Ahukumiwa kuchapwa viboko 6 kwa kosa la ubakaji

John Emmanuel (18) Mkazi wa Kijiji cha Malangi Babati Vijijini amekutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu kuchapwa viboko 6.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Mariam Lusewa ikibainishwa kuwa Sheria ya Hukumu hiyo inaeleza kama Mvulana mwenye umri wa miaka 18 au chini ya hapo ikiwa kosa lake ni la kwanza hukumu yake ni kuchapwa viboko.

Chanzo: Azam TV
Hizi taarifa za ubakaji zimekuwa nyingi sasa katika jamii.
 
Kama alifanya kosa akiwa under age mbona hakupelekwa Juvenile court?

Sasa Panya road si ndio umri wao huo? Nao wawe treated under Juvenile?

Tunahitaji marekebisho ya sheria ziendane na wakati na uhalisia.
Hivi wewe umekazana kutetea panya Road, wewe ndiyo sponsor wao nini,maana unaumia sana wanavyokamatwa?
 
Mahakama ya mkoa Manyara imemhukumu John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ya kesi namba 73 ya mwaka 2021 imetolewa leo Septemba 26,2022 na Hakimu mkazi mkoa wa Manyara Mariam Rusewa.Hakimu Rusewa ameiambia mahakama hiyo kuwa Emmanuel alimbaka mwanafunzi wa darasa la nne (13) Septemba 10,2021 katika kijiji cha Malangi.

Kwa mujibu Kifungu cha 131 (2) cha sheria namba 16 kinaeleza kuwa, Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini; Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu ambapo hakimu ataamua ni viboko vingapi.

Chanzo: Mwanzo TV
Angembaka binti yangu na mimi ninge.....😡
 
hakimu amutumia hekma sana aisee..ukilinganisha umri wa aliyebakwa na mbakaji ...unaweza kuta mbakaji ana umbo dogo kuliko aliyebakwa...na huenda alimtega mwenzake
 
Mahakama ya mkoa Manyara imemhukumu John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ya kesi namba 73 ya mwaka 2021 imetolewa leo Septemba 26,2022 na Hakimu mkazi mkoa wa Manyara Mariam Rusewa.Hakimu Rusewa ameiambia mahakama hiyo kuwa Emmanuel alimbaka mwanafunzi wa darasa la nne (13) Septemba 10,2021 katika kijiji cha Malangi.

Kwa mujibu Kifungu cha 131 (2) cha sheria namba 16 kinaeleza kuwa, Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini; Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu ambapo hakimu ataamua ni viboko vingapi.

Chanzo: Mwanzo TV
Kwa nini kumchapa binadamu mwenzio?

Ahukumie miaka/miezi ama/na hela. Viboko sio kitu na ni ubinadam.
 
Huyu angeshitakiwa kama mtum mzima.... umri sio namba tu, umri ni majukumu... kama kaweza kubaka, ni mtu mzima huyo!
 
Viboko sita vile sio mchezo mtu anakunya kabisaa 😄😄😄
Acha utani aisee.
Nakumbuka sisi tulikuwa tunalala chini alafu wanapita walimu kama saba hivi wanapiga bila kuhesabu zaidi ya tanotano hivi na wanarudia karibu saa nzima. Ukitoka hapo sio chini ya 50 alafu wakati mwingine kosa hatukufanya sisi.

Hivyo vibakora sita mwanaume unapigwa bila hata kufuta wala kugusa, hausikii chochote yaani.
 
Mzee ile stick ya kule ni maalumu acha kabisaaaa, weka mbali na watoto.. Hizo za shule mnapalazwaa tu 😄😄
 
Kuna ticha mmoja misifa alikuwa anajulika shule nzima anapiga kiunoni kudadadeki.
Sasa imagine bakora size ya kidole gumba ishuke kiunoni kwa nguvu zote za mtu mzima.

Hujawahi kupitia maisha ya kipigo aisee.
 
Nimeishi na kulelewa kijeshi kweli kweli school sikuwa napata tabu, home unapigwa na mkandaa wenyewe ule, unafungwa kambaa unabamizwaaa, na hiyo huli chakula, ukifunguliwa kamba cha kwanza wana test umeelewa mapigo au vipi, unatumwa kuchota maji 😄😄😄😄😄 stick za hukumu ya mahakama achana nazo zile sio fimbo za kawaida
 
Mzee alikuwa mjeshi hiyo bakora ya jeshi alikuwa nayo ni ya kawaida sana ukilinganisha na magongo ya shule.
Rumors tu lakini mimi naona maumivu ndio yaleyale.
 
Acha utani aisee.
Nakumbuka sisi tulikuwa tunalala chini alafu wanapita walimu kama saba hivi wanapiga bila kuhesabu zaidi ya tanotano hivi na wanarudia karibu saa nzima. Ukitoka hapo sio chini ya 50 alafu wakati mwingine kosa hatukufanya sisi.

Hivyo vibakora sita mwanaume unapigwa bila hata kufuta wala kugusa, hausikii chochote yaani.
Zajela hazifananishwi zile zinaitwa henzilani watu wanapelekwa cuba kusomea kuchapa unazan utan

Sent from my DRA-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom