Mmhh?? Kwm kuna nchi ambayo haina CORONA kwa sasa?? Na tulivyojisahau watz Mungu atuepushe na balaa, watu hawana habari ya tahadhari kabisa.. hakuna kunawa mikono kwa maji tiririka, hakuna kuvaa barakoa, hakuna kutakasa mikono "sanitizer"... yote ya yote, TUSIFIKE KWENYE LOCK DOWN!!!Wizara ya afya Tanzania imesema kuanzia kesho wasafiri wote kutoka nchi zenye maambukizi ya Corona watakaa karantini ya siku14.
Watanzania wanaorudi nyumbani watakaa karantini majumbani mwao.
Source BBC Dira ya Dunia
Tatizo wateule wengi kwenye nchi hii ni maprofesa na madokta....!!Huu ni mtazamo wa kiuchumi kuliko kiafya.
Kwahiyo wageni ndio wana possibilty kubwa ya kuambukiza corona kuliko wenyeji?Kwanini wwnyeji wanaruhusiwa kujitenga nyumbani?
Hivi serikali mnachotafuta kwenye hii janga ni nini,kwanini hamko makini?
Mwaka jana tuliwaambia hamkusikia.
Mwaka huu tunawaambia tena,chukueni hatua za kudhibiti mwingiliano na mataifa yaliyoathirika kama India mapema.
Mnabeba dhamana ya afya zetu sote,nchi si yenu peke yenu,BE STRICT on this issue kwa ajili yetu watu milioni 60!
ACHENI KUJIVUTAVUTA!BE STRICT!😡
Niliwahi kutoa uzi hapo awali kuhusu wave MPYA ya corona kali toka India ambako kuna taarifa kundi la wahindi waliokuepo india linarudi tanzania kukimbia janga jipya la corona cha ajabu serikali yetu ipo kimya bado tumetia pamba masikioni, usafiri na India Uko pale pale huku nchi nyingi zikifuta Safari za kwenda na kutoka India.
Yaani ungeweza kuandika bila kuongeza hiyo paragraph yako ya mwisho ya pizza ungekuwa juu sana..Kuna kitu nyuma ya Pazia kimeanza kutokota
Ili kikiwaka vizuri waseme hatua zilichukuliwa
Lakini mambo bado hayajaharibika sana
Kwa jinsi India kilivyoumana na Hawa wenzetu lazima Itakuwa kuna ndugu zao huko wanasepa kuja Bongo kujificha
India wana hali tete sana sana
All in all, Sijajua kwanini hawa virusi wanawavamia sana ngozi nyeupe
Au wanakula sana Burger, Pizza na vile vitu laini laini kama biscuits na choklate
Mmhh?? Kwm kuna nchi ambayo haina CORONA kwa sasa?? Na tulivyojisahau watz Mungu atuepushe na balaa, watu hawana habari ya tahadhari kabisa.. hakuna kunawa mikono kwa maji tiririka, hakuna kuvaa barakoa, hakuna kutakasa mikono "sanitizer"... yote ya yote, TUSIFIKE KWENYE LOCK DOWN!!!
Well said..Tanzania kwa wananchi waliopo ndani watangazieni watumie barakoa hali sio shwari na iwe lazima hiyo rapid test kazungura iliwachanganya mtu huyo huyo mmoja asubuhi akipima ana corona jioni hana tena ile wave two wakati imekomaa wakaacha kupima wakawa wanabaki kusoma majibu ya kipimo cha UTH Lusaka..inatakiwa kusitisha safari za ndege kutoka na kuingia India au Brazil kama zipo...
Matumizi ya sanitizer au kunawa na kupunguza misongamano isiyo ya lazima..
Kila ofisi au duka iwekwe sanitizer au maji ya kunawa na sabuni..
Kupunguza misongamano kwenye vyombo vya usafiri wa ndani..
Kupunguza misongamano huko polisi..
Watu waache kusalimiana kwa kushikana mikono...
Mechi ya Simba vs Yanga washabiki waruhusiwe wachache tuu..
Kuhamasisha matumizi ya barakoa kuwa ya lazima..
Mkuu hakuna chochote serikali zetu za Africa zinaweza kufanya. Watakaokufa watakufa, na wakaoumwa wataumwa tu. Maisha yetu bora mkono kwenda kinywani, ngono na kungojea kufa. Ni Mungu tu ndo msaada wetu.Why serikali iko kimyaa??
Kuna waraka wametoa. Thread ipo humu.Why serikali iko kimyaa??
Ni kweli mkuu. Sasa serikali isaidie nini jamani. Ni Mungu tu. Na ninamwomba isitokee kama ilivyo india we will perish. Lord help us!Mungu atusaidie tu