Agenda ya Mohamed Said ina ukakasi

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Huyu mzee wangu wa gerezani aangaliwe vizuri.

Nakubali ni msomi mzuri hapa nchini, nakubali ana busara ila anatumia akili zake kucheza na akili za watu.

Sijawahi kusikia popote duniani mtu anajiita mwana historia kwa kubobea kwenye kata moja tu.

Mohamed Said anajiita mwanahistoria lakini ukimfuatilia hana anachojua zaidi ya historia ya Kariakoo.

Maandishi yake yana udini ndani yake, mara nyingi ndiyo agenda kuu ya kila anachoandika, udini. Ngugi wa Thiong'o aliwahi kutunga kitabu akasifiwa na Mzee Kenyatta, lakini kumbe kitabu kinamsema vibaya, alitumia literature, ambayo kila mtu huwa na tafsiri yake.

Kwa tuliosoma literature na history tunamuekewa sana huyu mzee, aporwe tuzo alizowahi kupewa.

Kuna kitabu cha "The Modern World Since 1870" na L. Snelgrove kinaelezea nchi nyingi za Ulaya zilivyoingia vitani kwa sababu ya watu dizaini ya huyu mzee.

Huyu mzee sio kilaza, yupo vizuri kichwani ila agenda yake ina ukakasi, ndio maana kipindi cha nyuma alijistukia akawa anaandika kimachale machale kumuogopa bwana yule.
 
Wewe huna hoja yoyote ya maana. Huyu unaemshutumu kasoma na KAISHI ndani ya hiyo historia anayo zungumzia.

Lazima pale historia ilipo pindishwa inyooshwe hii ni kwa maslahi ya jamii yote. Kama una hoja tofauti na anayoandika leta hoja na ushahidi wako tuamue na sio kushutumu kws kuleta mambo ya usalama.

Wote tunaomba nchi yetu ibaki salama hata kama tuna mawazo tofauti.

Mzee Mohammef endelea na kazi. We ni Johari ya historis ilio hai.
 
Nasimama kumtetea mzee Mohamed Said

Pale mwanzoni wakati anajiunga na JF akaanza kuweka makala zake nilikuwa namuona ni instigator fulani hivi. Lakini nikajipa muda kusoma makala zake kwa kina nikagundua huyu mzee anastahili nafasi kwenye jamii kwa sababu amesimama kutueleza ukweli uliofichwa kuhusu Tanzania hii unayoiona.

Kitu kingine nimeelewa namna uhalifu wa kijamii unaotendwa na state against Muslims kielimu ba kihistoria. Kuna mambo tunapaswa kuyaangalia kwa kina ili kuondoa future commotions kama zinazoendelea maeneo mengine duniani.

Nasema hivii, nasema hivii. Tumkosoe Mzee Mohamed kwa hoja bila kuinstigate chuki na kupeana majina mabaya.
 
Huyu mzee sio kilaza ila ni mchochezi
 
Huyu akipewa nafasi kuna kikundi cha watu kitapata shida sana,ana chuki sana na watu wasio wa mrengo wake,apuuzwe
 
Mwambie na Faiza Foxy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…