Mtu menopause bado,kwanini asiwe na hamu?..ushafika miaka 42 ukaona hilo?
Kwani menopause inaanza ghafla bin vuu?
Ipo kama mvua inavotaka kunyesha, huanza kwa dalili!
Sasa usimshangae Wangari kushangaa umri huo kwa mwanamke kuwa kizabizabina wa kitanda!
Kwa 42-50 inategemeana mtu na mtu, wengi hamu huanza kuwa ni za kusikilizia, kama pikipiki tunasema huwaka 'kwa kiki' ama kama ni gari kwa 'handling'.
Sasa hapo mwanamke huanza kuigiza ama kutumika kuridhisha mwanaume bila yeye kujisikia na hatimaye yakimfika kabisa, huomba talaka ya kitanda.
Kama mwanaume ni 'msomi' huitoa kwa kugawana vyumba ili wasisumbuane.
Majirani na watu wasiohusika hamuwezi kuelewa lolote hapo, maana upendo wa nje kwa watu hao huongezeka maradufu, wakipika na kupakuliana kwa furaha pamoja
maana wajibu wao wa kuijaza dunia washaufanya na kuutimiza.
Na hayo ndiyo mapenzi ya kweli na ya dhati kabisa.
Sent using
Jamii Forums mobile app