubungo na TAZARA ambayo ukiwa kwenye barabara moja huwezi kubadili kwenda barabara nyingine.

SHIDA YA CHAWA, MAFANIKIO KIDOGO, SIFA INAKUWA KAMA VILE SISI TUMEFANYA MAMBO YA AJABU KULIKO DUNIA NZIMA. TANZANIA KATIKA MAMBO MENGI, BADO TUPO NYUMA.
Ila ubungo pale ile ramani yake ya mwanzo ilikua nzuri sana sijui ikawaje,sehemu nyingine inayoenda kuharibiwa ni hilo daraja la jangwani,imagine pale inajengwa interchange itakayounga na daraja la salendar,kinondoni mkwajuni,likaenda hadi jangwani njia panda ya loyola ,kinapigwa kitu cha juu toka mapipa hadi fire,barabara iliyopo sasa ikabaki chini vile vile sababu ya interchange,ila kitapigwa kitu kama cha mfugale ndio imeisha hiyo
 
Tanzania ni ya 12 kutokana na hio list ranking.
Kuweka mpka namba kumi na moja kwenye list ya nchi 15 zilizotajwa ni wazi kia upo biased.
Tujitaidi kusema ukweli objectively.
Kwa hiyo unajivunia kushika namba 12 kati 15?
 
Sasa Sisi ni wangapi ?.
Bwana yuleeee alikuwa mwongo kweri kweri.
Mshukuruni hata hapo alipotufikisha, wakati anaingia mabasi yalikuwa yanapitia Kenya kwenda mikoa ya nfnai ya nchi yetu au mlisha jjisahaulisha haya? Lakini ni yeye aliyesema tutaendesha taxi mpaka huko mikoa iliyokuwa inafikika kupitia nchi jirani...

Watu msio na aibu wala moral conscious...
 
Uliyemtaja ni awamu ya 5 ,umesema hajafanya kitu,hao wengine mbona huwazungumzii?Nchi ulizotaja hapo hizo barabara zilijengwa ndani ya awamu moja au mbili?Ujenzi wa nchi ni mchakato.Siyi jambo la kuamka na mtu mmoja ghafla tu na kutimiza.Sema chama Tawala kwa zaidi ya miaka 40 na awamu zaidi ya nne bado inasua sua katika ujenzi wa nchi kulinganisha na nchi nyingine Afrika.
Mleta post mwenyewe ni CCM sema sio timu Magufuli.

Tanzania kwasasa hakuna upinzani wa vyama kama zamani.

Kwasasa kuna upinzani baina ya HAPAKAZI TU, na KAZI IENDELEE.

Mtoa post anaonekana ni timu KAZI IENDELEE!!!!!
 
Eeh kumbe,mwanasiasa mtu wa ajabu,akimmaliza jirani anahamia kwake
 
Mshukuruni hata hapo alipotufikisha, wakati anaingia mabasi yalikuwa yanapitia Kenya kwenda mikoa ya nfnai ya nchi yetu au mlisha jjisahaulisha haya? Lakini ni yeye aliyesema tutaendesha taxi mpaka huko mikoa iliyokuwa inafikika kupitia nchi jirani...

Watu msio na aibu wala moral conscious...
Unamwongelea Magufuli au Kikwete? Ni utawala wa Kikwete ndio uliofanya magari ya kutoka kanda ya Ziwa kwenda Dar yasipite tena Kenya. Wakati huo Magufuli alikuwa ni mtu wa kutumwa na siyo wa kufanya maamuzi.

Kwa kweli utawala wa Kikwete, kwenye upande wa ujenzi wa barabara za lami, mpaka sasa, ndio uliojenga kilometa nyingi kuliko utawala mwingine wowote.
 
Kila awamu ingefanya katika kiwango hichi
Mshukuruni hata hapo alipotufikisha, wakati anaingia mabasi yalikuwa yanapitia Kenya kwenda mikoa ya nfnai ya nchi yetu au mlisha jjisahaulisha haya? Lakini ni yeye aliyesema tutaendesha taxi mpaka huko mikoa iliyokuwa inafikika kupitia nchi jirani...

Watu msio na aibu wala moral conscious...
kila awamu ingefanya kwa aslimia hizi tungekuwa mbali sana.Naona kuna watu hawaoni kabisa juhudi zilozofanywa na JPM,Tupongeze na wengine wenye moyo huo wakija wafanye mengine zaidi.Tunachotaka wananchi ni maendeleo yanayoonekana na yanaisaidia jamii.
 
