Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Afrika tunashindwa na nchi za Asia tulizopata uhuru muda sawa. Shida ni nini?

Viongozi wa Africa hawana vision Wala mission
Hivyo hawana uwezo !! Huo ndio ukweli kataa kubali
 
Jaribu kutafuta mkorea au mjapan au mchina akuoneshe nini maana ya kufanya kazi na kufanikiwa au tembele site zao za construction, viwanda vyao au miradi yao ukishindwa kabisa jifunze mitandaoni kuhusu ufanyaji kazi wa hao jamaa na kufanikiwa kwao
Mmmh so we must be like them...Ila vitu kama hivi vipo in their culture mtu tokea udogoni anavyo
 
Uongozi,fikiria tuna miaka zaidi ya 60 ya uhuru hatuwezi kuendesha bandari,hatuwezi kuchimba gas,hatuwezi kuchimba dhahabu,hatuwezi kuingia mikataba yenye maslahi ya nchi.

Tumewekeza zaidi katika kuiba uchaguzi,kununua wapinzani,kuteuana kwa upendeleo,tumetengeneza nafasi nyingi za kuteuana wakati kazi zenyewe hakuna eg DC,DAS,DED.......

Afrika imejaa watawala walafi,wajinga,wapumbavu,majambazi na wasifikiri juu ya nchi zao mwisho wa fikra zao unaishia katika familia zao.
Hahaha umeongea kwa hisia kichizi...sawa bwana that is so true ..we need to change ourselves on that
 
Unashabikia muungano au unashabikia ukoloni una tofauti na wazungu waliotukoloni ? Wewe na Nyerere akili moja hovyo kabisa mnawaza tu kutawala watu kimabavu.

Sasa mkoloni mlikuwa haumtaki kwa nini ? Huku upuuzi wake mkoloni mnauendeleza kwa weusi wenzenu ?
Asa...ukisema utugawe tayari ushasumbua vitu vingi
 
Hahaha unataka tupigane vita ama

Hapana ,wananchi wakiamua kuiondoa serikali wenyewe pasipo kumwaga damu ,ni kama zile harakati za kudai uhuru alizozifanya Nyerere na watu wake ,kwasasa sisi tuna mkoloni mweusi tudai uhuru wa pili kumuondoa "MKOLONI MWEUSI".
 
Asa...ukisema utugawe tayari ushasumbua vitu vingi
Kila taifa liishi kwa amani kivyake acha kukumbatia ukoloni jinga kabisa kuendelea kuua na kumwaga damu za Wazanzibar kisa muungano ni zaidi ya ukoloni wa mzungu

Muungano haulindwi kwa bunduki huo ni ukoloni mna akili za kipuuzi sana nyie majitu roho za kinyama zimewajaa roho za Wazanzibar zitaendelea kuwalilia maisha yote waacheni wawe huru na nchi yao kina wauma nini wao wakiwa huru kivyao ?
 
Jamani tuongee serious, nchi Kama India, Singapore, Malaysia, Indonesia zimepata uhuru almost the same time na nchi za kiafrika. Cha ajabu wenzetu wameendelea Sana halafu sisi bado tuna umaskini wa kutupa.

Afrika jamani shida ni nini?
Shida ya waafrika ni kuiga mambo ya nje hatutaki kufanya mambo yetu wenyewe basiii
 
Solution sio hio Sasa... solution sio violence..mbona ulaya hawachomani moto...na wako peaceful na wanaendelea.
Wanaendelea sababu taasisi ziko strong. Mahakama ya Marekani huwezi kuichezea kijinga kwa kupiga simu zako eti kisa wewe ni billionea.

Bongo ukiwa kapuku milango ya jela iko wazi ila ukiwa na connection na IGP na DPP tu na mpunga unao jela kuingia ni ndoto.
 
Solution sio violence...unakuwa unafanya nchi isiwe na amani.. solution ni elimu na sheria kufuatilia
Nchi ikokosa amani kidogo tutajifunza kitu flani.

Kwa sasa kila mtu ni mbinafsi kwa sababu sio shida zake familia yake inakula na kulala bila shida wengine wanaonyanyasika na ushenzi wa watawala wanaonekana ma foreigner tu.

Ila siku kikinuka janga litakuwa la kitaifa tutashikamana bila kampeni. Wenye nacho na wasio nacho lengo litakuwa ni moja tu kumfurusha jinamizi Chama cha Mambuzi na viongozi wake wasiothaminu utu.
 
🤣Ishu ya CAG si ilinyamazishwa na propaganda za ushoga ..si unajua wabongo wakiskia ushoga wanasahau kila kitu...
Sasa wamekuja na wizi wa 450m na kuacha ule wa Kijambazi mpaka leo hawaongelei tena ntaona wapo serious kama watakuja kujadili taarifa ya CAG kuliko kuhangaika na kesi za rushwa mahakamani zote ni kujenga maadili mema ila kwa nini zingine ziachwe na zingine zifatiliwe kwenye Nchi hiyo hiyo moja...
 
Na sisi tungejaribu mwizi Fulani na Fulani unawafungisha ndoa na RPG pale Taifa uone Kesho kuna mwenye balls za kuiba mali ya umma mwizi mmoja bomu moja[emoji2][emoji2][emoji2]

Wanaiba Kwa sabab wanajua hatuna cha kuwafanya
Hio ni chap nchi ingenyooka kama China. Adhabu ziboreshwe ili watu wasikimbilie uongozi kilafi bali uwajibikaji
 
Kwanin isiwe na Amani

Kwani wananchi waiba simu si wanachomana moto mbona Amani ipo

Ndio iwe kwa kimkurugenzi umekishindilia risasi za kichwa kwa wizi wake???

Kila atakayeingia ofisini atajua kuheshim mali inayoitwa ya Nchi
Hii point ndio sawa na zile propoganda za kuleta taharuki wakati watu wanaandamana kwa amani.
 
Ukitaka kujua huu wizi ni sababu ya sheria zetu mbovu za kubebana angalia awamu iliopita jinsi ambavyo watu walinyooka. Ila amekuja mama tu tumerudi miaka 10 nyuma kwenye uwajibikaji.

Baba akiwa strong kimfumo familia haiyumbi.
Wizi ni ngazi ya familia hadi juu Kila mmoja kwa level yake.Mwingine atauza nchi,baba anaiba ofisin analeta home,mama nae anampiga baba apate za vicoba,dada wa kazi nae anapiga za matumizi huku anawashindisha watoto wa boss viporo ili atume kijijini kwa mzazi wake amlimie mazao, mzazi kijijini nae anakula bata kilabuni ye ndo boss akitamba kwamba ye ndo anajua kuzaa binti anafanya kazi mjini.

Tufanye maombi tu kuondoa hii roho ya upigaji
 
Back
Top Bottom