Ahmed Rajab akosoa historia ilivyoandikwa na Dr.Ghassany!!

Na umemsahau MS. na Mohamed Saidology yake

..wazee wake Mohamed Said waliteswa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

..kwa hiyo mimi wala sishangai yeye kumuandika Nyerere vile ambavyo anafanya.

..pamoja na hayo mimi nakushauri usimuite majina ambayo siyo mazuri.
 
Last edited by a moderator:
Mkirua,
Huenda wewe ni kuku mgeni hapa Majlis...
Ikiwa maana hujaielewa muulize Maalim Faiza.

Mohamed Said nawasoma sana tu. Sina kamba mguuni.
Nimeshangazwa namna mnavyoshindwa kujibu swali rahisi sana mnabaki tu kuruka ruka jukwaaani.
Baado tunauliza....Ni halali au si halali?
 
Mohamed Said nawasoma sana tu. Sina kamba mguuni.
Nimeshangazwa namna mnavyoshindwa kujibu swali rahisi sana mnabaki tu kuruka ruka jukwaaani.
Baado tunauliza....Ni halali au si halali?

Mkirua,
Ukitaka uwe mtu wa kuheshimiwa na uwe msomi makini chunga lugha yako.
Lugha, "kurukaruka," ni matusi, kejeli na kebehi.

Nitakufunza adabu ya mjadala.
Ingekuwa mie ni wewe swali hilo ningeliliuliza hivi:

"Mohamed Said nimeshanga namna mnavyoshindwa kujibu swali hili rahisi
mimi nakuomba utuoe jibu...ni halali au si halali?"
 
Mohamed, umeona kauli za Mkirua tu, vijana wako wakiporomosha mitusi unawapa like.

Mzee Said, tunajukumu la kulea vijana

Haya watu wameelewa ‘’adabu’’, Mkirua kauliza, ni Mapinduzini halali au ni haramu?
 
Ritz pia kaomba niweke ushahidi.

Nina waasa muachane na hoja hiyo. Mnatambua huwa sisemi bila ushahidi, Mohamed Said kaka kimya hajaomba niweke ushahidi. Anachowaambia ni kuwa achanane na hayo


Narudia, mkitaka ushahidi muwe tayari kumsiitiri mzee.

Nimeamua kumkumbusha Mzee Said, nisingependa tuanze kuvuana nguo.

Mnajua wazi nina uwezo huo. Waungwana tuache ‘jibwa lililo lala lilale'
vingienvyo msije kuniona mbaya. Nawa nasahi sana!

Mzee Said, je, ungependa nifungue makabrasha yangu hapa Magila, Muheza?

Unakumbuka hapo nyuma nilifungua makabrasha kwambi la Ritz yaliyonyofolewa na panya na mengine uchagoni. Kilichofuata ni dhahma!

Mimi sipendi kufungua,unanishauri vipi?
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,
Hivi unajua kuwa kwa CCM Zanzibar wameshindwa uchaguzi mara tatu?
Sasa hayo mapinduzi yanayolindwa ni yapi?

Umemsikia Mzee Moyo kasema nini kuhusu uchaguzi wa 2005?

Yani unaulizwa lingine unajibu usichoulizwa..!! sasa wewe mwanazuoni huko ambapo huwa unatowa/wasilisha papers ndio huwa unawajibu hivyo!!??
 
Yani unaulizwa lingine unajibu usichoulizwa..!! sasa wewe mwanazuoni huko ambapo huwa unatowa/wasilisha papers ndio huwa unawajibu hivyo!!??

Remote,
Hamaki zinaondoa fikra njema.
Ikiwa wewe unanitambua mimi ni mwanachuo basi ni wazi umeniweka juu.

Ikiwa hivyo ndivyo ikiwa nakuja na swali ambalo wewe kwa haraka linakujia
limekuja sipo inatakiwa ujiulize: "Kwa nini huyu mtu wa hadhi hii kafanya hivi,
kuna ujumbe gani anataka kufikisha?"

Taratibu tutaelekezana na tutaelewana In Sha Allah.
 

Nguruvi3,
Hapa ni mahali pa mjadala wala si mahali pa "kuvuana nguo."
Hapa wala si mahali pa matusi na kukashifiana.

Hapa tunashindanisha hoja.

Ikiwa una majalada ambayo yatanogesha hoja zako na Majlis itanufaika kwa
nini nikuzuie kufanya hivyo?
 
Mohamed, umeona kauli za Mkirua tu, vijana wako wakiporomosha mitusi unawapa like.

Mzee Said, tunajukumu la kulea vijana

Haya watu wameelewa ''adabu'', Mkirua kauliza, ni Mapinduzini halali au ni haramu?

Nguruvi3,
Mimi sina mtu hapa Majlis nachangia kama anavyochangia mtu mwingine yoyote yule.

Pili siwezi kuunga mkono matusi na ikiwa una ushahidi wa mie kuunga mkono matusi
ulete tafadhali.
 
Baada ya kusoma, ukaweka ‘like' ukiunga mkono matusi

 
Baada ya kusoma, ukaweka ‘like' ukiunga mkono matusi


Kama unauliza swali la kijinga ukaambiwa hivyo ni matusi?

Unapozuwa uongo ukaweka maneno yako bila ushahidi, ukaambiwa ulete huo ushahidi ukashindwa, ukaambiwa wewe ni fataani ni matusi kikwenu?

Hizo ni sifa mbaya ulizonazo, si matusi hayo - kumbuka hilo.

JF kuna kanuni kali kabisa, wakiona matusi hawastahamili amma wanaifuta post amma wanakulamba ban - kumbuka na hilo pia.
 

Huko mimi nnakuita kubwabwaja na kuhororoja bila mpango, eti "ungependa nifungue makabrasha yangu".

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Umewahi kumsoma Mshume Kiyate katika historia ya kudai Uhuru Tanganyika?
 
Mohamed, umeona kauli za Mkirua tu, vijana wako wakiporomosha mitusi unawapa like.

Mzee Said, tunajukumu la kulea vijana

Haya watu wameelewa ''adabu'', Mkirua kauliza, ni Mapinduzini halali au ni haramu?

"halali au haramu", "sahihi si sahihi", "sawa au si sawa", haja/hujayaona majibu yake huko juu? au mnachokisoma hamkielewi?

Hivi wewe unaonaje "halali au haramu"?
 
Mohamed Said nawasoma sana tu. Sina kamba mguuni.
Nimeshangazwa namna mnavyoshindwa kujibu swali rahisi sana mnabaki tu kuruka ruka jukwaaani.
Baado tunauliza....Ni halali au si halali?

Wewe hebu tusaidie jawabu, sisi tumeshindwa kujibu swali lako gumu sana Dah!

Hapo sasa!
 

Hapo ndipo mnapokosea kila mara,siku zote mnaingiza mara sheria/kanuni za dini kwenye mambo yasiyohusu dini.Mnakwepa maswali ya msingi kwa kuweka uwongo wa dini hapa hakuna dini itasalimika na uwongo.Nikutakeni yote wenye hyo kariba ya kuchanganya dini na mada zisizo dini mwache huo ujuha,tufanye mijadala na tujibu maswali bila kukwepa kwa kutumia vigezo vya kidini.
 

Nini maana ya "dini"?
 
Meneno mengi hata kwenye kanga tumezoe kuyasoma leta ushahidi .
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…