Haki ni suala la katiba na sheria wala siyo mtazamo wa mtu binafsi.
Siyo kila utamaduni ni utamaduni mzuri.Kusema asante pale unapopewa haki yako siyo jambo sahihi wala siyo jambo zuri.
Wenye akili timamu tunakataa kushukuru pale ambapo mtu unapewa haki yako kwa sababu hili litamfanya anaetoa haki aone kuwa kutoa haki ni mapenzi yake au ni kudra yake au ni hisani yake au ni hiari yake wakati suala la kutoa haki ni la lazima kwa sababu lipo kwa mujibu wa katiba na sheria.
Hili suala la viongozi wetu kuona kuwa kutupa haki zetu ni mapenzi yao limesababisha waongoze nchi hii kwa kudra na hisani yao badala ya kuongoza kwa mujibu wa katiba na sheria.
Suala hili limesababisha viongozi wetu kuona kuwa katiba siyo chochote wala lolote kwa sababu watu kama ninyi mmeshawafanya viongozi wetu waone kuwa kutupa haki zetu ni hiari yao na wala siyo takwa la katiba.