Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Ninaangalia hapa kitindi cha Chetu ni Chetu kupitia ITV, naona malalamiko ya wafanyabiashara wadogo ndani ya stendi ya Igunga wakilalamikia agizo la Waziri wa Uchukuzi kuruhusu mabasi yanayosafirisha abiria kutotumia stendi za Halmashauri zilizojengwa kwa fedha ya kodi zetu.
Athari zake pamoja na haya malalamiko ya wajasiriamali ambao wapo kwenye maeneo hayo maalumu ya stendi kukosa wateja, Halmashauri kukosa mapato yake halali ya ushuru wa magari yanaotumia stendi hizo.
Ikumbukwe pia kila Halmashauri ina vyanzo vyake vya ndani vya mapato ikiwemo ushuru wa stendi hizi.
Halmashauri hizi Inawajibika kisheria kutoa asilimia 10% ya mapato yake kuwapatia mikopo nafuu kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.
Wachuuzi ndani ya stendi hiI hulipia uahuru wa pango kwa Halmashauri. Tegemeo lao ni abiria wanaotumia vituo hivyo vikuu vya Halmashauri.
Tamko la Waziri limesababisha mkanganyiko na kupelekea hasara ya kuviendesha vituo hivyo ikiwa vitakosa mapato ya uhakika.
Inawezekana agizo ama tamko la Waziri kwamba endapo basi halina abiria wa kushuka s basi lisilazimike kupitia stendi hizo likawa na nia ya kupunguza usumbufu kwa waendeshaji wa vyombo vya usafiri. Lakini ifanyike tathmini ya kina kuhusu athari zinazoweza kujitokeza.
Nchi Yetu,
Maendeleo Yetu,
Tupate Katiba yetu.