Tatizo lipo kichwani tu, hata hatujui tunafanya nini means kama binadamu kutoka afrika hatujui tunataka nini... mentality tu wazee, enzi na enzi waafrika tuna chembe ya ubinafsi, tulishakosea huko nyuma ila bado tunazidi kukosea huo si ukichaa?, usije ukadhani watu wanahubiri uzalendo majukwaani ukachukulia serious sana
Tumeshindwa ku channel sifa yetu ya ubinafsi kwenye mambo ya msingi ya nchi kilichobaki Kila mtu alinde familia yake. Ubinafsi ni jambo ambalo tumezaliwa nalo tumekuzwa kwenye hayo mazingira enzi na enzi, sisi tumekubali kuchagua mfumo wa Kila mtu ashibishe wa kwake Hadi wasaze then kitakachobaki tutawapa wengine wakombeleze, ni jambo la hatari sana kuishi kwenye jamaa inayoona UBINAFSI ni kama sifa na hitaji la msingi
Ukitaka kuona hili Fanya survey ndogo mtaani uliza tu kishkaji kuwa "ukipata nafasi sehemu labda uongozi, nguvu etc cha kwanza utafanya Nini", kwanza utasikia akikwambia cha kwanza bro nitapiga pesa kinoma maana viongozi wenyew si unawaona, we fikiri nikitoka hapa Kila mtu atanicheka kuwa nilikuwa sehemu nzuri nikazubaa Sasa Sina kitu, nitachekwa Hilo ni jibu la wengi, hii collectively inaathari Kwa taifa lote hivyo ni endless circle ya mentality hii.
Kaa na watu wa hayo mataifa uliyotaja hata watatu wanne hivi then uongea nao jambo lolote la msingi, utaona mwenyewe vitu vya msingi wanavyoongea kwenye masuala nyeti na ya muhimu au nenda YouTube etc, utaona mentality za hayo mataifa uliyotaja.
Vichwa vyetu ni mzigo Kwa shingo.