Agizo la Waziri kuruhusu Mabasi kutoingia stendi ni kuwanyima Halmashauri vyanzo vya mapato

Ninaangalia hapa kitindi cha Chetu ni Chetu kupitia ITV, naona malalamiko ya wafanyabiashara wadogo ndani ya stendi ya Igunga wakilalamikia agizo la Waziri wa Uchukuzi kuruhusu mabasi yanayosafirisha abiria kutotumia stendi za Halmashauri zilizojengwa kwa fedha ya kodi zetu.

Athari zake pamoja na haya malalamiko ya wajasiriamali ambao wapo kwenye maeneo hayo maalumu ya stendi kukosa wateja, Halmashauri kukosa mapato yake halali ya ushuru wa magari yanaotumia stendi hizo.

Ikumbukwe pia kila Halmashauri ina vyanzo vyake vya ndani vya mapato ikiwemo ushuru wa stendi hizi.

Halmashauri hizi Inawajibika kisheria kutoa asilimia 10% ya mapato yake kuwapatia mikopo nafuu kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Wachuuzi ndani ya stendi hiI hulipia uahuru wa pango kwa Halmashauri. Tegemeo lao ni abiria wanaotumia vituo hivyo vikuu vya Halmashauri.

Tamko la Waziri limesababisha mkanganyiko na kupelekea hasara ya kuviendesha vituo hivyo ikiwa vitakosa mapato ya uhakika.

Inawezekana agizo ama tamko la Waziri kwamba endapo basi halina abiria wa kushuka s basi lisilazimike kupitia stendi hizo likawa na nia ya kupunguza usumbufu kwa waendeshaji wa vyombo vya usafiri. Lakini ifanyike tathmini ya kina kuhusu athari zinazoweza kujitokeza.

Nchi Yetu,
Maendeleo Yetu,
Tupate Katiba yetu.
Ni hatari sana kufikiri unaweza ukampendezesha kila mtu kwa maamuzi yako.
 
Ziliejengwa KUSHUSHA na kupandisha abiria.

Kila Gari linaajent Kwa kila Stend.
Mabasi Kabla hayajaingia Stendi tayari yana taarifa ya idadi ya abiria waliopo kwenye Stendi fulani, au hakuna abiria
Zingatia pia kuwa Kila ajent hufanya juu Chini Kupata abiria ili naye apate Pesa.
Hivyo abiria akifika Stendi hawezi kukosa Gari Kwa sababu maajenti wapo
Na maajenfi wakishakatisha tiketi abiria anapelekwa kupandia basi mjini au highway....
 
Hiyo ni kazi sasa ya halmashauri kusimamia hao maajenti katika hizo Stendi.
Pili, Madereva wa mabasi wapigwe marufuku kubeba abiria highway hasa ikiwa Stendi Ipo karibu/mjini.

Ila mabasi kuingia Stend alafu hakuna abiria WA kupanda wala kushuka, hizo ni Akili Matope
 
sawa kabisa na ilele na nane nane Dodoma unaingia kwenye foleni ya magari ya Dar saa nzima ndugu. Kama kweli waziri ametoa huo uamuzi Mungu ambariki sana.
Kwanza stand zenyewe zimekosa wasimamizi wenye akili, mfano hiyo stand kuu Dodoma ni hovyo kabisa, design ni excellent ila management no 0, kulikuwa na restaurent pzuri sana pale wameweka masharti magumu ya uendeshaji ili zife kupromote mamalishe

Stand yenyewe tangu kunakucha mpaka usiku wa manane kelele za tangazo la mkurugenzi wa jiji as if hakuna entertainment
 
Hiyo ni kazi sasa ya halmashauri kusimamia hao maajenti katika hizo Stendi.
Pili, Madereva wa mabasi wapigwe marufuku kubeba abiria highway hasa ikiwa Stendi Ipo karibu/mjini.

Ila mabasi kuingia Stend alafu hakuna abiria WA kupanda wala kushuka, hizo ni Akili Matope
Nakazia ni upuuzi uliopitiliza
 
Ninaangalia hapa kitindi cha Chetu ni Chetu kupitia ITV, naona malalamiko ya wafanyabiashara wadogo ndani ya stendi ya Igunga wakilalamikia agizo la Waziri wa Uchukuzi kuruhusu mabasi yanayosafirisha abiria kutotumia stendi za Halmashauri zilizojengwa kwa fedha ya kodi zetu.

Athari zake pamoja na haya malalamiko ya wajasiriamali ambao wapo kwenye maeneo hayo maalumu ya stendi kukosa wateja, Halmashauri kukosa mapato yake halali ya ushuru wa magari yanaotumia stendi hizo.

Ikumbukwe pia kila Halmashauri ina vyanzo vyake vya ndani vya mapato ikiwemo ushuru wa stendi hizi.

Halmashauri hizi Inawajibika kisheria kutoa asilimia 10% ya mapato yake kuwapatia mikopo nafuu kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Wachuuzi ndani ya stendi hiI hulipia uahuru wa pango kwa Halmashauri. Tegemeo lao ni abiria wanaotumia vituo hivyo vikuu vya Halmashauri.

Tamko la Waziri limesababisha mkanganyiko na kupelekea hasara ya kuviendesha vituo hivyo ikiwa vitakosa mapato ya uhakika.

Inawezekana agizo ama tamko la Waziri kwamba endapo basi halina abiria wa kushuka s basi lisilazimike kupitia stendi hizo likawa na nia ya kupunguza usumbufu kwa waendeshaji wa vyombo vya usafiri. Lakini ifanyike tathmini ya kina kuhusu athari zinazoweza kujitokeza.

Nchi Yetu,
Maendeleo Yetu,
Tupate Katiba yetu.
Wekezeni vzr Kwenye stendi zenu, baadhi ya stendi hata Maji vyooni hakuna
 
Sasa mtu hana abiria anaingia stendi akalipetu ushuru,hiyo nayo ni dhuluma.

Jambo lingine ni mikopo kwa vijana wanawake na walemavu. Sasa mbona hii habari inasifiwatu lakini hakuna uhalisia kwa baadhi ya halmashauri?
 
Back
Top Bottom