Afumaniwa akidaiwa kuwaingilia vijana wawili kinyume na maumbile

Afumaniwa akidaiwa kuwaingilia vijana wawili kinyume na maumbile

Aisee hizi mambo tulikuwa tunaziskiaga kama habari za mbali ila sasa zipo mlangoni kwetu.Wanaume wanaishaa
 
wewe CAPO DELGADO , njoo huku uwatete mashoga wa kigalatia

Ongezea na huku mlikojaa unakosema hakuna mashoga

1790022955939.png


1790022975901.png

1790023168207.png

1790023214666.png
 
Kama ni kweli yalitaka kufanyika hayo inaonekana wazi walikubaliana, polisi wa nini?
 
Wanaume watatu wamekutwa katika chumba kimoja eneo la Msasani, Kitongoji cha Oloresho, Kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, katika mazingira yaliyoibua mashaka miongoni mwa Wananchi.

Mmoja wa Wanaume hao, aliyefahamika kwa jina la Alex Kimario, anayedaiwa kuwa dereva wa bodaboda, alishikiliwa na wananchi baada ya vijana wawili waliokuwa naye kutoroka katika eneo hilo.

Baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa Alex alikuwa akiwafanyia Vijana hao wawili kitendo cha ngono kinyume na maumbile, madai ambayo bado hayajathibitishwa na mamlaka.

Akizungumza, Alex ameeleza kuwa vijana hao walimuita ili awapeleke eneo la Kambi ya Fisi, akisema tayari alikuwa amewahi kuwapeleka sehemu mbalimbali zaidi ya mara tatu.

β€œHawa vijana wameniita kuwapeleka mtaa wa Kambi ya Fisi, nilivyokuja kumbe hawa vijana tabia zao sizijui. Nimeshakuja zaidi ya mara tatu nawachukua na kuwapeleka mahali wanataka,” amesema Alex.

Kuhusu mafuta yaliyodaiwa kukutwa katika chumba hicho, Alex amesema ni mafuta ya kawaida ya kujipaka ambayo yanaweza kutumika katika sehemu mbalimbali za mwili.

Mke wa Alex aliyefika eneo la tukio baada ya kupata taarifa amesema ameshtushwa na tukio hilo, akieleza kuwa anamfahamu mume wake kama mtu wa dini na mwimbaji wa kwaya.

Balozi wa eneo hilo, Lydia Danieli, amesema analifahamu tukio hilo na kwamba baadhi ya mienendo ya vijana hao ilikuwa imewahi kuwafanya wananchi kuwa na mashaka.

Jeshi la Polisi lilifika katika eneo hilo na kumchukua Alex kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.

View attachment 3675305
Hapo penye mtu wa dini na mwimbaji wa kwaya ndipo palipokuvutia zaidi
 
Hii nchi ngumu hii. Sasa hawa si watu wazima wanaburudika kama wanavyonunua machangu? Kipigo hicho kakosa nini? Awageuzie kibao hao waliompiga ili wajue sheria.
Inaonekana ushawahi kupata hiyo "burudani".

Wakuu nimekuja kugundua JF sio sehemu salama sana kwa afya zetu za akili comrades. Maudhui tunayoyapata humu yanapaswa kuchunguzwa na sio kufuata kila jambo kisa limewekwa JF. Tupo wengi humu na kila aina ya tabia ipo hapa. Mwisho naomba wanajamvi tuzidi kumsogelea M/Mungu kila mtu kwa imani yake.
 
Back
Top Bottom