GE2025 Ahadi za Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za kwanza za uongozi wake miaka mitano ijayo (2026 -2030)

GE2025 Ahadi za Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za kwanza za uongozi wake miaka mitano ijayo (2026 -2030)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea wa Urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2025 ametoa ahadi zifuatazo katika siku zake 100 za kwanza akiwa madarakani;

1. Marufuku kuzuia miili ya Marehemu hospitalini

2. Bima ya Afya kwa Wazee, Watoto, Walemavu

3. Wagonjwa wa saratani, sukari, figo kugharamiwa kwa aslimia 100

4. Wahudumu 5,000 wa afya kuajiriwa

5. Walimu wapya 7,000 kuajiriwa

6. Bilioni 200 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo

7. Kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya

8. Mawaziri, wakuu wa mikoa kuwajibika kwa wananchi

9. Kurasmisha sekta isiyo rasmi

10. Kuanzisha Gridi ya Taifa ya Maji


Mdau unaona nini itawezekana au vipi??
Katiba katiba katiba ndio muhimu lakini mara zote huwa tunaahidiwa pepo tu lakini uhalisia inakuwa ni jehanam
 
Mgombea wa Urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2025 ametoa ahadi zifuatazo katika siku zake 100 za kwanza akiwa madarakani;

1. Marufuku kuzuia miili ya Marehemu hospitalini

2. Bima ya Afya kwa Wazee, Watoto, Walemavu

3. Wagonjwa wa saratani, sukari, figo kugharamiwa kwa aslimia 100

4. Wahudumu 5,000 wa afya kuajiriwa

5. Walimu wapya 7,000 kuajiriwa

6. Bilioni 200 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo

7. Kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya

8. Mawaziri, wakuu wa mikoa kuwajibika kwa wananchi

9. Kurasmisha sekta isiyo rasmi

10. Kuanzisha Gridi ya Taifa ya Maji


Mdau unaona nini itawezekana au vipi??

IMG_20240428_070927.jpg
 
Anaandika @aman_martins
IMG_1737.jpeg

Hapo Juu ni picha iliyonivutia kutoka katika tukio la Uzinduzi wa Kampeni za CCM. Picha iliyobeba historia kubwa ya nchi yetu inayoambatana na kampeni za mwaka huu: Ni mara ya kwanza kwa Chama Cha Mapinduzi kumsimamisha mgombea mwanamke kuomba Urais, na ni mara ya kwanza mwanamke kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.
.
Nimesikiliza aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea Urais, Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.
.
Katika aliyozungumza, mimi binafsi nimevutiwa na Yale yatayotekelezwa ndani ya siku 100 iwapo CCM itachaguliwa. Kwa ujumla wake na kwa muhtasari, ni mambo 8:

1. Afya: Watoa Huduma 5,000 wataajiriwa, Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote utazinduliwa kwa awamu ya Majaribio na Serikali kubeba gharama Magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wasiojiweza. Lingine lilishongaliwa na wengi ni Marufuku kwa Hospitali kuzuia Miiili ya Marehemu.

2. Elimu: Mkakati Madhubuti wa Kisayansi kuhakikisha wanafunzi Darasa la Tatu wako vizuri darasani na kulipa nguvu hilo na mengine katika elimu wataajiriwa walimu wapya 7,000. Lingine la muhimu ni kuanzishwa kwa Mpango wa Pamoja kati ya Waajiri, Vyuo vya Vya Ufundi Stadi na vyuo vikuu kulinganisha mafunzo na mahitaji ya Sekta za Kipaumbele, itasaidia kuhakikisha kinachofundhishwa kinakidhi mahitaji ya Soko.

3. Bilioni 200 zitakazotengwa kuwezesha upatikanaji wa Mitaji kwa Wafanyabiashara wadogo. Hili linaenda sambamba na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi. Naamini wanangu Mawinga, Bodoboda na Mama Ntilie wanaotujazia ubwabwa kitaa watanufaika.

4. ⁠Kuanza kwa Programu Maalum ya Ujenzi wa Mitaa ya Viwanda Wilayani

5. ⁠Kuanza Utekelezaji wa Ujenzi Wa Gridi ya Taifa ya Maji

6. ⁠Kuendeleza Jitihada za matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

7. Kuanzishwa kwa Mifumo itakayowezesha watendaji wa Serikali kupokea na kujibu kero za Wananchi kwa njia ya Kidijitali. #MamaKasema hicho kitakuwa kipimo kwa Mawaziri wake (Umesikiliza, kujibu na kutatua kero ngapi)

8. Kuwa na Tume ya Maridhiano na Upatanishi, sanjari na kuanza mchakato wa Katiba Mpya.

#Champ. 28/08/2025. Mbezi Beach
 
Ukirudi nyumbani kulala fikiria kero za usafiri na za maisha utakazopitia mpak muda wa kushusha neti kulala.
Halafu uje tena kuandika danganya toto za wanasiasa.
 
Mbona kama ni mambo mepesi sana ukiacha hilo la Afya...
 
