Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.

Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
Lol! Nimecheka sana mkuu, hasa hiyo code ya Namibia.

Ova
 
Nafikiri kuna ushahidi Mwingine zaidi ha huu ulioeleza hapa.

Haitoshi kumtia mtu hatiani.

Simu ya Njoroge, Mita ya Umeme ya Njoroge na Namba ya Nyumba ya Njoroge.

Yaani simu itumike kwenye uharifu badala ya kuiharibu yeye anaiuza tena?

Huyo Gaidi gani hajielewi
Muamala wa umeme ulikuwa mmoja, labda alitaka kuwapoteza wachunguzi kwa kuipeleka simu kwenye njia nyingine, ila muamala ukairudisha simu kwenye mfumo.

Maana kuna watu waliiba TV kubwa yenye kifaa cha kuitambua iliko, kisha wezi wakafanikiwa kujua kilipo wakaking'oa kisha wakakiweka kwenye daladala.

Wachunguzi wakaanza kuhangaika na safari za daladala, huku TV yao inazidi kwenda. Hapo uchunguzi ulifanikiwa kupotezwa maboya.

Ova
 
Wangekuwa wachunguzi wa nchi ya Namibia hata wasingejisumbua kufika kote huko. Angekamatwa mtu mmoja ambaye hahusiki kabisa, kisha kupewa kesi zote kuanzia kupanga hadi kutekeleza, halafu anaunganishwa na watu wake wa karibu wanaokunywaga bia pamoja.

Wale watu akili zipo kwenye mafuta ya tumboni.
Shambulio la mwaka 1998 Yuesi Embassy, wazee wakaingia mtaani kutafuta wahalifu wanaohusika, wakakamata watu sehemu tofauti jijini wanaosadikika kuhusika.

CIA walipofika kujiridhisha ile kuwatizama tu wale raia waliokamatwa, jamaa wakasema hatuoni gaidi hata mmoja hapa😂.
Ni wale walevi, wezi na wanywa gongo.😂.
Bongo sio poa.
 
Ilitokea Vodacom kipindi kile Vodacom inaanza Anza. Kulikua na mzungu mnoko, Sasa washahili wakajisemea tununue laini mpya Kisha tumtumie mzungu meseji za matusi. Kosa walilofanya waliweka Ile laini mpya kwenye moja ya simu zao.
Walinaswa asubuhi kweupe Tena mapema Sana.
 
Omar, Njoroge and Mbuthia were linked by telephone records to a mobile phone that was attached to a third suicide bomb vest, which failed to explode. Kenyan media reports have claimed Omar was a leading figure in the bomb plot.
 
Shambulio la mwaka 1998 Yuesi Embassy, wazee wakaingia mtaani kutafuta wahalifu wanaohusika, wakakamata watu sehemu tofauti jijini wanaosadikika kuhusika.

CIA walipofika kujiridhisha ile kuwatizama tu wale raia waliokamatwa, jamaa wakasema hatuoni gaidi hata mmoja hapa
Nilikuwa najikumbusha thread inayohusu hilo tukio.
Eti polisi wa bongo waliwakamata watu kibao wakawasweka central. FBI walivyofika wakaambiwa kuna watuhumiwa wa ugaidi wapo ndani, jamaa wakasema tunaomba tuwaone.
Jamaa kuwaona wakasema hakuna gaidi hata mmoja hapa labda vibaka.

Jamaa walivyoingia kazini sasa ndio wakawanasa wahusika wote na jinsi mpango mzima ulivyosukwa na kuna jamaa wa kimara huyo alishirikishwa bila kujua.
 
Mzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena mbele ya M16 na CIA, huyo mtu alikuwa na deep connection na hao wahusika, bongo hapa yule ambae gereji yake ilitumika mbona aliachiwa? Hawakufungi kizembe hao jamaa, ukinaswa jua upo kweli
Gereji alifungwa na alikaa miaka kuja kutoka hakukaa sana akafa. Ninamjua
 
Tanzania huwezi kuendesha gari likiwa na bomu bila kunaswa na rada za jeshi. Ndiyo maana huwa nawaambia watu kiulinzi tuko vzr sana. Mnakumbuka wale jamaa wa rufiji walivyonaswa na kupotezwa walipohama na kukimbilia huko mapori ya morogoro?
 
Mzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena mbele ya M16 na CIA, huyo mtu alikuwa na deep connection na hao wahusika, bongo hapa yule ambae gereji yake ilitumika mbona aliachiwa? Hawakufungi kizembe hao jamaa, ukinaswa jua upo kweli
Yule muuza maziwa wa bongo alipona kwakuwa ana jina la kigalatia
 
Unakumbuka tukio la kigaidi lililotokea Kampala, Uganda wakati wa mechi ya fainali ya World Cup 2010, kati ya Spain na Holland?

Tukio lile lilimfanya mtangazaji wa Radio Salaam FM ya Mombasa, Habib Suleiman Njoroge kuingizwa kwenye kesi ya ugaidi wa tukio lile, na sasa anatumikia kifungo cha maisha.

- Unajua Ilikuwaje?

Mara tu baada ya lile tukio, vikosi vya upelelezi vya MI6 na FBI ni miongoni mwa vikosi vilivyoalikwa ili kufanya uchunguzi, kwa ajili ya kufanikisha kuwanasa wahusika wote.

Jambo la kwanza waligundua mabomu yote yaliyotumika katika tukio lile yaliundwa Mombasa nchini Kenya, na yakasafirishwa kwa basi hadi Malaba, mpakani mwa Kenya na Uganda.

Kisha, Mtanzania (Seleman Hijar Nyamandondo) aliyasafirisha hadi Kampala kwa gari aina ya Land Qruiser (Pickup) na kuyafikisha kwa aliyekuwa Msuka Mipango Mkuu, Issa Ahmed Luyima.

- Alivyoingizwa Mtangazaji!

Vikosi hivyo vya uchunguzi vilibaini, moja ya simu (device) zilizowasiliana na waliolipua mabomu yale, bado ilikuwa ikitumika huko maeneo ya Ukambani, nchini Kenya kwa namba tofauti na ya awali.

Kazi ya kuisaka simu hiyo ikaanza na ikanaswa ikiwa mikononi mwa mchuuzi wa sokoni, Mohamed Adan Abdow naye akiuziwa na Mtanzania, Husein Agade huku akiwa sokoni hapo.

Baada ya simu (device) hiyo kunaswa na kufanyiwa uchunguzi ikagundulika kwamba, iliwahi kufanya huduma ya kununua umeme (kama Luku), wa mita ya nyumba anayoishi mtangazaji huyo, Njoroge iliyopo Mombasa.

Hilo liliwatosha wachunguzi hao kuamini kwamba magaidi hao waliishi kwenye nyumba ya Njoroge wakati wakiunda mabomu hayo na ndiyo maana waliwajibika kulipa bili ya umeme.

- Funzo Kuu
Hiki kilichotokea kwa mtangazaji, Njoroge ni kama ambavyo mhalifu yeyote angelipia kisimbuzi chako au umeme wa mita yako kwa simu yake na moja kwa moja ukaingizwa mtegoni, endapo simu yake itachunguzwa.

Hivyo, si vema kupokea huduma za kulipiwa vifaa vyako vya nyumbani pasipo kumjua vizuri unayemwomba akulipie.

Ova


Ninaamini kuna maelezo mengi zaidi yaliyomfanya afungwe na sio ulichoeleza peke yake.
 
Back
Top Bottom