Huyu mzee wangu wa Gerezani aangaliwe vizuri.
Nakubali ni msomi mzuri hapa nchini, nakubali ana busara ila anatumia akili zake kucheza na akili za watu.
Sijawahi kusikia popote duniani mtu anajiita mwana historia kwa kubobea kwenye kata moja tu,.
Mohamed Said anajiita hi historian lakini ukumfuatilia hana anachojua zaidi ya historia ya kariakoo.
Maandishi yake yana udini ndani yake,mara nyingi huwa ndio agenda kuu ya kila anachoandika, udini. Ngugi wa Thiong'o aliwahi kutunga kitabu akasfiwa na mzee Kenyatta kumbe kItabu kinamsema vibaya,alitumia literature,ambayo kila mtu huwa na tafsiri yake.
Kwa tuliosoma literature na history tunamuekewa sana huyu mzee,aporwe tuzo alizowahi kupewa.
Kuna kitabu cha The Modern World Since 1870 by L Snelgrove kinaelezea nchi nyingi za ulaya zilivyoingia vitani kwa sababu ya watu dizaini ya huyu mzee.
Huyu mzee sio kilaza, yupo vizuri kichwani ila agenda yake ina ukakasi,ndio maana kipindi cha Nyuma alijistukia akawa anaandika kimachale machale kumuogopa bwana yule.