MABADILIKO NI MUHIMU ILI KUENDANA NA NYAKATI.
Tujadili kwa ku-balance Pande Zote!
Ni kweli,halmashauri za wilaya zinapaswa kuwa na vyanzo vyao vya Mapato.
Stendi kuu za mabasi kwa kila wilaya,zinakuwa kichocheo cha mzunguko wa pesa,Ikiwemo mapato ya halmashauri na pia wafanyabiashara na wachuuzi wa bidhaa husika kwenye hizo stendi.
Lakini ingewekwa sheria ya miji mikuu ya kila wilaya pekee.
Na sio huu utaratibu wa kila mji unaokuwa jirani na barabara kuu,kulazimisha Magari kuingia stendi,hata pale yanapokuwa yamejaza abiria wa moja kwa moja.
Huo ni upotezaji wa muda na hasara kwa abiria na pia waendeshaji wa hivyo vyombo vya usafiri.
Kwa sababu,vinapoteza muda wa abiria,pamoja na raslimali mafuta.
Bila kusahau ule ushuru wa Tozo,ambazo wanalazimishwa kulipa eti kusa tu,kaingia stendi.ebu fikiria kuanzia Dar-Mza kwa mfano.
Kwa kuingia,kusimama na baadae kurudi njia kuuu.
Wanalazimika kutenga shilingi ngapi kwa safari nzima?
Pia ni Jambo linalowasababishia usumbufu abiria,kutokana na kuchelewa kufika,na kulazimika kuingia gharama za ziada,kutokana na kufika usiku.
Hivyo kulipishwa gharama ambazo ni za nje ya muda rasmi wa kazi....mathalani Taxi na Bodaboda.
Na hata wengine kulazimika kulala Guest Houses,sababu hawawezi ku-risk usiku huo.
Pia linawahatarishia usalama wao,sababu ya kufika usiku sehemu ambazo wengi wanakuwa wageni pia.
Halmashauri,bado zinao uwezo wa kukusanya mapato kupitia stendi zake,kwa kutumia yale mabasi ambayo yatalazimika kuingia na kuchukua au kushusha abiria..
Kwa sababu sio wote watapitiliza,na pia ikumbukwe kwamba,bado kuna mabasi mengi ambayo yanatoka miji ya makao makuu ya .mikoa na kurudi wilayani kila siku.
Na tusisahau kwamba,mara nyingi hizo tozo za stendi,zimekuwa hazifiki kwenye mifuko husika,imekuwa chaka la ubadhilifu kwa watumishi wa halmashauri,wasiokuwa waaminifu.
Mabadiliko ni Muhimu ila yaendane na wakati.