Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Yamewakuta kitu gani?

Umelishwa propaganda na wewe unakuja kutufokea humu.

Unalipenda neno kufokewa sana eeh? Umetafuta wapi ulitumie hadi kwa tochi umekosa, mwisho umeona isiwe taabu lazima ulitumie tu?

Hebu onyesha ulipofokewa tujiridhishe kuwa kweli umefokewa.

Kiswahili asili yake siyo usukumani si unalijua hilo?

Hiiiiii bagosha!
 
Corona ipo ninyi endeeleni kufanya dhihaka na jinis ilivyo inaenda kwa level badala ya kuongelea kuwa na mazingira mazuri ya gesi na vifaa vingine eti mnajiona mpo salama...kuendelea kubisha ina maana huko India hakuna Corona ni wasanii tuu na huko Brazil na SA walivyohangaika nayo...
 
Sasa kwanini mnasema mnazuia wahindi wasije wakakimbilia Tanzania ili kukwepa Corona kwao wakati sisi hatukuwa tunachukua Tahadhari means sisi ni kitovu cha Corona, leo imekuwaje tena tuzuie watu kwamba watatuambukiza wakati sisi ndani tayari tunamaambukizi yasiyopimika? Where is the logic? Where is the common sense?

Kwa swali lako ninapata picha ya uelewa wako. Kila mtu ana uelewa wake na hivyo wewe, mimi au yule kuwa na wake si kosa, ujinga wala werevu.

Kutokea hapo juu ninaomba sasa nikujibu maswali yako yote kama ifuatavyo:

Corona kuna mbegu mbali mbali (strains). Kuna cha SA, Tanzania,UK, India nk. Hii ni kama kilivyo kwa kile cha Arusha, cha Tabora nk.

Mbegu zote hizo zina makali tofauti. Mfano cha India ni matata zaidi. Chenyewe hata kwa under 40 na wasio kuwa na magonjwa mengine kinawatoa kamasi kweri kweri.

Unaonaje kama tukiongeza jitihada kidogo zaidi ya kuizuia hii mbegu kutokea India ili kutotuongezea taabu zaidi?

Bado logic wala common sense ya kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya India hauioni?
 
Corona ipo lakini sio Tanzania.
Corona sio ukimwi useme utakaa nao hata miaka 10
Corona ipo ninyi endeeleni kufanya dhihaka na jinis ilivyo inaenda kwa level badala ya kuongelea kuwa na mazingira mazuri ya gesi na vifaa vingine eti mnajiona mpo salama...kuendelea kubisha ina maana huko India hakuna Corona ni wasanii tuu na huko Brazil na SA walivyohangaika nayo...
 
Unapomwambia mtalii/ mgeni akae Karantini kwa siku 14 tafsiri yake ni nini? Kwamba baada ya siku 14 asipoonesha dalili ndio unamruhusu kwenda mbugani, unafikiri kuna mtu anapemda kufungiwa siku 14 tena kwa gharama zake? Kuna chizi wa kuja kuchezea pesa zake hivyo kwa hali ya sasa? Mzungu chizi wa hivyo atoke wapi?
Au kichwa chako kinapata shida kuona uhusiano wa utalii na uchumi?
Kuna wageni wanaotoka baadhi ya nchi sio zote ndio wanaotakiwa kukaa quaranteen. Btw huwa sijjadili hoja na mtu asie na ustaarabu. Uwe na siku njema.
 
Kuna wageni wanaotoka baadhi ya nchi sio zote ndio wanaotakiwa kukaa quaranteen. Btw huwa sijjadili hoja na mtu asie na ustaarabu. Uwe na siku njema.
Kumbe kuna nchi hazina Corona kabisa, siku njema kwa kweli.
 
Kwa swali lako ninapata picha ya uelewa wako. Kila mtu ana uelewa wake na hivyo wewe, mimi au yule kuwa na wake si kosa, ujinga wala werevu.

Kutokea hapo juu ninaomba sasa nikujibu maswali yako yote kama ifuatavyo:

Corona kuna mbegu mbali mbali (strains). Kuna cha SA, Tanzania,UK, India nk. Hii ni kama kilivyo kwa kile cha Arusha, cha Tabora nk.

Mbegu zote hizo zina makali tofauti. Mfano cha India ni matata zaidi. Chenyewe hata kwa under 40 na wasio kuwa na magonjwa mengine kinawatoa kamasi kweri kweri.

Unaonaje kama tukiongeza jitihada kidogo zaidi ya kuizuia hii mbegu kutokea India ili kutotuongezea taabu zaidi?

Bado logic wala common sense ya kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya India hauioni?
Tumeishi bila tahadhari kwa zaidi ya mwaka, bila restrictions za aina yeyote, bila shaka , hizo strains zote tayari tunazo na bahati nzuri miili yetu imeshajua jinsi ya kuishi na hizo strains zote ndio maana huoni purukushani zozote za ajabu mahospitalini, sasa ya nini kununua mwamvuli wakati mvua imeshatulowesha chapachapa na imeshakata? Tena mwamvuli tunaununua kwa pesa ya kula ili tushinde njaa, kama si utaahira ni nini?
 
