GE2025 Ahadi za Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za kwanza za uongozi wake miaka mitano ijayo (2026 -2030)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Haya bhana kama Bado Kuna watu hawaoni.
Basi hata
Wasiendelee kudanGanyika
 
Siasa bhana.. Utadhani ni ukweli atafanya.

Ila hapo namba 8, watu wanataka waingizwe kweny mfumo wa kulipa kodi
 
...a good politician is the one who promises people about the future, when the future comes he/she promises about another future.

Who cares.
Eti . Si afannye tu kabla ya October tuna tiki?
 
1. Tutaanza rasmi kutekeleza sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Kwa
kuanzia, ndani ya siku 100 tutazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima
ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianzia kwa wazee,
watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za
matibabu kwa makundi haya zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima.

2. Serikali itaanza kugharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya
kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa
yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na
mishipa ya fahamu. Haya ndiyo magonjwa yenye gharama kubwa na
ambayo wananchi wasio na uwezo wamekuwa wakishindwa kumudu
gharama zake.

3. Kuanzia sasa ninapoongea ni marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia
miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zake hata kama gharama za
matibabu za matibabu aliyopatiwa marehemu hajazilipwa.

4. Serikali itaajiri wahudumu wa afya wapya 5,000, wakiwemo wauguzi na
wakunga, ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.

5. Tutaanda mkakati madhubuti na ya kisanyansi kuhakikisha kila mtoto
wa darasa la tatu anaweza kusoma, kuhesabu na kuandika bila shida.

6. Tutazindua mkataba (National Skills Compact) wa kitaifa wa ujuzi kwa
viwanda – mpango wa pamoja kati ya waajiri, vyuo vya ufundi stadi
(TVETs) na vyuo vikuu kwa lengo la kulinganisha mafunzo na mahitaji
ya sekta kipaumbele, kuanzia na nishati, TEHAMA, na viwanda vya
kuongea thamani.

7. Tutaajiri walimu wapya 7,000 wa masomo ya hisabati na sayansi.

8. Nitazindua Mfuko wa Ajira kwa Vijana na Wanawake wenye wa thamani
ya shilingi bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya
biashara ndogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa kampuni
changa.

9. Nitazindua programu maalum ya kurasimisha sekta isiyo rasmi kwa
mama lishe, usafiri na usafirishaji na wajasiriamali wadogo.

10.Tutaanzisha programu maalum ya ujenzi wa mitaa ya viwanda kwa kila
wilaya yenye kulenga kuzalisha ajira kwa watanzania kupitia kuongeza
thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na misitu, pamoja na
vifaa vya ujenzi.

11.Tutaanza utekelezaji wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa lengo la kuwa na
vyanzo vya uhakika vya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo,
mifugo na biashara. Gridi ya Taifa ya Maji itahusisha vyanzo vikubwa
vya maji kutoka maziwa: Victoria, Tanganyika, na Nyasa, pamoja na
mito mikubwa nchini.

12.Tutazindua miradi ya haraka ya nishati, ikiwemo umeme vijijini kwa
kutumia nishati jadidifu (solar, wind), nishati safi ya kupikia. Hatua hii
itapunguza utegemezi wa kuni na mkaa na kuhifadhi mazingira.
13.Kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na zege
katika maeneo ya mijini na vijijini.

14.Tutaanzisha mfumo rafiki ya uwajibikaji ambapo mawaziri, wakuu wa
mikoa na watendaji wengine wa serikali watatoa taarifa na kujibu
maswali kutoka kwa wananchi kwa njia ya kidijitali na SMS bure.

15.Kuanzisha mazungumzo ya wadau wakiwemo asasi za kiraia, viongozi
wa dini, wafanyabiashara na vyama vya siasa ya kuhuisha na
kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.
 
