Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Ishu ya tumbo ilianza hata kabla ya ukoloni kwa muafrika kumuuza ndugu yake kwenye misafara ya watumwa
Okay okay...so now we know tumezingua ndo tuje na strategies mpya...shida mtu anaweza sema hivi akipewa uongozi na yeye anatamani
 
Hivi unajua katika nchi zenye slums za kutosha na gap ya classes india ipo ? Yaani unaweza ukakuta masikini wa kutupwa India ambae huku hujawahi kumuona..., Lakini usihofu na sisi huko ndipo tunapoelekea... (Sio kwenye So called Uchumi wa kwenye vitabu..., Bali Umasikini wa Kutupwa)
Fyn .ndo superpower tayari asa...huwezi badilisha kitu
 
Uvivu wetu ndio tatizo letu. Waafrika tulio wengi tu wavivu sana kwenye suala la kufanya kazi.

Muda mwingi tunautumia kwa kubwabwaja tu badala ya kufanya kazi kwa bidii.

Fuatilia waajiriwa. Kabla ya kupata kazi mtu ananyenyekea vilivyo, akishaajiriwa anakuwa na nyodo, kiburi, jeuri, majivuno na mbwembwe za kufa mtu, tena wakati mwingine kwa kujisifu kuwa hata iweje mshahara wangu mwisho wa mwezi upo palepale.

Hao wasomi ndio wezi wa rasilimali na mali za uma ni hatari

Tuache uvivu tujitume kufanya kazi kwa maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kwamba majority ya watu wa western countries ni religious. Lakini hata hao inategemea na wapi, na religion wanaichukulia vipi.

Kwa mfano, Ulaya watu wengi wanajitambulisha kwamba hawaamini Mungu, atheists. Nchi kama Finland na Spain around 20% ya nchi hawaamini Mungu. Netherlands ndiyo around 45%, yani karibu nusu. Nchi kama Estonia watu hao wako around 60%, Czech Republic wako around 78%. Na hawa watu hawapendi uongo wa dini na Mungu, lakini wamejiwekea mifumo inayojali utu, inajali uhai, ina demokrasia, inajali watoto, inajali wazee.

Sisi tuna unafiki wa kuendekeza Mungu na dini halafu tunaminyana, kuuzana na kuuana kila siku.

Hata hao wenye kuamini Mungu na dini, kwa kiasi kikubwa wanaamini kiutamaduni tu, wanapenda sense of community ya kanisani, wanapenda kwaya, wanapenda architecture za makanisa zile stained glasses, na hao ni wazee ambao wanaenda kuisha sasa, vijana hawana affiliation na dini sana.

Wale wenzetu wamebaki na dini kama hobby, sisi tunatumia dini kama uchawi.

Ndiyo maana Africa makanisa ya uponyaji na kusaidia watu wafanikiwe kiuchumi yanashamiri.
Watu wengi wanafuata dini kama mbadala wa waganga wa kienyeji, dini inatumiwa kama uchawi tu, iwaponye, iwaletee mafanikio, wenye kufuata dini kwa misingi ya dini hasa ni wachache sana.

Yani ni hivi, kwa wenzetu in the west umuhimu wa dini umepunguzwa sana dunia inayoendelea kwa sababu ya sayansi.Mtu akiumwa kuna huduma nzuri za afya, si kwetu mtu akiumwa sehemu nyingi hakuna tumaini, inabidi aombe Mungu tu, atake asitake.

Nchi zina ajira kwa kila mtu, mpaka mtu mwenye mtindio wa ubongo yule anapangiwa kazi kwa mujibu wa uwezo wake. Mimi nimekuja New York mara ya kwanza nilikuwa napanda basi la asubuhi kabisa kwenda kazini, kukaw na jamaa mmoja ana matatizo kama ya Down Syndrome or something like that, hawezi kusema vizuri, hata kutembea kwake kwa tabu. Lakini jamaa alikuwa anapanda basi hilo hilo kila siku, halafu kwenye basi ana kelele kuongea na watu, halafu wazungu wanampenda kichizi wanapiga stories naye (alikuwa black). Jamaa ana matatizo ya mfumo wa ubongo lakini alikuwa na kazi yake supermarket anapanga vitu, na jamii inamthamini, na yeye anachangia uchumi wao kwa kiasi chake, analipwa mshahara wake.

