Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mfumo wa maisha maana afrika watu wanapenda sana vitu vitam
Upo sahihi, lakini tatizo kubwa lipo kwenye too much of carbohydrates.
Tatizo kubwa ni kwamba waafrika vyakula aina ya wanga ndiyo chakula kikuu.
Vyakula kama sembe na mchele vina carbobydrate nyingi, na ndiyo chanzo kikuu cha sukari aian ya glucose. Unapokula ugali au wali, maana yake unakula carbohydrate. Ukishakula carbohydrates, mwili unaivunja vunja na kuzalisha glucose ambayo ni sukari.
Sukari kama zile zinazowekwa kwenye cake au soda, ni fractose. Hii ikiingia mwilini ni mbaya kuliko hata ile inayopatilana kwa kuvunja carbohydrates.
Mtanzania haamini kama amekula bila ya kula ugali au wali, tofauti na jamii za wazungu ambao wanaweza kumaliza hata siku 3 bila kula carbohydrates au kula kwa kiwango kidogo sana.