GE2025 Ahadi za Mgombea Urais CCM, Samia Suluhu Hassan kwa siku 100 za kwanza za uongozi wake miaka mitano ijayo (2026 -2030)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Siku 100 za Rais Samia katika awamu ya pili zimeweka kipaumbele cha kipekee katika afya ya wananchi. Kupitia uamuzi huu wa kimkakati, Serikali inagharamia kikamilifu matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza yenye gharama kubwa kama Figo, Kisukari, Saratani, Moyo na Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu. Hatua hii inaleta mapinduzi ya kijamii kwa kuondoa mzigo wa kifedha uliokuwa ukiwakwamisha wananchi wasio na uwezo. Ni dhihirisho kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inawajali watu wake na inalinda maisha yao. Huu ni ushahidi wa uongozi wa kizalendo unaoweka afya ya Watanzania mbele ya yote.
.
.
#haijawahikutokea
#tukawashangaze
 
Attachments

  • IMG-20250828-WA0801.jpg
    IMG-20250828-WA0801.jpg
    154.9 KB · Views: 31
1. Nitazindua Rasmi mfumo wa Bima ya afya kwa wote (wazee, watoto, wamama wajawazito na walemavu), pia serikali itagharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vikubwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyo ambukizwa ( saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na mishipa ya fahamu.

2. Serikali itaajiri wahudumu wa afya wapya 5000 ndani ya siku 100.

3. Tutapiga marufuku hospital yoyote nchini kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa.

4. Tutahakikisha kila mtoto wa darasa la 3 anasoma na kuandika bila shida, tutaajiri waalimu 7000 kwa masomo ya hisabati na sayansi.

5. Tutatenga fedha kiasi cha bilioni 200 ilikuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na wakati na kuwezesha kampuni changa.

6. Bodaboda na mama lishe watalasimishwa

7. Tutaanzisha program maalum ya ujenzi mitaa ya viwanda wilayani yenye kuzalisha ajira kwa watanzania kupitia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, Uvuvi , madini na misitu.

8. Ujenzi wa gridi ya Taifa ya Maji

9. Tutaendeleza jitihada za matumizi safi ya nishati ya kupikia hatua ambayo itapunguza utegemezi wa kuni na mkaa.

10. Tukiongozwa na Falsafa ya 4rs tutaendeleza mashauliano na wadau wa siasa na kuazisha tume ya mazungumzo, maridhiano na upatanishi na kuanda mazingira ya kuanza mchakato wa katiba Mpya.

11. Kuongeza nguvu kwa huduma ya kusimamia haki amani na utulivu wa kisiasa ilituweze kukuza uchumi na maendeleo kwa ustawi wa taifa letu.
 
Maana yake Kila kituo mtaletewa EFD muonje utamu wa kulipa Kodi
 
Kwa ufupi,hawatajisumbua kutengeneza ajira bali watavizia waliojiajiri wawe wanawaorodhesha tu.Ni kama kusubiri njiapanda kukusanya ushuru kutoka kwa wauza mchicha na maembe pori.
 
AHADI ZA SAMIA NDANI YA SIKU 100 BAADA YA KUCHAGULIWA (ATAKAYOFANYA)​

1. Utazinduliwa rasmi mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote, kwa awamu ya majaribio. Wakianza Wazee, Watoto, Wajawazito, na Wenye Ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi haya zitabebwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

2. Serikali itaanza kugharimia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya Kibingwa kwa Wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukiza, ikiwemo Saratani, Figo, Moyo, Sukari, Mifupa na Mishipa ya Fahamu. Haya ndio magonjwa ya gharama kubwa kwa watu wasio na Uwezo

3. Serikali itaajiri Wahudumu wa Afya Wapya 5,000 ndani ya hizo siku 100, wakiwemo Wauguzi na Wakunga kusaidia zaidi afya ya Mama na Mtoto.

4. Serikali itapiga marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya Marehemu kuchukuliwa na ndugu zao hata kama gharama za matibabu aliyopatiwa marehemu yazijalipwa. Serikali itakuja na mfumo mwingine wa kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama hizo.

5. Serikali itaandaa mkakati madhubuti wa Kisayansi kuhakikisha kila mtoto wa darasa la 3 anaweza kusoma, husebu na kuandika bila shida. Katika kutimizia hilo, Serikali itaajiri Walimu 7000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

6. Uzinduzi wa mpango wa pamoja kati ya Waajiri, Vyuo vya Ufundi stadi (VETA) na vingine na Vyuo Vikuu ili kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta za kipaumbele kama Nishati, TEHAMA, Viwanda vya kuongeza thamani na maeneo kama hayo na kufanya Wanafunzi wa VETA kuchukuliwa viwandani kufanya kazi za mazoezi

7. Serikali itatenga Bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa Wafanyabishara ndogondogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa Kampuni changa (Start-Ups)

8. Tutarasimisha sekta zisizo rasmi yaani Mama Lishe , Maafisa Usafirishaji (Bodaboda), na bajaji na Wajasiriamali wadogo watarasimishwa ili waingie mfumo rasmi wa Serikali waweze kupata huduma zao na kuweza kushirikiana na Serikali

9. Uanzishwaji wa Programu maalimu za Mitaa ya Viwanda Wilayani yenye kulenga kuzalisha ajira kwa Watanzania kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Madini, Misitu na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi

10. Ujenzi wa gridi ya Taifa ya maji utaanza kwa lengo za kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji. Vyanzo ni kutoka Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa pamoja na mito mikubwa

11. Jitihadi za matumizi ya Nishati safi zitaendelezwa ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ili kutunza mazingira

12. Uanzishwaji wa mifumo rafiki ya Uwajibikaji ambapo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wengine wa Serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa Wananchi kwa njia ya Kidigitali na SMS za bure. Hiki ndicho kitakuwa kipimo cha Mawaziri - Ameulizwa ngapi, amejibu ngapi na kuchukulia hatua ngapi

13. Tutaendeleza mashauriano na Wadau wa Siasa, Taasisi za Kiraia na Sekta Binafsi, kwa kuunda Tume ya Kuanzisha Mazungumzo ya Maridhiano na Upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza kwa Mchakato wa Katiba Mpya.

Samia amesema "Kwa ujumla kwa miaka 5 ijayo serikali ya CCM imejipanga kuongeza nguvu kwenye ubora wa huduma zinazotolewa kusimamia haki, amani na utulivu wa kisiasa ili tuweze kukuza uchumi na kuleta maendeleo na ustawi wa Taifa."

Form 4 failure, mwenye PhD ya kupewa. Hapo tutegemee miaka mitano ya utekaji, wizi wa rasilimali, and much more. Mungu tuepushie hili balaa.
 
Wa

Uongo wakubwa
 
Ukitaka kumuweza mtz kwenye Jambo lolote lile mpe maneno mengi, risala ndefu Hadi kuisoma au kuisikiliza itamchosha then ondoka, ukiondoka wengi watakuwa washasahau na hata wanaokumbuka hawana uwezo wa kujiuliza chochote. Primitive robotic system.
 
Nina file la CCM limenifikia, wasiponipa namimi posho nayabwaga kama polepole
 
Back
Top Bottom