Nikasema huyu ashukuru sana kazaliwa Marekani, angekuwa Tanzania watu wangemfungia ndani asionekane, ingekuwa aibu kwa familia huyu kuonekana, licha ya kupanda basi na kufanya kazi.

Unaona watu wanavyothamini utu wa mtu hata mwenye kilema hapo? Jamii iko so inclusive.

Huko kwetu watu wazima wenye afya zao na akili zao hatutumii hiyo human resource, unajua vijana wanaokaa bila kazi tunapoteza nguvukazi kiasi gani kwa mwaka hapo?

Hawa watu walishagundua kwamba dini ipo kama utamaduni, sasa tutajipangia sheria zaenye maadili ya utu, ndiyo maana unaona kuna sheria kali dhidi ya ubaguzi wa watu walemavu au kubagua watu kwa race, au kubagua wanawake na wazee. Dini ipo, lakini sheria ndiyo kali zaidi.

Sisi hatufuati dini wala sheria, tunafuata unafiki na ubinafsi tu.

Sasa kama una taifa lenye nguvukazi kubwa sana, unaipoteza kwa umachinga na ubodaboda tu, unategemea utaendelea vipi kiuchumi?

Angalia nchi masikini zinavyoamini dini.

Ni vigumu sana kukuta nchi masikini ambayo haina historia ya Ukomunisti kuwa na atheists zaidi ya 20%

Hio story ya huyo jamaa imenitouch Sana . Kufika levels za hizo nchi kwa fikra zetu hizi...tutasubiri Sana .. labda viongozi wanaokuja might do it
 
Ni kweli ishu sio Afrika, ishu ni waafrika wenyewe, walio iharibu Afrika ndio maana Afrika imekuwa ngumu kuishi

Hao wazungu wanao kuja kuishi Afrika, wanakuja wakiwa na mitaji yao na hela zao.

Wanajua huku mali zipo, na kwa vile waafrika wengi ni wajinga ndio mwanya mzuri wa kupiga pesa za wajinga wasio jitambua.

Mzungu akija Afrika anashika ardhi kubwa na kuanza kuajiri wakazi walewale walio shindwa kutumia ardhi hiyo.
🤣Wawekezaji au sio...usimsahau na mwarabu nae yupo moto
 
Nyerere alikataa madini yasichimbwe hadi watanzania waje wasome na wapate Akili na utaalamu wa kutosha kuchimba madini hayo.

Wasomi hao walio tarajiwa wamekuja kuwa Wezi na Wajinga, Wasiojua hata thamani halisi ya madini yenyewe katika soko la Dunia.

Nchi ina ishia kupata 3% tu ya mapato.Huku asilimia nyingine zikienda kwa wazungu.

Tanzanite inapatikana Tanzania pekee lakini anaye ongoza kwa kuuza Tanzanite Worldwide ni India.

Wananchi wa Manyara Simanjiro inako patikana Tanzanite hiyo, wame achiwa mashimo na mahandaki tu....[emoji1][emoji1]

Geita mji wenye dhahabu lakini Raia wake wengi ni Maskini choka mbaya wame achiwa mashimo na GGM...[emoji1787][emoji1787]

Sometimes unawaza waafrika ni kama
ma mbumbumbu flani vilee..!!!

Dead people walking....!!
🤣Nyie ..mi spendi mnavyosema shida ni waafrika sijui rangi...no we can change that...Kuna nchi zilikuwa hoi ila now zipo moto kina south Korea china etc
 
narudia tena kusema hili,..yaweza kuwa kuna uhusiano mkubwa sana kati rangi ya ngozi na akili yake (race and intelligence)...maana mpaka waafrica walioko Caribbean wote kichwani ziro.... waafrica wao ni kuzaliana kama simbilisi au sungura huku MALEZI kwa watoto ni sifuri,.kulewa, ngono na wizi.......hiiii ni zaidi ya laaana!
Usiseme hivi...ukisema shida rangi unakuwa unakatisha tamaa
 
Aisee africa binafsi naweza sema mungu alilaani rangi nyeusi full stop tuna matendo mabaya sana ata ukienda kwenye maandiko matakatifu utaona jinsi kaini alivyomuua mwenzake kwa sababu ya tamaa tu vivyo ivyo kea kwa watu weusi ni kuwaza wizi tu kuanzia huko juu hadi serikali za mitaa alafu tunataka tujiringanishe na nchi za wenye akili na mawazo chanya kweli sisi africa mpaka yesu arudi maendeleo tutayasikia tu uko kwa wenzetu weupe
Ukisema laana unakuwa unajiumiza tu mwenyewe...unajiaminisha ujinga
 
So solution ni serikali mpya

Hiyo serikali Mpya itapatikanaje wakati wezi/wahuni/majambazi/matapeli ndiyo wapo kwenye mifumo yote? Ukisema Katiba Mpya hao ndiyo wanaamua ipatikane au isipatikane ,ukisema Bunge litunge sheria kali hao ndiyo wapo kuwalinda.

