Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Ishu ya tumbo ilianza hata kabla ya ukoloni kwa muafrika kumuuza ndugu yake kwenye misafara ya watumwa
Okay okay...so now we know tumezingua ndo tuje na strategies mpya...shida mtu anaweza sema hivi akipewa uongozi na yeye anatamani
 
Fyn .ndo superpower tayari asa...huwezi badilisha kitu
 
Uvivu wetu ndio tatizo letu. Waafrika tulio wengi tu wavivu sana kwenye suala la kufanya kazi.

Muda mwingi tunautumia kwa kubwabwaja tu badala ya kufanya kazi kwa bidii.

Fuatilia waajiriwa. Kabla ya kupata kazi mtu ananyenyekea vilivyo, akishaajiriwa anakuwa na nyodo, kiburi, jeuri, majivuno na mbwembwe za kufa mtu, tena wakati mwingine kwa kujisifu kuwa hata iweje mshahara wangu mwisho wa mwezi upo palepale.

Hao wasomi ndio wezi wa rasilimali na mali za uma ni hatari

Tuache uvivu tujitume kufanya kazi kwa maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio story ya huyo jamaa imenitouch Sana . Kufika levels za hizo nchi kwa fikra zetu hizi...tutasubiri Sana .. labda viongozi wanaokuja might do it
 
ukiwa na wananchi wajinga bas utazalisha viongozi wajinga , ona wengine wanashabikia na kukosoa mkataba bila kuusoma , kwa wajinga hawa utaendeleaje?
We unaona mkataba upo freshi
 
🤣Wawekezaji au sio...usimsahau na mwarabu nae yupo moto
 
🤣Nyie ..mi spendi mnavyosema shida ni waafrika sijui rangi...no we can change that...Kuna nchi zilikuwa hoi ila now zipo moto kina south Korea china etc
 
Usiseme hivi...ukisema shida rangi unakuwa unakatisha tamaa
 
Ukisema laana unakuwa unajiumiza tu mwenyewe...unajiaminisha ujinga
 
So solution ni serikali mpya

Hiyo serikali Mpya itapatikanaje wakati wezi/wahuni/majambazi/matapeli ndiyo wapo kwenye mifumo yote? Ukisema Katiba Mpya hao ndiyo wanaamua ipatikane au isipatikane ,ukisema Bunge litunge sheria kali hao ndiyo wapo kuwalinda.

Solution ni kama alivyosema Dr Slaa ,Madaraka yanatoka kwa Watu ,wananchi ndiyo waamuzi wa Mwisho ,Tukipata kina Mwabukusi/Mdude kama 50 hivi tutapata serikali Mpya.
 
Kazi Kazi tu Kama wenzetu
 
Hahaha sawa tusubirie uchaguzi
 
Spirit unamaanisha nini mkuu
Hali ya kutaka kufanikiwa, kuendelea, kufanikisha, kupenda nchi, kupenda chao, kupenda maendeleo, kufanya kazi kwa bidii kusiko kawaida, kutokuvumilia upuuzi wa viongozi spirit ya watu East Asia ina cover vitu vingi hivyo ni vichache.

Hao jamaa hawapendi ujinga kabisa sisi tunapenda ujinga nyuzi nyingi za humu zinathibitisha hilo hata mitaani hali ni hiyo hiyo we are not serious about our country
 
Sijawahi ndo maana nauliza
Jaribu kutafuta mkorea au mjapan au mchina akuoneshe nini maana ya kufanya kazi na kufanikiwa au tembele site zao za construction, viwanda vyao au miradi yao ukishindwa kabisa jifunze mitandaoni kuhusu ufanyaji kazi wa hao jamaa na kufanikiwa kwao
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Uongozi,fikiria tuna miaka zaidi ya 60 ya uhuru hatuwezi kuendesha bandari,hatuwezi kuchimba gas,hatuwezi kuchimba dhahabu,hatuwezi kuingia mikataba yenye maslahi ya nchi.

Tumewekeza zaidi katika kuiba uchaguzi,kununua wapinzani,kuteuana kwa upendeleo,tumetengeneza nafasi nyingi za kuteuana wakati kazi zenyewe hakuna eg DC,DAS,DED.......

Afrika imejaa watawala walafi,wajinga,wapumbavu,majambazi na wasifikiri juu ya nchi zao mwisho wa fikra zao unaishia katika familia zao.
 
🤣Mi nashabikia muungano wetu ..staki amani itoweke
Unashabikia muungano au unashabikia ukoloni una tofauti na wazungu waliotukoloni ? Wewe na Nyerere akili moja hovyo kabisa mnawaza tu kutawala watu kimabavu.

Sasa mkoloni mlikuwa haumtaki kwa nini ? Huku upuuzi wake mkoloni mnauendeleza kwa weusi wenzenu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…