Afrika ndiyo kinara wa kufanya kazi ngumu lakini kisukari ni tishio je kazi ngumu sio mbadala wa mazoezi?

Usisahau kama vijana wa umri huo ndio watumiaji wakubwa wa vyakula na vinywaji vya viwandani haijalishi ni pombe, soda, au sharubati hapo sijataja vyakula vyao pendwa kama chipsi na taka taka zingine
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari...
Si wote wanafanya kazi ngumu, hasa mijini. Wanaokuwa maofisini hawatumii misuli kufanya kazi. Wakiwa nyumbani wanakaa, wakitoka nje wanaingia kwenye magari kukaa, na wakifika ofisini wanakaa, tena muda mwingi.

Kuna vijana wanashinda vijiweni bila kazi yoyote na kujiingiza kwenye ulevi hatarishi iwe mijini au vijijini. Aina ya maisha tunayoishi yamebadilika sana!

Aidha, aina ya vyakula na vinywaji vingi ni hatarishi, ikiwemo mafuta, chips, na nyama za ufugaji wa kisasa kwa madawa mengi. Mwili unatiwa sumu nyingi kutokana na kuacha vyakula na vinywaji asilia. Lakini pia kuna kisukari cha kurithi.
 
Afrika watu wanafanya kazi ngumu sana lakini bado kisukari ni tishio, nilikuwa Dodoma kukawa na upimaji wa Bure Cha kushangaza vijana below 40 wengi tu wana sukari...
Ulaji wa wanna ndio tatizo mkuu.
 
Si wote wanafanya kazi ngumu, hasa mijini. Wanaokuwa maofisini hawatumii misuli kufanya kazi. Wakiwa nyumbani wanakaa, wakitoka nje wanaingia kwenye gari kukaa, na wakifika ofisini wanakaa, tena muda mwingi...
Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya vijana wengi kuwa na kisukari. Asilimia ndogo sana ambayo inapata kisukari cha kurithi, lakini asilimia kubwa ni ulaji wa hivyo vitu ulivyovianisha. Kuna uhusiano mkubwa sana wa mlundikano wa mafuta mwilini na kisukari aina ya pili(type 2 diabate).
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Unaweza kufanya mazoezi na bado ukaugua kisukari kutokana na aina ya vyakula na vinywaji unavyotumia.

Fanya mazoezi, kula chakula asilia na kunywa kinywaji asilia, hususan maji safi na salama na matunda au juisi yake asilia.

Na zaidi sana, wakulima tuanze kulima Kilimo-afya (Agrihealth) na si kilimo-biashara (Agribusiness), chenye kemikali hatarishi kwa ardhi, mazao na miili yetu.
 
Sahihi kabisa
 
Ni kweli
 
Mifumo ya Ulaji hasa nyakati za usiku nalo ni tatizo, Waafrica wengi Dinner tunakula saa 2.30 na kuendelea kuna familia mpaka saa tano usiku ndo wanakula unaenda kulala, Kile chakula kinageuka sumu
😂😂😂😂
 
Mkuu, naomba uhusiano wa kisukari na mazoezi. Kuna kitu nataka kujifunza.
Inaaminika kadiri mtu anapofanya kazi ngumu sana matumizi ya sukari nayo huwa makubwa, nadhani huo ndo msingi wa mleta uzi, rejea tafakuri ya Pro Janabi kwamba kama unatoka clods FM kwenda Escape one huna haja ya kujaza mafuta full tank
 
Mafuta vs Kisukari?
 
kwan hujui wanaougua kisukari ni wale wanaoish kiulaya na sio kiafrika!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…