Serikali itaanza kugharimia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya Kibingwa kwa Wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo Saratani, Figo, Moyo, Sukari, Mifupa na Mishipa ya Fahamu. Haya ndio magonjwa ya gharama kubwa kwa watu wasio na Uwezo

Hapo kwenye kujua nani ana uwezo na nani hana uwezo wa kugharamia matibabu ya magonjwa hayo ni kipengele.

Ni siasa tu hakuna uhalisia, mgonjwa atafika hospitalini ataanza kuambiwa sijui alete namba ya balozi wake, barua ya mwenyeti nk.

Atazungushwa mpaka ajipange kuipambania roho yake mwenyewe vinginevyo atakufa kwenye mizunguko.

Hapo ni siasa na miyeyusho tu, mkakati wa utekelezaji wake haupo na hakuna uhalisia wowote.

Si huwa wanasema matibabu kwa wazee na watoto chini ya miaka mitano ni bure, lakini hali ikoje?

Tuambizane tu ukweli watu wajipange kujenga maisha yao, tuache uongo.
 
Ndugu yangu Huduma za bima za afya zimeboreshwa muda tu tokea mama ameingia madarakani, nitoe mfano kwenye Bima za Vyuo, kwenye matibabu ya asilimia 100 bima ina cover asilimia 80 tu mtu Ndio anaongezea, kwanza waelewa nini maana ya Bima?
Si kweli Mama amefanya kazi kubwa sana Hadi kufikia hapo wew ni muongo tu
 
AHADI ZA SAMIA NDANI YA SIKU 100 BAADA YA KUCHAGULIWA (ATAKAYOFANYA)​

1. Utazinduliwa rasmi mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote, kwa awamu ya majaribio. Wakianza Wazee, Watoto, Wajawazito, na Wenye Ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi haya zitabebwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

2. Serikali itaanza kugharimia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya Kibingwa kwa Wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo Saratani, Figo, Moyo, Sukari, Mifupa na Mishipa ya Fahamu. Haya ndio magonjwa ya gharama kubwa kwa watu wasio na Uwezo

3. Serikali itaajiri Wahudumu wa Afya Wapya 5,000 ndani ya hizo siku 100, wakiwemo Wauguzi na Wakunga kusaidia zaidi afya ya Mama na Mtoto.

4. Serikali itapiga marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya Marehemu kuchukuliwa na ndugu zao hata kama gharama za matibabu aliyopatiwa marehemu yazijalipwa. Serikali itakuja na mfumo mwingine wa kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama hizo.

5. Serikali itaandaa mkakati madhubuti wa Kisayansi kuhakikisha kila mtoto wa darasa la 3 anaweza kusoma, husebu na kuandika bila shida. Katika kutimizia hilo, Serikali itaajiri Walimu 7000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

6. Uzinduzi wa mpango wa pamoja kati ya Waajiri, Vyuo vya Ufundi stadi (VETA) na vingine na Vyuo Vikuu ili kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta za kipaumbele kama Nishati, TEHAMA, Viwanda vya kuongeza thamani na maeneo kama hayo na kufanya Wanafunzi wa VETA kuchukuliwa viwandani kufanya kazi za mazoezi

7. Serikali itatenga Bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa Wafanyabishara ndogondogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa Kampuni changa (Start-Ups)

8. Tutarasimisha sekta zisizo rasmi yaani Mama Lishe , Maafisa Usafirishaji (Bodaboda), na bajaji na Wajasiriamali wadogo watarasimishwa ili waingie mfumo rasmi wa Serikali waweze kupata huduma zao na kuweza kushirikiana na Serikali

9. Uanzishwaji wa Programu maalimu za Mitaa ya Viwanda Wilayani yenye kulenga kuzalisha ajira kwa Watanzania kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Madini, Misitu na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi

10. Ujenzi wa gridi ya Taifa ya maji utaanza kwa lengo za kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji. Vyanzo ni kutoka Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa pamoja na mito mikubwa

11. Jitihadi za matumizi ya Nishati safi zitaendelezwa ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ili kutunza mazingira

12. Uanzishwaji wa mifumo rafiki ya Uwajibikaji ambapo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa Serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa Wananchi kwa njia ya Kidigitali na SMS za bure. Hiki ndicho kitakuwa kipimo cha Mawaziri - Ameulizwa ngapi, amejibu ngapi na kuchukulia hatua ngapi

13. Tutaendeleza mashauriano na Wadau wa Siasa, Taasisi za Kiraia na Sekta Binafsi, kwa kuunda Tume ya Kuanzisha Mazungumzo ya Maridhiano na Upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Samia amesema "Kwa ujumla kwa miaka 5 ijayo serikali ya CCM imejipanga kuongeza nguvu kwenye ubora wa huduma zinazotolewa kusimamia haki, amani na utulivu wa kisiasa ili tuweze kukuza uchumi na kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa."

Ajira 5000 😹😹😹 Huku wanohitaji ajira ni mamilioni
 
Sawa tumekusikia raisi, Tunachotaka ni utekelezwaji kwa wakati, kama alivyo sema ndugu rostam Aziz
 
Back
Top Bottom