Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
AGNES MARWA AWAHASA WAZAZI KUSEMA NA VIJANA WAO
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Mathew Marwa, ametoa wito kwa wazazi nchini kuchukua jukumu la moja kwa moja katika kuwaelekeza na kuzungumza na watoto wao, hususan vijana, kuhusu umuhimu wa uzalendo, nidhamu, na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Akizungumza na Wakazi wa Musoma Mjini , Mhe. Agnes alisema kuwa vijana wengi wanajikuta wakishiriki katika harakati zisizo na tija kwa taifa kutokana na kukosa mwongozo wa karibu kutoka kwa wazazi na walezi wao.
Aidha, alisisitiza kuwa Taifa linahitaji mshikamano na uwajibikaji wa kila Mtanzania, na siyo kuvuruga amani iliyopo kwa visingizio vya tofauti za kisiasa, kidini au kikabila.
Alimalizia kwa kupongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza taifa kwa busara, maono na moyo wa kujenga mshikamano miongoni mwa Watanzania wote.