Car4Sale Agiza gari kutoka South Africa

Car4Sale Agiza gari kutoka South Africa

🤣😅😅😅 Mtu akitaka kununua gari hapa lazima twende traffic register tukajiridhishe kwamba muuzaji ndiye mmlikia wa chombo. Kama ni dealerships pia kuna taratibu zake.
....police interpol clearance certificate ni documents muhimu mno,pia angalia isiwe ni bank financed car..otherwise gari za kwa Madiba ni top class one,binafsi nazipenda na kuziamini sana
 
Hio sio sababu watu wana-forge documents huwezi kubali ila vita vingi vya south afrika vinanuka damu za watu
Huu ni uongo,kunuka damu ?,sio kweli na unaposema watu wana forge documents ni ngumu maana SA wana systems nzuri zaidi kuliko tuliyokua nayo hapa nchini,kule ID yao inaongea kwenye systems zote za nchi
 
Ila hunijui alafu unaniambia huna hela stress zako za maisha tafuta sehemu za kupeleka
Fair enough ila usiandike uongo hapa,ukweli utamalaki na huwezi ukaniambia kuwa eti magari mengi ya SA ni ya wizi wakati Dar imejaa magari mengi ya SA yaliyo safi
 
Hiyo 65 milioni ni pamoja na TRA au au ni ya gari tu bila usajili?
Screenshot_20240326_120110_Chrome.jpg
 
Hio sio sababu watu wana-forge documents huwezi kubali ila vita vingi vya south afrika vinanuka damu za watu
Yes kuna ukweli fulani lakini nipo hapa na maisha tunayoishi ni tofauti na mtu anavyosikia kwenye vyombo vya habari. Kuna mengi sana mazuri kuliko mabaya,pia ni cycle za watu tunaojihusisha nao zinaweza kukuweka mtu matatani. Kama umenyooka basi utaishi vizuri tu.
 
....police interpol clearance certificate ni documents muhimu mno,pia angalia isiwe ni bank financed car..otherwise gari za kwa Madiba ni top class one,binafsi nazipenda na kuziamini sana
Karibu sana chief,bank financed cars huuzwa kwa minada au insurance companies kama zimepata ajali au majanga ya aina yoyote. Suvs na pickup cars za kisasa hapa na nafuu kuliko kuagiza UK au Japan.
 
Ndo ukweli unaponunua bidhaa ya mtumba kutoka south afrika kuwa makini
Nyingine watu wameuliwa ndo zimepatika kwa njia ya kuporwa
Umetoa tahadhari ya kweli Kabisa.

Nina ndugu yangu alipata mkasa mkubwa alinunua gari kumbe liliibwa South na Mmliki aliuwawa katika tukio Hilo, maaskari wa Interpol wakabaini lipo Tanzania, kesi ilimtesa sana alikaa segerea miezi kadhaa.

Ilihitaji fedha, Muda na connection kuhakikisha ananasuka katika huo msala.
 
Ndo ukweli unaponunua bidhaa ya mtumba kutoka south afrika kuwa makini
Nyingine watu wameuliwa ndo zimepatika kwa njia ya kuporwa
Usipake matope biashara za watu. Kinachotakiwa ni mnunuzi kuzingatia procedure sahihi. Kama Mali za wizi hata nchini kwetu zipo kwa wingi.
 
Usipake matope biashara za watu. Kinachotakiwa ni mnunuzi kuzingatia procedure sahihi. Kama Mali za wizi hata nchini kwetu zipo kwa wingi.
Sipaki matope bali ndo ukweli na sijasema yeye anauza mali ya uwizi ila nimesema bidhaa nyingi za south africa ni za uwizi ni kama tahadhari tu
 
Jamaa yangu aliingiza Toyota Hilux ya 2017,ile ni 2.8 GD6 alilipa ushuru 23 milion kwa maelezo yake. Lakini pia ukichek kwenye calculator ya tra utaona double cabins zina ushuru rafiki kuliko Suv,mfano Hilux/Fortuner au Ranger/Everest.

Pia hapa South Africa Kuna options za kununua gari zilizopata ajali na kuzitengeneza kisha kuleta Tz. Wengi wanafanya biashara hiyo,gari zinakua cheap kununua,garage wanafix chuma inakua kama mpya kuanzia replacement parts mpaka rangi.
Bado sijapata uelewa vizuri kuhusu import duty. Kwa sababu ya kuwa members wa SADC hatupaswi kulipa import duty kwa magari yanayozalishwa ndani ya SADC.
 
Back
Top Bottom