Solution ni kama alivyosema Dr Slaa ,Madaraka yanatoka kwa Watu ,wananchi ndiyo waamuzi wa Mwisho ,Tukipata kina Mwabukusi/Mdude kama 50 hivi tutapata serikali Mpya.
 
Uvivu wetu ndio tatizo letu. Waafrika tulio wengi tu wavivu sana kwenye suala la kufanya kazi.

Muda mwingi tunautumia kwa kubwabwaja tu badala ya kufanya kazi kwa bidii.

Fuatilia waajiriwa. Kabla ya kupata kazi mtu ananyenyekea vilivyo, akishaajiriwa anakuwa na nyodo, kiburi, jeuri, majivuno na mbwembwe za kufa mtu, tena wakati mwingine kwa kujisifu kuwa hata iweje mshahara wangu mwisho wa mwezi upo palepale.

Hao wasomi ndio wezi wa rasilimali na mali za uma ni hatari

Tuache uvivu tujitume kufanya kazi kwa maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla

Sent using Jamii Forums mobile app
Kazi Kazi tu Kama wenzetu
 
Hiyo serikali Mpya itapatikanaje wakati wezi/wahuni/majambazi/matapeli ndiyo wapo kwenye mifumo yote? Ukisema Katiba Mpya hao ndiyo wanaamua ipatikane au isipatikane ,ukisema Bunge litunge sheria kali hao ndiyo wapo kuwalinda.

Solution ni kama aliyesema Dr Slaa ,Madaraka yanatoka kwa Watu ,wananchi ndiyo waamuzi wa Mwisho ,Tukipata kina Mwabukusi/Mdude kama 50 hivi tutapata serikali Mpya.
Hahaha sawa tusubirie uchaguzi
 
Spirit unamaanisha nini mkuu
Hali ya kutaka kufanikiwa, kuendelea, kufanikisha, kupenda nchi, kupenda chao, kupenda maendeleo, kufanya kazi kwa bidii kusiko kawaida, kutokuvumilia upuuzi wa viongozi spirit ya watu East Asia ina cover vitu vingi hivyo ni vichache.

Hao jamaa hawapendi ujinga kabisa sisi tunapenda ujinga nyuzi nyingi za humu zinathibitisha hilo hata mitaani hali ni hiyo hiyo we are not serious about our country
 
Sijawahi ndo maana nauliza
Jaribu kutafuta mkorea au mjapan au mchina akuoneshe nini maana ya kufanya kazi na kufanikiwa au tembele site zao za construction, viwanda vyao au miradi yao ukishindwa kabisa jifunze mitandaoni kuhusu ufanyaji kazi wa hao jamaa na kufanikiwa kwao
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Uongozi,fikiria tuna miaka zaidi ya 60 ya uhuru hatuwezi kuendesha bandari,hatuwezi kuchimba gas,hatuwezi kuchimba dhahabu,hatuwezi kuingia mikataba yenye maslahi ya nchi.

Tumewekeza zaidi katika kuiba uchaguzi,kununua wapinzani,kuteuana kwa upendeleo,tumetengeneza nafasi nyingi za kuteuana wakati kazi zenyewe hakuna eg DC,DAS,DED.......

Afrika imejaa watawala walafi,wajinga,wapumbavu,majambazi na wasifikiri juu ya nchi zao mwisho wa fikra zao unaishia katika familia zao.
 
🤣Mi nashabikia muungano wetu ..staki amani itoweke
Unashabikia muungano au unashabikia ukoloni una tofauti na wazungu waliotukoloni ? Wewe na Nyerere akili moja hovyo kabisa mnawaza tu kutawala watu kimabavu.

Sasa mkoloni mlikuwa haumtaki kwa nini ? Huku upuuzi wake mkoloni mnauendeleza kwa weusi wenzenu ?
 
Back
Top Bottom