Hapa tulipo tuna jembe letu tumelirejesha kubakia Chatto milele, ukweli mchungu mno - kwa ugonjwa huu huu na kwa kuzembea kuchukua tahadhari za msingi tu.

Hapa tulipo hatuna uhakika hali iko vipi na tuchukue mwelekeo upi hadi ripoti ya wataalamu itakapokuwa wazi. Kwa maana nyingine kwamba mvua ingali inanyesha, inapungua, imekata au inaomgezeka hakuna ajuaye?

Taarifa za kuwa mvua imekata wewe unazipata wapi? Au wewe uko kwenye hii tume ya mama?

Tuache kupoka mamlaka ya hizi tume wajameni. Sisi sote hatujui tuitie shime tume kutupatia ripoti huru.
 
Serikali ya Tanzania hii leo imetoa mwongozo mpya kuhusu ugonjwa wa corona ambapo wasafiri watakaokuwa wanatoka katika nchi zenye maambukizo ya virusi vipya vya corona watatakiwa kukaa karantini kwa siku 14.

Mwongozo huo uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Profesa Abel Makubi utaanza kufanyiwa kazi rasmi kesho Mei 4 2021, unaeleza kuwa karantini hiyo itawahusu wasafiri ambao ni wakaazi na wageni.

Kabla ya kwenda karantini kwanza watafanyiwa vipimo vya lazima vya corona.

Kwa wageni watatakiwa kukaa karantini kwa gharama zao "watachagua eneo moja katika orodha itakayotolewa na serikali."

Wasafiri ambao ni wakaazi wa Tanzania wataruhiswa kujitenga kwa siku 14 katika nyumba zao wenyewe.

Hatua hizo zitawahusu pia wasafiri ambao safari zao zilipitia katika nchi hizo walau katika siku 14 zilizopita.

Mwezi mei mwaka jana Tanzania iliondoa karantini ya lazima kwa wasafiri kutaka nje ya nchi hiyo na badala yake wakatangaza kuwa kutafanyika vipimo vya ugonjwa huo.

Wizara ya Afya ya Tanzania imeeleza kuwa nchi hizo zenye virusi vipya vya corona zitatambuliwa kupitia taarifa zinazotolewa kila siku na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa sasa virusi vipya vinavyogonga vichwa vya habari zaidi ni vya India na Brazili.

Nchini India hali ni mbaya zaidi ambapo zaidi ya watu 300,000 kila siku hukutwa na maambukizi ya corona.

Wataalamu wanatahadharisha kuwa idadi ya maambukizi inaweza ikawa kubwa zaidi ya hiyo.

Hata Mimi Nimetumiwa huu Ujumbe niko nchi jirani tena yenye Maambukizi Mengi ya Corona mtu kuingia ni Kazi sana ila Mungu Wa Ajabu Niliingia nikapima hapo hapo na kupata Majibu na kupokelewa na Mtu Muhimu kwenye Hiyo nchi hata Sikukaguliwa Mizigo Sasa Sijui Saa ya kuludi itakuwa hivi niko Nawaza Pamoja na hayo "God is Good All the time"

Sent from my SM-N900 using JamiiForums mobile app
 
Wangekuwa wanajilinda wangekuwa na hali hii tuiyonayo? Mbona yaliyojiri hadi hali kuwa mbaya kiasi hiki yako hadharani? JIONGEZE ili ujue nini kinachoendelea kule India.
Kaka kwani India wao HAWAJILINDI?
 
Hapa tulipo tuna jembe letu tumelirejesha kubakia Chatto milele, ukweli mchungu mno - kwa ugonjwa huu huu na kwa kuzembea kuchukua tahadhari za msingi tu.

Hapa tulipo hatuna uhakika hali iko vipi na tuchukue mwelekeo upi hadi ripoti ya wataalamu itakapokuwa wazi. Kwa maana nyingine kwamba mvua ingali inanyesha, inapungua, imekata au inaomgezeka hakuna ajuaye?

Taarifa za kuwa mvua imekata wewe unazipata wapi? Au wewe uko kwenye hii tume ya mama?

Tuache kupoka mamlaka ya hizi tume wajameni. Sisi sote hatujui tuitie shime tume kutupatia ripoti huru.
Hii Corona tunayo na tumeishi nayo, nchi zilizochukua tahadhari za kufungia watu ndani kama India ndio zinazidi kuwa nayo, sasa ni uwendawazimu kuamini kwamba hizi tahadhari leo miaka miwili baadae ndio zitamaliza tatizo, infact tatizo lenyewe halipo hapa kwetu, tunapigana na kivuli kwa kelele za majirani, tuishie hapa.
 
Wangekuwa wanajilinda wangekuwa na hali hii tuiyonayo? Mbona yaliyojiri hadi hali kuwa mbaya kiasi hiki yako hadharani? JIONGEZE ili ujue nini kinachoendelea kule India.
India ile iliyofungia watu ndani kwa bakora? Imekuwaje tena? Au watu waliambukizana ndani ya lockdown?
 
Sawa na hapa Tanzania?
Wangekuwa wanajilinda wangekuwa na hali hii tuiyonayo? Mbona yaliyojiri hadi hali kuwa mbaya kiasi hiki yako hadharani? JIONGEZE ili ujue nini kinachoendelea kule India.
 
Back
Top Bottom