Agenda kuu ya uchumi ya Rais Samia ni ipi? Royal Tour?

Agenda kuu ya uchumi ya Rais Samia ni ipi? Royal Tour?

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,162
Reaction score
9,073
Enzi za Kikwete mlituambia uchumi wa gesi!!

Magufuli mkatuambia wa viwanda.

Hussein Mwinyi kule Zanzibar tunaambiwa wa uchumi BULUU.

Huyu Mama yenu yeye agenda kuu ya kiuchumi ni ipi?!! Royal Tour?!!

Nchi ndogo kama Rwanda inatangaza utalii kwenye ligi kuu ya England kupitia team ya Arsenal na pia ligi kuu ya Ufaransa kupitia PSG,huyu wa filamu iiyotumia mabilioni ya hela ambae anafanya jitihada za watu kutazama documentary,ina manufa makubwa yapi?!!

Mfano wa Rwanda kutumia Arsenal na PSG, tafakari kwa mwezi inatangazwa kwa watu million ngapi hapo Ulaya tu,bado Asia na kwingineko. Achana na huku Afrika tunapotazama mpira kwa ajili ya kubeti na kubishana, Ulaya ndio yenye watalii wengi wanaokuja Afrika.

Huko America watalii wengi wanaenda kutalii South America.

Mzungu kutoka America kuja kutalii Tanzania inamuhitaji hela nyingi saana haswa kwenye usafiri tu maana inabidi apande ndege kupitia Europe then Africa, na Africa yenyewe atazungusgwa transit nchi nyingine kabla ya kutua Tanzania!

Ili aje direct Tanzania inabidi apande direct flight ambapo hakuna kwa Tanzania to USA kwani ni more than 14hrs ndege kua hewani.

Kati ya Amerika na Ulaya,Tanzania inapokea watalii wengi kutoka ukaya,kwa nini watawala wameelekeza nguvu kubwa Marekani?

Walioasisi hii bongo movie ya royal Tour walikosa njia bora zaidi ya kutangaza na kuboost utalii wetu?!

Agenda kuu haswa ya kiuchumi kwa Rais Samia ni ipi?
 
Hili la KUUPIGA MWINGI HUJALIONA AU NI KIBURI CHAKO TU ?
Kuupiga mwingi kwenye jipi?!! Bei za vifaa vya ujenzi?!! Bei za vyakula?!! Bei za mafuta na usafiri wa umma kwa ujumla?!!

Anaupiga mwingi kwenye jipi haswaa?!!

Ama hiyo propaganda ya neno kuupiga mwingi ndio uchumi wenyewe?!!
 
Mama yeye ameamua asidanganye watu awe mkweli tu. Pale anapoona ukweli anasema ukweli bila muhali.

Hivyo kwenye uchumi yeye anakuza sekta zote kwa kadiri ya uwezo wake kwa kushirikiana na watanzania wote.

Pia anaamini "success is attracted not forced and we get what we deserve not what we say' yaani mafanikio huvutiwa sio kulazimishia ndio maana anaenda na royal tour kwa mfano. So mama anatransform utopian economic approaches tu scientific methods.

Tupo pamoja?
 
Kuupiga mwingi kwenye jipi?!! Bei za vifaa vya ujenzi?!! Bei za vyakula?!! Bei za mafuta na usafiri wa umma kwa ujumla?!!

Anaupiga mwingi kwenye jipi haswaa?!!

Ama hiyo propaganda ya neno kuupiga mwingi ndio uchumi wenyewe?!!
Wewe ungekuwa rais, ungefanya nini kuzuia mfumuko wa bei? Mfano ungefanyaje ili mafuta yasipande?
Tumepigwa na kitu kizito sana chenye ncha kali kichwani...
Wapigwe tu, tuneshachoka! Kama mtu anaambiwa kitu hasikii lazima atapigwa tu!
 
Viti vitapanda bei, kilakitu kitapanda bei na kila mmoja akule kwa urefu wa kamba yake
Ulitaka atudanganye kuwa tutaingia uchumi wa kati na sisi ni dona kantri wakati anajua sio?

Kwani nani asiyejua kuwa technically mafuta yakipanda hupelekea na vitu vingine kupanda bei? Watu mmezoea kudanganywa mpaka mkiambiwa ukweli mnaona kama vile mnaonewa.

Mama ni kiongozi muadilifu anayejaribu ku practice to her level best.
 
Kuupiga mwingi kwenye jipi?!! Bei za vifaa vya ujenzi?!! Bei za vyakula?!! Bei za mafuta na usafiri wa umma kwa ujumla?!!

Anaupiga mwingi kwenye jipi haswaa?!!

Ama hiyo propaganda ya neno kuupiga mwingi ndio uchumi wenyewe?!!
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Wewe ungekuwa rais, ungefanya nini kuzuia mfumuko wa bei? Mfano ungefanyaje ili mafuta yasipande?

Wapigwe tu, tuneshachoka! Kama mtu anaambiwa kitu hasikii lazima atapigwa tu!

Kazi kuu ya serikali ni kuhudumia wananchi na sio kujali kukusanya kodi tu,ningetoa tozo zisizo na ulazima kwenye mafuta, mfano Tanzania kwenye mafuta kuna tozo zaidi ya 10!!!

Serikali kama serikali,tungeenda kuongea na nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi,kama Saudia,Qatar etc,tuingie makubaliano ya nchi kununua mafuta direct kutoka kwa nchi mzalishaji baadala ya wafanyabiashara,hii ingesaidia pia kushusha bei.

Serikali kupitia wizara ya uchukuzi,ingenunua meli kubwa ya kusafirishia mafuta, kupunguza gharama pia ya usafiri wa kuleta.