HATUA 15 KATIKA SIKU 100 ZA MUHULA WA PILI WA SAMIA SULUHU
HASSAN KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CCM YA 2025 - 2030
kuanzia, ndani ya siku 100 tutazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima
ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianzia kwa wazee,
watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za
matibabu kwa makundi haya zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima.
kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa
yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na
mishipa ya fahamu. Haya ndiyo magonjwa yenye gharama kubwa na
ambayo wananchi wasio na uwezo wamekuwa wakishindwa kumudu
gharama zake.
3. Kuanzia sasa ninapoongea ni marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia
miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zake hata kama gharama za
matibabu za matibabu aliyopatiwa marehemu hajazilipwa.huyu ndoo mgombea URAIS KUPITIA CHAMA CHA CCM# HAIJAPATAKUTOKEA🇹🇿🇹🇿
 
Attachments

  • Screenshot_20250828-214645_Google.jpg
    Screenshot_20250828-214645_Google.jpg
    156.3 KB · Views: 28
  • Screenshot_20250828-215023_Google.jpg
    Screenshot_20250828-215023_Google.jpg
    211.8 KB · Views: 28
HATUA 15 KATIKA SIKU 100 ZA MUHULA WA PILI WA SAMIA SULUHU
HASSAN KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CCM YA 2025 - 2030
kuanzia, ndani ya siku 100 tutazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima
ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianzia kwa wazee,
watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za
matibabu kwa makundi haya zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima.
kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa
yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na
mishipa ya fahamu. Haya ndiyo magonjwa yenye gharama kubwa na
ambayo wananchi wasio na uwezo wamekuwa wakishindwa kumudu
gharama zake.
3. Kuanzia sasa ninapoongea ni marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia
miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zake hata kama gharama za
matibabu za matibabu aliyopatiwa marehemu hajazilipwa.huyu ndoo mgombea URAIS KUPITIA CHAMA CHA CCM# HAIJAPATAKUTOKEA[emoji1241][emoji1241]
SIASA TU.

Waajiri watumishi wa afya maana kazi zinatulemea sana aisee wagonjwa wengi kuliko wahudumu.
 
Anaweka ahadi muhumu ya kugharamia makundi muhimu kupitia bima ya Afya kwa wote.
N.B
mwaka 2015 niliwahi kuhoji wagombea Urais kupitia ukurasa huu huu wa JF Kuhusu bima ya afya kwa wote.
Kamwe sitaacha kuulizia na kuishinikiza Serikali,Vyama na wadau wote husika kuliweka sawa swala hili la bima ya Afya kwa wote.
Nimefurahi kuwa Mhe .Rais na mgombea wa CCM anaendelea kulitaja wakati huu wa kampeni.ni mategemeo yangu pia kila mgombea kwa nafasi yake aseme malengo yake kuhusiana na swala hili.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Tarehe 7/09/2017 ukiwa African Dreams Dodoma chumba namba 302 uliagiza vijana 4
 
AHADI ZA SAMIA NDANI YA SIKU 100 BAADA YA KUCHAGULIWA (ATAKAYOFANYA)​

1. Utazinduliwa rasmi mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote, kwa awamu ya majaribio. Wakianza Wazee, Watoto, Wajawazito, na Wenye Ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi haya zitabebwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

2. Serikali itaanza kugharimia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya Kibingwa kwa Wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo Saratani, Figo, Moyo, Sukari, Mifupa na Mishipa ya Fahamu. Haya ndio magonjwa ya gharama kubwa kwa watu wasio na Uwezo

3. Serikali itaajiri Wahudumu wa Afya Wapya 5,000 ndani ya hizo siku 100, wakiwemo Wauguzi na Wakunga kusaidia zaidi afya ya Mama na Mtoto.

4. Serikali itapiga marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya Marehemu kuchukuliwa na ndugu zao hata kama gharama za matibabu aliyopatiwa marehemu yazijalipwa. Serikali itakuja na mfumo mwingine wa kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama hizo.

