Afrika yaingia Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2022

Afrika yaingia Nusu Fainali ya Kombe la Dunia 2022

Jina lako linaonekana ni la kike, ama nakosea?!

Kama ndivyo, basi utakuwa mwanamke wa ajabu kwa kuendekeza chuki na ubaguzi! Sijui hao watoto wako wanapata malezi ya aina gani ikiwa mama anaonesha ana chuki za wazi wazi,,,

Kwahiyo huwa unawaambia "...usiende kucheza na akina Mohammed, hao ni waarabu na Waislam, mimi siwapendi"

I honestly feel sorry for your kids!!
Dah Chige chuki zina gender ?
 
Nimekua nikiona mada za aina hii, naona wote wanaobisha Morocco hawapo Africa, namuona pimbi.

Swali la msingi? Kwani Uafrika ni nini? Rangi, kama ndio na wale weusi waliopo France, Belgium, Papua Guinea, South American Countries je wote ni waafrika?

Au weupe waliopo humi Afrika, je wote ni waafrika?

Ili iwe Muafrika, inabidi nchi yako iwe ndani ya bara hili regardless ya Rangi, Kimo, nywele au unene?

Afrika, tutambue uafrika sio rangi.
Nini msingi wa mtu kuitwa "African American" huko USA!? Kama sio Rangi!?
 
Jina lako linaonekana ni la kike, ama nakosea?!

Kama ndivyo, basi utakuwa mwanamke wa ajabu kwa kuendekeza chuki na ubaguzi! Sijui hao watoto wako wanapata malezi ya aina gani ikiwa mama anaonesha ana chuki za wazi wazi,,,

Kwahiyo huwa unawaambia "...usiende kucheza na akina Mohammed, hao ni waarabu na Waislam, mimi siwapendi"

I honestly feel sorry for your kids!!
Acha kumshambulia kinafiki.
 
Hiyo ni theory yako Sasa usiilazimishe iwe ukweli

Fifa wanachoangalia na inavyotambulika morocco ni mwanachama wa CAF yaan (Confédération Africaine de Football ) ambacho ndo chombo kinachosimamia mpira africa
Maombi yao ya kucheza ulaya yangekubaliwa, je bado tungewahesabia kuwa wawakilishi wa Africa!? Mafanikio yao bado yangehesabiwa kuwa mafanikio ya Afrika!?
 
Kuna mambo tunazunguka tu mbuyu ukweli usemwe. Uafrika si ngozi, muafrika ni mkazi anayetoka bara la Afrika. Lakini, je, hao wenzetu ambao kimsingi mataifa yao yapo ndani ya bara la Afrika wanajihisi hivyo kama ambavyo inatakiwa kuwa? Jibu: si kweli.

Inabidi ifike lakini pia wakati 'waafrika weusi' tujitathmini kwanini tunakataliwa sana hapa duniani. Upumbavu wetu ambao umetufanya tuendelee kuwa duni ndio unatuponza, hatuheshimiwi na tunaonekana duni.

Anyway, all in all nawatakia mafanikio mema timu zote kuibuka na ubingwa(ushindi).
 
Kwa mara ya kwanza tangu kombe la dunia lianze, Afrika kupitia timu ya Morocco yaingia nusu fainali.

Pongezi kwa wawakilishi wetu morocco kwa kuweka historia.
Walishatukataa sisi sio ndugu zao,japo walifuta kauli.
 
Moroko iko ulaya zaidi kuliko Afrika, ni kama Kigamboni na Kurasini kwani ukiwa upande wa Moroko ulaya inaiona na insweza kuingia kwa kuogelea tu.
Hii hoja ni ya kipuuzi. Kama ni hivyo basi na Spain ipo Africa zaidi kuliko Ulaya kwa kuwa ukiwa upande wa Hispania Africa unaiona na unaweza kuogelea kwenye bahari ya Mediterranean. Kwa hiyo Hispania ni Africa.
 
Hii ni kwa tafsiri yako, kwao ni waarabu sio wafrika na sijawahi kishududia mwarabu anajinasibu kama mwafrika au kujivunia.
Tafsiri ya mwafrika ni mtu aliyezaliwa afrika na ni mweusi.
Mhindi akizaliwa Africa huyo ni mhind, Elon musk kazaliwa Africa sijawai kusikia akijiita mwafrica.
Mweusi akizaliwa America anaitwa black america au negro na ukienda wewe mweusi kutoka huku wanakubagua.
Mchina akizaliwa Africa huyo ni mchina hakuna mwarabu anataka kuchangamana na nyie waafrica mnajipendekeza tu, unless uwe muislamu undugu katika imani.
Waasis wa kuwaita (wahind ,waarab,makaburu) walozaliwa Africa kuwa ni (wahind ,Waarab ,makaburu) ni nan?

Hii continent ingekuwa inajiweza dunia ingepata tabu sana inawatu wapuuzi sana. Wee imagine mtu kasema ushindi wa Morocco ni ushindi wa Arabs na Morocco lakin kuna mtu anautaja uislam [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Maombi yao ya kucheza ulaya yangekubaliwa, je bado tungewahesabia kuwa wawakilishi wa Africa!? Mafanikio yao bado yangehesabiwa kuwa mafanikio ya Afrika!?
Mbona vit vingne hata sio vigumu kufikir.Okay wangekubaliwa mafanikio yao yangekua ya ulaya...Na mm nkuulize kwann hayo mafaniko yangekuwa ya Ulaya?
 
Kuna mambo tunazunguka tu mbuyu ukweli usemwe. Uafrika si ngozi, muafrika ni mkazi anayetoka bara la Afrika. Lakini, je, hao wenzetu ambao kimsingi mataifa yao yapo ndani ya bara la Afrika wanajihisi hivyo kama ambavyo inatakiwa kuwa? Jibu: si kweli.

Inabidi ifike lakini pia wakati 'waafrika weusi' tujitathmini kwanini tunakataliwa sana hapa duniani. Upumbavu wetu ambao umetufanya tuendelee kuwa duni ndio unatuponza, hatuheshimiwi na tunaonekana duni.

Anyway, all in all nawatakia mafanikio mema timu zote kuibuka na ubingwa(ushindi).
Tunabaguliwa kwa sabab ya uduni wa maisha.Na huu uduni wa maisha tunausababisha wenyew sababu hatuna akili
 
Mpira ni burudani usilazimishe mambo. Kama kuna Shabiki burudani yake ni waarabu wafungwe na kuna muarabu burudani yake ni ushindi uwawakilishe waarabu na sio watu wengine usilazimishe. Ww burudani yako ni kuwa Africa imeshinda pia sawa tu na Africa yako ya kwenye makaratasi ila watu wapo kwenye ulimwengu wa Soka ndo maana kuna mwingine anaiona ufaransa ikishinda kama vile watu wa Afrika wameshinda na anapata burudani.
Akuna anaelazimisha jambo ila ukweli utabaki kuwa ukweli Morocco ni Waafrika wenye asili ya kiarabu
 
Back
Top Bottom