Mfano inajenga kivuko Mwanza kwa 97bln,kwa nini ishindwe lununua meli ya mafuta?!!!
 
Halafu mleta mada unasema ;Rwanda wanatangaza utalii kupitia Arsenal, so unataka tuwe watu wa kudesa bila ubunifu wowote? Unasema royal tour itasaidia nini? Si usubiri uone? Unataka ujauzito utunge leo na mtoto leo leo?

Unasema kutoka marekani hadi tanzania hela nyingi, sasa wamarekani wamekuambia hawana hela?

Haya unasema hakuna ndege za moja kwa moja, si juzi mmeambiwa kutakuwa na route ya moja kwa moja toka U.S.A mkawa mnapinga humu humu? Sasa mnatakaje kwa mfano?
 
Kazi kuu ya serikali ni kuhudumia wananchi na sio kujali kukusanya kodi tu,ningetoa tozo zisizo na ulazima kwenye mafuta, mfano Tanzania kwenye mafuta kuna tozo zaidi ya 10...
Mfano taja kwa majina, tozo zipi ungezifuta kwenye mafuta? Kwa kufuta tozo husika, ungepunguza bei ya mafuta kwa sh. Ngapi kwa kila kila lita? Ni madhara gani ambayo yatajitokeza kwa kufuta tozo husika na utayakabili vipi? Au hakutakuwa na madhara yoyote?

Unasema tuchukue mafuta moja kwa moja kutoka Qatar, Kwani sasa tunachukulia wapi, na kwa nini Qatar na hiyo itasaidiaje?

Unasema serikali ikachukue mafuta moja kwa moja, so unakusudia serikali ndio iwe inafanya biashara? Unajua madhara ya serikali kufanya biashara? Unakumbuka nini kilitokea baada ya serikali kuamua kufanya biashara ya korosho?

Unasema serikali inunue meli ya mafuta, aliekuambia kinachopandisha mafuta ni meli binafsi ni nani? So ili kushusha nauli za mabasi serikali inunue mabasi ibebe abiria? Unajua air Tanzania imekuwa ikiendeshwa kwa hasara? Unafanya analyisis au unatafuta mtu wa kulaumu tu?
 
Mfano taja kwa majina, tozo zipi ungezifuta kwenye mafuta? Kwa kufuta tozo husika, ungepunguza bei ya mafuta kwa sh. Ngapi kwa kila kila lita? Ni madhara gani ambayo yatajitokeza kwa kufuta tozo husika na utayakabili vipi? Au hakutakuwa na madhara yoyote...

Maswali yako yanajirudia ila naamini umeelewa!!! Naamini mwanga umeuona.

Jikite kwenye hoja kuu ya bandiko sasa!!
 
Maswali yako yanajirudia ila naamini umeelewa!!! Naamini mwanga umeuona.

Jikite kwenye hoja kuu ya bandiko sasa!!
Majibu ya bandiko lako haya;
=================
Mama yeye ameamua asidanganye watu awe mkweli tu. Pale anapoona ukweli anasema ukweli bila muhali.

Hivyo kwenye uchumi yeye anakuza sekta zote kwa kadiri ya uwezo wake kwa kushirikiana na watanzania wote.

Pia anaamini "success is attracted not forced and we get what we deserve not what we say' yaani mafanikio huvutiwa sio kulazimishia ndio maana anaenda na royal tour kwa mfano. So mama anatransform utopian economic approaches tu scientific methods
 
Akimbie kwa lipi ? Uchumi wa nchi hauwezi kutegemea jambo moja tu , kuna masuala ya kidemokrasia , haki na usalama , bila Katiba mpya Royal Tour ni bure
Kuhusu demokrasia,mazungumzo yanaendelea na negociation & reconciliation ni hatua. Ni heri moja kuliko mbili nenda rudi.
 
Enzi za Kikwete mlituambia uchumi wa gesi!!

Magufuli mkatuambia wa viwanda.

Hussein Mwinyi kule Zanzibar tunaambiwa wa uchumi BULUU.

Huyu Mama yenu yeye agenda kuu ya kiuchumi ni ipi?!! Royal Tour?!!

Nchi ndogo kama Rwanda inatangaza utalii kwenye ligi kuu ya England kupitia team ya Arsenal na pia ligi kuu ya Ufaransa kupitia PSG,huyu wa filamu iiyotumia mabilioni ya hela ambae anafanya jitihada za watu kutazama documentary,ina manufa makubwa yapi?!!

Mfano wa Rwanda kutumia Arsenal na PSG,tafakari kwa mwezi inatangazwa kwa watu million ngapi hapo Ulaya tu,bado Asia na kwingineko. Achana na huku Afrika tunapotazama mpira kwa ajili ya kubeti na kubishana,Ulaya ndio yenye watalii wengi wanaokuja Afrika.

Huko America watalii wengi wanaenda kutalii South America.

Mzungu kutoka America kuja kutalii Tanzania inamuhitaji hela nyingi saana haswa kwenye usafiri tu maana inabidi apande ndege kupitia Europe then Africa,na Africa yenyewe atazungusgwa transit nchi nyingine kabla ya kutua Tanzania!!

Ili aje direct Tanzania inabidi apande direct flight ambapo hakuna kwa Tanzania to USA kwani ni more than 14hrs ndege kua hewani.

Kati ya Amerika na Ulaya,Tanzania inapokea watalii wengi kutoka ukaya,kwa nini watawala wameelekeza nguvu kubwa Marekani?!!

Walioasisi hii bongo movie ya royal Tour walikosa njia bora zaidi ya kutangaza na kuboost utalii wetu?!

Agenda kuu haswa ya kiuchumi kwa Rais Samia ni ipi?!!
Hivi fucking Royal Tour ina faida gani haswa
 
Back
Top Bottom