Alikuwa mtu wa kutumwa na akatumika kwa usahihi na kwa kujitoa hata baada ya yeye kushika hatamu akaendeleza na kufanya mazuri aliyojifunza alipokuwa wa kutumwa Juhudi alizozionyesha alipokuwa akitumwa ndo hizo zilifanya apewe dhamana kubwa zaidi.Kila anayetumwa kutumikia wananchi afanye kwa kiwango cha juu ili nchi ipige hatua.kila awamu ikifanya hivyo basi baada ya miaka 10 tutakuwa tumepanda kwenye orodha.
 
Unamwongelea Magufuli au Kikwete? Ni utawala wa Kikwete ndio uliofanya magari ya kutoka kanda ya Ziwa kwenda Dar yasipite tena Kenya. Wakati huo Magufuli alikuwa ni mtu wa kutumwa na siyo wa kufanya maamuzi.

Kwa kweli utawala wa Kikwete, kwenye upande wa ujenzi wa barabara za lami, mpaka sasa, ndio uliojenga kilometa nyingi kuliko utawala mwingine wowote.
Akishirikiana na Magu katika wizara ya ujenzi.
 
Uwongo kabisa walahi [emoji2959]
Kenya kuna barabara mbaya na mbovu kweli kweli [emoji3062]
Hii mijitu inatuonea uwivu haswa! Dadadeki zao walahi
 
Salaam Wakuu,
View attachment 2382228
Huwa nasikia watu wanamsifia Magufuli eti ni Baba wa Barabara/Mabarabara, hakutaka Demokrasa Nchini eti yeye ni Hapa kazi tu.

Lakini hakuna kazi hata moja alofanya inatambulika kwa watu wenye akili zao wanaojua nzuri na au maendeleo ni nini.
View attachment 2382234
Hayati Magufuli alivyokuwa anajisifia hadi kujiita Askari wa Mwamvuli kwa kufanya kazi ya barabara vizuri

Umasikini Ujinga na Maradhi; Kundi la Wajinga likapumbaza Taifa eti Hayati ni Mchapa kazi kajenga barabara, sijui Nchi iliibiwa sana hivyo kaongea na Barrick watalipa Kodi trilioni zaidi ya 347, huku bajeti ya nchi kwa mwaka ikiwa haifiki trilioni 40.

Haya mambo ya kumsifia hayati Magufuli tuwaachie Wananchi wa Chato japo hajawahi kuwa hata balozi wao wa nyumba kumi.

Mungu anajibu maombi.
View attachment 2382185
Top 11 African Countries With Quality Road🛣

1: Namibia🇳🇦 (score 5.2) world ranking 23

2: Egypt 🇪🇬(Score 5.0)world ranking 28

3: South Africa🇿🇦 (score 5.0) world ranking 29

4: Rwanda🇷🇼 (score 5.0) world ranking 31

5: Ivory Coast🇮🇪 (score 4.7) world ranking 42

6: Mauritius🇲🇺 (score 4.7) world ranking 44

7: Morocco🇲🇦 (score 4.4) world ranking 55

8: Kenya🇰🇪 (score 4.2) world ranking 61

9: Botswana🇧🇼 (score 4.1) world ranking 64

10: Cape Verde🇨🇻 (score 4.1) world ranking

11: Senegal🇸🇳 (score 4.0) world ranking 71

🌐Source: World Economic Forum’s Global Competitiveness Report Index
Sio kila kitu watanzania mtachukua nafasi ya kwanza...... Alaf hapa TZ bado sana sio huyo maza sio huyo chuma sio huyo kikwete wote walewale
 
Magu amekuwa rais kwa miaka mitano tu.
Unauhakika miundo mbinu ya Barbara katika hizo nchi imejengwa ndani ya miaka mitano sawasawa na kipindi Cha Magu?.
Kitu gani kinakufanya ulinganishe utendaji wa Magu kwenye miundombinu katika kipindichake Cha miaka mitano na hizo nchi ulizo taja.
 
Jamaa yetu alijua kutafuta sifa za kijinga
Kila anaposimama barabarani ni kuita mkurugenzi na kumuuliza
Eenheee hebu tuambie bajeti ya mwaka jana ulijenga barabara ya km ngapi
Usinidanganye nazijua barabara zote za nchi hii [emoji1] [emoji1787] [emoji23]
 
Back
Top Bottom