Ndio maana waafrika wengi wanapambana kulikimbia kabisa hili bara.
West Africans na North Africans kila mara hujaribu kuvuka bahari ya mediterranean wakijaribu kuingia Ulaya. Licha ya wengi kufa maji, lakini hawa achi kujaribu bahati yao ya kuvuka bahari.
Vijana wengi wa Afrika, hupambana kwenda kusoma bachelor degrees, Masters na PhD kwenye vyuo vya Ulaya, America na Asia waki target kubakia huko huko kufanya kazi na kuishi, ila si kurudi Afrika.
Wachezaji wa mpira kutoka Afrika, wakifika ulaya hubadilisha kabisa uraia wao na kuomba uraia wa nchi za Ulaya. Mfano mzuri ni timu ya taifa ya Ufaransa.wachezaji wengi ni kutoka Afrika.
Mpaka hapa unaona kwamba kuwa Mwafrika na kuishi Afrika ni ngumu sana, kutokana na mifumo mibovu iliyopo.