5. Serikali itaandaa mkakati madhubuti wa Kisayansi kuhakikisha kila mtoto wa darasa la 3 anaweza kusoma, husebu na kuandika bila shida. Katika kutimizia hilo, Serikali itaajiri Walimu 7000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

6. Uzinduzi wa mpango wa pamoja kati ya Waajiri, Vyuo vya Ufundi stadi (VETA) na vingine na Vyuo Vikuu ili kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta za kipaumbele kama Nishati, TEHAMA, Viwanda vya kuongeza thamani na maeneo kama hayo na kufanya Wanafunzi wa VETA kuchukuliwa viwandani kufanya kazi za mazoezi

7. Serikali itatenga Bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa Wafanyabishara ndogondogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa Kampuni changa (Start-Ups)

8. Tutarasimisha sekta zisizo rasmi yaani Mama Lishe , Maafisa Usafirishaji (Bodaboda), na bajaji na Wajasiriamali wadogo watarasimishwa ili waingie mfumo rasmi wa Serikali waweze kupata huduma zao na kuweza kushirikiana na Serikali

9. Uanzishwaji wa Programu maalimu za Mitaa ya Viwanda Wilayani yenye kulenga kuzalisha ajira kwa Watanzania kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Madini, Misitu na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi

10. Ujenzi wa gridi ya Taifa ya maji utaanza kwa lengo za kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji. Vyanzo ni kutoka Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa pamoja na mito mikubwa

11. Jitihadi za matumizi ya Nishati safi zitaendelezwa ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ili kutunza mazingira

12. Uanzishwaji wa mifumo rafiki ya Uwajibikaji ambapo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa Serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa Wananchi kwa njia ya Kidigitali na SMS za bure. Hiki ndicho kitakuwa kipimo cha Mawaziri - Ameulizwa ngapi, amejibu ngapi na kuchukulia hatua ngapi

13. Tutaendeleza mashauriano na Wadau wa Siasa, Taasisi za Kiraia na Sekta Binafsi, kwa kuunda Tume ya Kuanzisha Mazungumzo ya Maridhiano na Upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Samia amesema "Kwa ujumla kwa miaka 5 ijayo serikali ya CCM imejipanga kuongeza nguvu kwenye ubora wa huduma zinazotolewa kusimamia haki, amani na utulivu wa kisiasa ili tuweze kukuza uchumi na kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa."

Miaka 4 toka 17-03-2025 MSD na upotevu wa Madawa , NHIF toka kuwa na Bima ya watoto, mpaka kuifuta kabisa, na ripoti za siegi zisizo jadiliwa Bungeni, na Sethi kuachiwa na kulipwa hela zake na kuja kuchangia sisiemu. Ili watu mange zaidi
 
mungu ambariki Rais Samia
 
Kilichomkwamisha kufanya hayo kwa miaka MINNE ni nini? Nguvu za kufanya kwa siku 100 zitatoka wapi na zilikuwa wapi? NIJIBIWE VIZURI TAFADHARI
 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonesha dhamira thabiti ya kulinda afya za Watanzania wote kwa kuanzisha Mfuko Maalum wa Bima ya Afya utakaowahakikishia watoto, wazee na wajawazito kupata matibabu bila gharama.

Umuhimu kwa Taifa

Mfuko huu utalinda makundi yenye uhitaji mkubwa, kupunguza umaskini unaotokana na gharama za matibabu, na kuhakikisha kila raia anaishi maisha yenye afya na tija.

Ni hatua kubwa ya kujenga usawa na mshikamano wa kijamii, ikionesha kwamba serikali chini ya Dkt. Samia ni ya watu na kwa ajili ya watu.

#haijapatakutokea
#haijapatakutokea
 
Watanzania tuna kila sababu ya kumpa kura za NDIYO Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Ameendelea kuthibitisha kuwa afya ni kipaumbele kikuu katika Taifa letu kwa kusema:
“Tutazindua rasmi Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianza na wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi hayo zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.”
Hatua hii ni ushahidi wa dhamira yake ya kuijali jamii, kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya bila ubaguzi.

#haijawaikutokea
#ikulumawasiliano
#Oktobatunatiki
#ccmtanzania
 
Attachments

  • 9c3608a2-0b5e-4a6a-b20a-8f4f6f902369.mov
    8.1 MB
Tanzania ya Samia inaenda kuondoa changamoto za Afya kupitia Bima kwa wote.

Huu ndo wakati sahihi wa kummininia Kura Mh Rais
 
Huo mfumo usitegemee. Ungefanya utafiti kwa waliotangulia nao. Wajawazito na majeruhi ndo hunufaika na mfumo huo. Maradhi mengine, utaongea muda ukifika.
 
Back
Top Bottom