Pre GE2025 Ahobokile Mwaitenda anusurika kuuawa kwa kuukosoa mkataba wa bandari!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tusipokuwa makini hata mlima Kilimanjaro siku moja atauziwa mwarabu. Tuna viongozi washamba sana


Tunataka BANDARI zetu tulipigania Uhuru Kwa kutaka Mali zetu Leo Samia MANGUNGO anagawa Kwa waarabu , DPWORLD waondoke
An assassination of the government critics is not a proper or permanent solution to the problems that are facing the country. The proper solution is to find the proper ways of solving or eliminating the problems themselves, but not eliminating people.
Badala ya kuondoa matatizo wnaondoa watu.
Waingereza wana msemo wao kwamba "barking up the wrong tree".
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Mlinda legacy hata LISSU aliposema anafuatiliwa na gar flan na no flan mlimbeza na kumwambia anatafuta umaaruf kupitia JPM. Nadhan baada ya masaa kadhaa mliona wenyew!!! NB: Kwann walinda legacy wengi ni hamnazo?
Kwanini mtuletee filamu za hollywood!
 
Kick tu wameshindwa waua au taka waua kina Mbowe, Lissu wamtafute mtu ambaye hajulikani
 
Wanaokoswa kuuliwa ni wanyakyusa tu ,ebu acheni drama za kitoto na ushamba wenu.
 
Huu ndio uaskofu na utumishi uliotukuka.

Mwanakondoo ameshinda
 
Inabidi tujiulize Kwenye hili kama tumechambua Both Economical and Social consequences za kuendelea na hili jambo ?

Na je suala hili lina manufaa kwa wote au kuna watu wanajali their personal economical benefits ? Dinari kadhaa kwa watu kadhaa zisijetuachia makovu ambayo tiba yake itachukua muda...

Hili jambo lina figisufigisu nyingi sana mbaya zaidi na huu usiri uliopo; It makes you wonder... maybe, just maybe what Ndugai Said was True....,
 
Dalili ya mvua ni mawingu. DPW ikiingia hapa tanzania ni umafia umeingia. Hii kampuni italeta ubeberu wa moja kwa moja nchini. Concempt yao ni kupora kwa nguvu mali asili ya nchi changa kama vile bandari. Watanzania watambue kama nchi tumewekeza na tunawekeza sana. Sgr na mpango mzima wa kuhakikisha tunateka afrika ya kati na mashariki yote kutumia pwani yetu kama lango uko mlangoni kuzaa matunda. Mara DPW wanatokea kupitia vibaraka waliyohongwa eti tukabidhi bandari zetu wao ndio wavune faida..eti sisi hatuwezi kuendesha bandari zetu. Ni uendawazimu gani huu.
 
Watekaji wakamlazimisha kuingia Kwa gari akawa mateka..
Halafu akaendesha gari peke yake huku wanamfata??
Labda atakuwa amekosea kiuandishi maana mwenyewe sijaelewa pale.
 
Huyo si ni mdogo wake Dr. Ulimboka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…