Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lol! Nimecheka sana mkuu, hasa hiyo code ya Namibia.Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.
Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
Kumbe?Shida nyingine majina yote ni ya waarabu.
Waarabu na ugaidi ni kama samaki na maji
Muamala wa umeme ulikuwa mmoja, labda alitaka kuwapoteza wachunguzi kwa kuipeleka simu kwenye njia nyingine, ila muamala ukairudisha simu kwenye mfumo.Nafikiri kuna ushahidi Mwingine zaidi ha huu ulioeleza hapa.
Haitoshi kumtia mtu hatiani.
Simu ya Njoroge, Mita ya Umeme ya Njoroge na Namba ya Nyumba ya Njoroge.
Yaani simu itumike kwenye uharifu badala ya kuiharibu yeye anaiuza tena?
Huyo Gaidi gani hajielewi
Shambulio la mwaka 1998 Yuesi Embassy, wazee wakaingia mtaani kutafuta wahalifu wanaohusika, wakakamata watu sehemu tofauti jijini wanaosadikika kuhusika.Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.
Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
Braza wenzetu wako vizuri wanakufata baada ya kujua ukweli.Mzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena..m
Watumwa wao watasema ni marekani anauchafua uislam,kweli ibilisi ni baba wa uongo!Shida nyingine majina yote ni ya waarabu.
Waarabu na ugaidi ni kama samaki na maji
Nilikuwa najikumbusha thread inayohusu hilo tukio.Shambulio la mwaka 1998 Yuesi Embassy, wazee wakaingia mtaani kutafuta wahalifu wanaohusika, wakakamata watu sehemu tofauti jijini wanaosadikika kuhusika.
CIA walipofika kujiridhisha ile kuwatizama tu wale raia waliokamatwa, jamaa wakasema hatuoni gaidi hata mmoja hapa
Gereji alifungwa na alikaa miaka kuja kutoka hakukaa sana akafa. NinamjuaMzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena mbele ya M16 na CIA, huyo mtu alikuwa na deep connection na hao wahusika, bongo hapa yule ambae gereji yake ilitumika mbona aliachiwa? Hawakufungi kizembe hao jamaa, ukinaswa jua upo kweli
Vipi kama mnunuaji wa hizo token alikosea,akanunua token za huyo muhusika?
Watamuamini?
Yule muuza maziwa wa bongo alipona kwakuwa ana jina la kigalatiaMzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena mbele ya M16 na CIA, huyo mtu alikuwa na deep connection na hao wahusika, bongo hapa yule ambae gereji yake ilitumika mbona aliachiwa? Hawakufungi kizembe hao jamaa, ukinaswa jua upo kweli
Unakumbuka tukio la kigaidi lililotokea Kampala, Uganda wakati wa mechi ya fainali ya World Cup 2010, kati ya Spain na Holland?
Tukio lile lilimfanya mtangazaji wa Radio Salaam FM ya Mombasa, Habib Suleiman Njoroge kuingizwa kwenye kesi ya ugaidi wa tukio lile, na sasa anatumikia kifungo cha maisha.
- Unajua Ilikuwaje?
Mara tu baada ya lile tukio, vikosi vya upelelezi vya MI6 na FBI ni miongoni mwa vikosi vilivyoalikwa ili kufanya uchunguzi, kwa ajili ya kufanikisha kuwanasa wahusika wote.
Jambo la kwanza waligundua mabomu yote yaliyotumika katika tukio lile yaliundwa Mombasa nchini Kenya, na yakasafirishwa kwa basi hadi Malaba, mpakani mwa Kenya na Uganda.
Kisha, Mtanzania (Seleman Hijar Nyamandondo) aliyasafirisha hadi Kampala kwa gari aina ya Land Qruiser (Pickup) na kuyafikisha kwa aliyekuwa Msuka Mipango Mkuu, Issa Ahmed Luyima.
- Alivyoingizwa Mtangazaji!
Vikosi hivyo vya uchunguzi vilibaini, moja ya simu (device) zilizowasiliana na waliolipua mabomu yale, bado ilikuwa ikitumika huko maeneo ya Ukambani, nchini Kenya kwa namba tofauti na ya awali.
Kazi ya kuisaka simu hiyo ikaanza na ikanaswa ikiwa mikononi mwa mchuuzi wa sokoni, Mohamed Adan Abdow naye akiuziwa na Mtanzania, Husein Agade huku akiwa sokoni hapo.
Baada ya simu (device) hiyo kunaswa na kufanyiwa uchunguzi ikagundulika kwamba, iliwahi kufanya huduma ya kununua umeme (kama Luku), wa mita ya nyumba anayoishi mtangazaji huyo, Njoroge iliyopo Mombasa.
Hilo liliwatosha wachunguzi hao kuamini kwamba magaidi hao waliishi kwenye nyumba ya Njoroge wakati wakiunda mabomu hayo na ndiyo maana waliwajibika kulipa bili ya umeme.
- Funzo Kuu
Hiki kilichotokea kwa mtangazaji, Njoroge ni kama ambavyo mhalifu yeyote angelipia kisimbuzi chako au umeme wa mita yako kwa simu yake na moja kwa moja ukaingizwa mtegoni, endapo simu yake itachunguzwa.
Hivyo, si vema kupokea huduma za kulipiwa vifaa vyako vya nyumbani pasipo kumjua vizuri unayemwomba akulipie.
Ova