Agizo la Waziri kuruhusu Mabasi kutoingia stendi ni kuwanyima Halmashauri vyanzo vya mapato

Hii stori ilibidi imfikie mezani Waziri kuhusu ATCL haya mengine ya muziki tutayapata tuuuu!!!!
 

Matamko haya bila kuwapo kisheria yanabaki kuwa maneno matupu. Mwakyembe akiwa waziri wa usafirishaji aliwahi kuja na tamko kama hilo ambalo lilikufa kifo cha mende alipobadilishwa wizara.

Kwanini mabasi ya mikoani 'yalazimishwe' kuingia kila stendi?

Haya mengine yamekuwapo miaka nenda rudi.

Bila katiba mpya mwendo wa serikali kutowajibika kwa watu kutaendelea sana.
 
Pambana ndugu yangu utafute njia nyingine ya kuingiza kipato kuliko ya kuishi kwa kutegemea basi liingie stand
 
Sasa kama basi halina abiria anaepanda au anaeshuka hapo liingie kufanya nini. Kama ni ushuru wao wanapewa juu KWA juu. Kuna vistendi vingine eti unakuta ni lazima basi liingie tu lizunguke KISHA litoke pasipo faida mfano stand ya kibaha nani anaelipia ile dizeli,oil,kulika kwa tairi na spea,na mda unaopotea bus linatoka highway linazunguka kilometa kuitafuta stand iliyopo uchochoroni halishushi halipakii linaingia kulipa ushuru tu KISHA linarudi highway nani analipa hio cost. Stand inatakiwa iwe hatua chache toka highway.
 
Hili ni jambo zuri sana, muda mwingi sana unapotezwa kupita kwenye stendi za Halmashauri na wakati mwingine hakuna abiria wanaopanda au kushuka.
 
Zilijengwa kishamba, matokeo yake nyingi zake zimegeuka kuwa mateso badala ya msaada kwa wasafiri.
Hapo ndiyo tatizo letu waafrika lilipo.

Hizo stend zilijengwa za nini kwa fedha gani?
 
Ukimaliza ujadiri vile tunapoteza muda njiani kisa halmashauri

Kuweni wabunifu
Stand ya lazma iwe ya mkoa na kama ipo njiani la sivyo hapana
Hivi kusafiri ni adhabu?
Ndio maana mnapata maajali yasioeleweka.
Panga Muda wako vizuri, mwezi naondoka nyumbani siku 4 njiani.
2 kwenda 2 kurudi.
Unaenda Mbeya piga nusu route mpk Iringa pumzika.
Kesho mchana huyoo Mbeya ushafika jioni.
Yote ni njaa tu unakuta familia nzima mnapanda kapajero kamoja baba anaendesha mawenge pombe za jana na mchepuko mara kubuum njiani huko hatoki mtu.
Peaneni muda.
Mama tangulia na hawa wawili,mke nenda na wawili, kesho we huyo taratibu na wawili mnakutana kijijini.
 
Kuna mkuu wangu wa wilaya juzi tu alikuwa tunagombana nae ananilalamikia mapato ya stendi yapo chini na gari za mikoani zinapita hapo naomba aone hii tusichoshane
 
Tamko la Waziri wa Uchukuzi Safi sana. Mimi ni miongoni mwa watu wanaochukia basi kulazimika kuingia stendi hata kama hakuna abiria anayeshukia hapo
Ni usumbufu sana na upotevu wa muda tu.
 
... kila halmashauri ina magari ya mizunguko ndani ya halmashauri husika. Hivyo vistendi vya halmashauri vihudumie magari ndani ya halmashauri; isiwe lazima kwa long safari's unless wameona kuna wateja waingie wenyewe na sio kulazimishana.
 
Watanzania mbona mnakuwa mazuzu kiasi hicho? Shida ni nini inayowafanya kushindwa kuelewa hata mantiki ya jambo husika, ni udumavu wa lishe?. Kila kitu wafanyabiashara wadogo, hizo biashara zenu za kulazimishana? Ulipoamua kufanya biashara yako eneo flani hukufanya upembuzi yanikifu? Basi halina abiria wa kushusha na limejaa haitafuti abiria liingie stand kupoteza muda kwa sababu ya kuja kuwachangia wafanyabiashara wadogo? Tumieni akili. Hizo ni stand za Halmashauri km ulivyosema ni kwa ajili ya magari yenu ya wilyani hapo Igunga na ya kwenda mikoa ya jirani ukiwemo mkoa wenu wa Tabora siyo kwa ajili ya mabasi ya masafa yanayopita?
 
Hapo ndiyo tatizo letu waafrika lilipo.

Hizo stend zilijengwa za nini kwa fedha gani?
Hizo stand zilijengwa kwa ajili ya magari yenu huko kwenu. Kwani wilaya ambako hazipiti highway stand zao ni kwa ajili ya nini. Mfani Stand za wilaya za Meatu, Kishapu, Bariadi kutaja chache ambako hakuna highway zinapita zimejengwa kwa ajili ya nini. Nyie Igunga kwasababu mnapitiwa na highway mkafikiri ni kwa ajili ya hayo mabasi? Ujinga changanya na ushamba ni mzigo mzito kuubeba
 
Ndio madhara ya kujenga stand Kwa kukurupuka.

Hata hivyo hizo stand binafsi zinalipia ushuru Halmashauri
 
sawa kabisa na ilele na nane nane Dodoma unaingia kwenye foleni ya magari ya Dar saa nzima ndugu. Kama kweli waziri ametoa huo uamuzi Mungu ambariki sana. Hvi watu wengine wanawaonaje wenzao? Kwa hiyo utesek ili kwenda kumpelekea biashara mwenzio? Mtu unatoka Arusha kwenda Songea, unafika Dodoma saa 7 mchana utatoka saa 8 unusu kisa kwenda kwanza nane nane ambako unakutana na foleni ya mabasi, malori na magari mengine ambayo ni mengi ktk barabara ile.
 
Hapo ndiyo tatizo letu waafrika lilipo.

Hizo stend zilijengwa za nini kwa fedha gani?

Ziliejengwa KUSHUSHA na kupandisha abiria.

Kila Gari linaajent Kwa kila Stend.
Mabasi Kabla hayajaingia Stendi tayari yana taarifa ya idadi ya abiria waliopo kwenye Stendi fulani, au hakuna abiria
Zingatia pia kuwa Kila ajent hufanya juu Chini Kupata abiria ili naye apate Pesa.
Hivyo abiria akifika Stendi hawezi kukosa Gari Kwa sababu maajenti wapo
 
we usipoteze muda wako ujue siyo halmashauri zote nchini zimepitiwa na highways ni chache na je hizo ambazo hazijapitiwa na highways zinapataje mapato ya halmashauri? Wasiwalazimishie binadamu wenzao biashara zao kwa gharama ya kuwapotezea muda wao, huo ni ubinafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…