Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Afrika tuna shida sana, Kiongozi gari ya milion 600?

Mtu kazaliwa kijijini, kakulia chumba kimoja na mbuzi leo ana madaraka anataka atembelee gari ya million 600, ambayo hajaitolea jasho, ni kodi za maskini wenzake.View attachment 2476045View attachment 2476044
Unatuambia sisi wanainchi au serikali yako ya ccm? lakini ujue serikali ni gharama mkuu kuongoza watu vichaa wenye chuki kama wewe ni lazima uwe na ndinga kama hiyo ili wakikukimbiza na vindinga vyao wasikupate.
 
Ulikuwa unashauri viongozi watumie vits au ist. Hizo gari ni gari za kazi na masafa marefu huwezi kuta imeharibika kirahisi more money more value. Ziendelee kutumika na serikali pamoja na viongozi kwanza inaleta heshima.
 
Sijawahi kuelewa kwa nini hizi gari zinagharama hivyo. Kwa wingi wa magari tunayonunua kutoka Toyota, ungetegemea tupewe discount kubwa ila inaonyesha si hivyo, gharama ni kama tena zinaongezeka.

Wanaokula hizi hela za nchi hawatazifaidi wao wala vizazi vyao. Hizi pesa zina laana.
Hizo gari sidhani kama bei yake halisi ni hiyo inawezekana kuna watu wa manunuzi wanazidisha bei kwa kuongea na watengenezaji ili wapige cha juu
 
Sio madarasa tu hata vyoo nya shimo hakuna!! Hivi huyu Samia haoni kuwa kuagiza magari ya gharama namna hiyo kila mwaka ni mzigo kwa wananchi? Mama anashindwa hata kuiga kutoka jirani zetu wa Zambia ambao Rais wao alikataa kuidhinisha ununuzi wa magari mapya ili hali yaliyokuwepo yalikuwa mazima.!!
Kinachouma zaidi ni tabia ya serikali kuwa na tendency ya kununua magari kama hayo kila mwaka haijalishi yaliyopo ni mazima au mabovu ni kuyauza tu kwa bei ya kutupwa kwa kigezo cha depreciation
 
Huko wanapoenda hakuna economic benefits zozote zinazozalishwa zaidi ya kutafuta per diems kwa nguvu.

Waziri anasafiri kilomita 800 kwenda kukagua ujenzi wa darasa, kazi ambazo katibu kata anaweza ifanya.

Mawaziri wanajipa roles ambazo haziendani na hadhi zao. Kuzurura bila sababu zozote.
Yaani hio ya mkuu eg waziri, katibu mkuu, mkurugenzl kusafiri inaumiza sana, kuna wakati nimeesafiri kwenda Mtumba - Dodoma mpaka wafanyakazi wakafikiri mie Ni mfanyakazi mwenzao
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy! Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P

nafahamu una feel sana life style yao, ndio mana bado upo kwenye maombi na wewe upate Teuzi.
 
Kama hizo fedha zipo, why not?. Viongozi wetu deserve the best that money can buy! Tena baada ya Lissu kushambuliwa, mimi nikashauri magari wote yawe ni armored.

P
Haaa haaaa ! Tupe mfano wa kiongozi Aliye uwawa,,, ishu ya Lisu, kila mtanzania anajua kilichotokea....! Wanadamu wanatabia ya Kusahau pale, malengo yao yanapotimia...!
 
Nikiwa Rais naondoa huu upuuzi wa magari..kila mtu ajinunulie gari lake au adandie daladala..

Mbona wafanyakazi wengine wanatumia gharama zao kufika maeneo yao ya kazi?.

Gari zitakuwa chache tu na zitakuwa hazina mwenyewe..ukitokea uhitaji wa kusafiri kikazi ndo utatumika tu and not otherwise.
Utawaua uvccm. Mawazo yao yote yapo kujineemesha!
 
Back
Top Bottom